Jamii ya Mungu ambayo ndio muumba wa anga yote, na ambayo iko na wenyeji wawili kwa sasa, yaani, neno , na Mungu- Yohana.1:1-3, inaishi yale maisha ambayo yameorodheshwa katika biblia( kwa maelezo zaidi, soma ujumbe, “Mungu wa pekee wa kweli”). Baada ya muda Fulani, hiyo jamii iliamua kuongeza wenyeji wake, kama wanavyoeleza katika hayo maandik yao wakisema, “…waliazimia kuwaleta wana wengi katika utukufu- Waebr.2:10”. Je walikuwa watekeleze nia yao kwa njia gani? Walisema, “ Natuumbe mtu kwa mfano wetu, na kwa sura yetu(aliye kama sisi- miungu-Yohana.10:34), ili waitawale Dunia-Mwa.1:26”. Rafiki, mimi na wewe ni wenyeji watarajiwa wa jamii ya Munguikitegemea uamusi wetu wa kuishi kama wao na kuumbika hizo tabia zao, ambazo zinaitwa uhaki na utakatifu-ona Waebr.12:14. Baada ya Mungu kuanza mpango wake kwa kumuumba mzazi wetu wa kwanza(Adamu), Alimweka katika Dunia hii ambayo inatawaliwa na Shetani(mpinzani wa chote kiitwacho Mungu- soma ujumbe, “Shetani ni nani?”). Adamu katika ujinga wake alidanganyika, na kuchagua maisha maovu ambayo ndiyo ulimwengu wa leo. Kinyume na maisha ya jamii ya Mungu ambayo tuliumbwa tuwe washirika wake, ambayo yameunganishwa na akili moja, aina moja ya maisha, roho moja- ndio, kila kitu, kimoja( soma-Yohana.5:19-20; 10:30; 17:21), Wazao wa Adamu walianza maisha yalio kinyume na yale ya Mungu; maisha ya kugawanyika, kuchukiana, kubishana, kupigana, wakigawanyika kwa mamilioni ya vikundi ambavyo kila kimoja kina njia yake. Lakini kwa vile Mungu ana kusudi lake kwa mwanadamu, na ni lazima aitimize, Amekuwa kila wakati kupitia kwa wateule wake(manabii na mtume,ambayo ujumbe wao ndio Biblia),akijaribu kumujulisha mwanadamu hiyo kusudi lake. Angalia kutoka Ibrahimu, Waisraeli, na sasa, kanisa lake.Hawa wote wamekuwa ni mpango wa Mungu wa kumfunulia mwanadamu ile kusudi lake la kumuumba. Hii anafanya, kwa kuwafundisha awa watumishi wake hayo maisha ya kweli, na kupitia kwa kuyaishi, wanaonyesha kwa vitendo, yale maisha ya upendo, kujikana, umoja na ushirikiano ambayo huwafanya wote wanaoyashiriki kuwa jamii moja(kama ilivyokuwa kusudi). Lakini Shetani naye,upande ule mwingine amekuwa akiwadanganya wanadamu kila wakati Mungu anapowafunulia huu ukweli. Siku hizi za mwisho, jamii ya Mungu, kupitia kwa mmoja wao, ambaye ndiye Bwana na mwokozi wetu, Yesu kristo, Mungu amewaita watu ambao waliyakubali hayo maisha yake, na saa hii, wanaendelea kujifunza kuyaishi. Hawa ndio ambao aliwafanya kuwa Kanisa lake. Ni ya nini? Ili, hali wakiendelea kuyaishi hayo maisha, wawe mfano(sio kwa Wakristo tu) kwa watu wote, “…..wa ule mpango wa siri silizofichwa tangu enzi za zama, kwa Mungu aliyeviumba vitu vyote-Waef.3:9-10”. Ndio, hii kanisa inapaswa kuwaonyesha(kuwa nuru) watu wote,yale maisha ambayo Mungu alikusudia kwa wanadamu, maisha yale ya upendo katika jamii moja ya Mungu, “.. kwa kuwa kitu kimoja, kama vile mimi na wewe tuko, wawe wamoja ndani yetu, ili ulimwengu upate kujua….” “…..ili, wakiwa na upendo wao kwa wao, ulimwengu upate kujua-Yohana.17:21;13:35”. Lakini, Shetani naye aliliingilia kanisa kupitia kwa maajenti wake( soma matendo.20:29-31), ambao uleta migawanyiko( ona Yuda.1:19); ambao waliligawanya kanisa kwa haya makundi yanayotofautiana huku wakijiita kanisa, ili waikozeshe kusudi la Mungu la kuonyesha upendo na umoja ambao jamii lake uishi kwayo, na kuonyesha kanisa kuwa sawa na ulimwengu ambao unaishi maisha yake. Bwana wetu anasema haya kuhusu haya makanisa; “ Hawa ni wa ulimwengu, na wanaoyanena ni ya ulimwengu, na ulimwengu uwasikiza-1 Yohana.4:5”. Kanisa la Mungu sasa hivi limedanganyika na kugawanyika kwa huu mfano wa shetani kama ulimwengu ulivyo. Hii ni baada ya, “..kupotoka kutoka kwa ule msingi wa kuunganisha lililojengwa juu yake-2 Wathes.2:3”. Kanisa limemtupa Yesu waliyemkubali wakati waliamini ujumbe wake,na ambaye alianza kuishi ndani ya mioyo yao- Yohana.14:23. Hii ni kwasababu, saa hii, anaonekana nje ya mioyo yao, “..akibisha-Ufu.3:20”. Kwa hivyo, limechukua maumbile ya Dunia hii, ile ya kugawanyika,na ushindani, na hivyo, limewacha kufanya ile kazi Mungu alilijenga lifanye, ile ya kuonyesha ulimwengu maisha ya upendo na umoja.
