Mungu ni roho. Hawezi kuonekana au kueleweka kupitia kwa hii akili ya kimwili isipokuwa iwe imeongezewa uwezo mwingine wa kiroho. Bwana wetu ambaye ndiye peke yake amewahi kuwa mbinguni mahali Mungu anaishi, na ambaye ndiye Mungu alimtuma kwa wanadamu ili awajulishe kusudi la maisha, anayathibitisha haya tunayosema hapa akisema, “ Mwanadamu wa asili hawezi kuyapokea mambo ya kiroho; maana hayo kwake ni ujinga, wala hawezi kuyaelewa, maana yanaeleweka tu kwa jinsi ya kiroho-1 wakor.2:14”. Kulingana na huo ukweli, wengi wa waalimu wa Biblia, wamewavunja moyo wanafunzi wao, kwa kuwaambia eti wao hawawezi kuielewa biblia peke yao bila kuwategemea hao waalimu. Wao uwaambia eti maandiko ni ya kiroho na ni lazima mtu afunuliwe na mwalimu na si aelewe tu kwa kujisomea. Kwa kuchukua huo msimamo, hawa waalimu wamefaulu kuchanganya biblia mpaka sasa, ni kama maandiko hayamaanishi vile yanasema. Kulingana nao, ni kama