Kwa sababu hii, kama ilvyo tabia ya Mungu ya kutuma wajumbe wake kila wakati Shetani anapopotosha huu mpango wa ushuhuda wake, yuko hapa saa hii kupitia kwa huu ujumbe akirejesha mpango wake kwa msingi, na wakati huu, ni kwa mara ya mwisho. Kristo ameunua watumishi wake ambao sasa hivi, ni “…agano kwa watu(kanisa), na nuru kwa mataifa( ushuhuda kwa wote)- Isaya.42:6”. Ulimwengu sasa hivi uko katika giza kuu-soma Isaya.60:1-3, maana watu wamewacha ule msing ambao maisha yao yamejenga juu yake. Hawa watumishi, ambao ujumbe wao ndio huu unaousoma saa hii wanatangaza ujumbe wa malaika was aba kwa kanisa la Leodikia, huku wakiushuhudia na kuuonyesha ulimwengu wote, yale maisha ya kweli. Kristo analikusanya Kanisa lake kupitia kwa huu ujumbe, ili wakiwa kundi moja waweze kuushuhudia ulimwengu kwa mara ya mwisho, yale maisha aliwapangia wanadamu wote, maisha ya upendo na umoja. Anabisha, “….milangoni ya mioyo ya waumini-Ufu.3:20”, maana anataka, “…kuwasafisha kwa maji kupitia kwa neno, ili apate kujiletee kanisa tukufu lisilo na mawaa-Waef.5:26-27”. Sio kazi yetu kuketi pamoja kupanga vile tutaungana. Sio kazi ya mmoja wetu kushawishi wenzake wamfuate, au waunge mkono maoni yake. Ni Kristo, akiishi ndani ya moyo wa kila atakayekubali huu ujumbe wake(neno lake), ambaye atatuunganisha ndani yake,na hivyo auonyeshe ulimwengu kile alichowaumba wanadamu wote wafanye, ambacho ndicho kitakachokuwa katika huo ufalme wake unaokuja. Umoja wa hili kanisa la pekee la Mungu uja kwa njia la kila mshirika kuishi katika neno binafsi, ambao kwa njoa hiyo, maisha ya upendo na akili moja ya Mungu itaumbika ndani ya kila mmoja, na ambayo yatawafanya waumini wakose kitu cha kutofautiana wala kubishania. Hivyo, hayo maisha, yakiwa ndani ya ila mmoja yatawafanya waumini kuwa mwili mmoja pasipo unafiki, maana, “ wote watakubaiana,pasiwe mgawanyik kati yao; watakuwa na akili moja, na uamuzi mmoja- 1 Wakr.1:10”. Wandugu, Haya mahubiri ni ya Kristo mwenyewe, akifanya hii kazi la kulirejesha kanisa kwenye msingi. Usituamini sisi. Chukua Biblia yako na uchunguze ili kuthibitisha kama sisi ni watu tunajfanya ama kwa kweli, ni Kristo anaongea ndani yetu. Ukishaa thibitisha, usitugeukie sis, mgeukie Yule anayenena ndani yetu, yaani ,mwokozi wetu Yesu.Shirikiana nasi katika kumtazama yeye ambaye peke yake, ndiye awezaye kukuumba ata akufanye kiumbe wa kiroho, na kukupa sehemu katika ufalme wake wa milele unaokuja. Nafasi imewekwa hapa, tayari kwa kila anayetamani kuurithi uzima wa milele. Fuatilia na kusoma maujumbe yote katika huu mtandao, ili uweze kuelewa kikamilifu.
“ Ikiwa mapenzi yako ni kuyafanya mapenzi ya Mungu, basi utaelewa kama mafundisho yetu yanatoka kwa Mungu au, tunaongea kwa uwezo wetu wenyewe-Yohana.7:17”.
WASILIANA NASI KUPITIA KWA,
KANISA LA MUNGU.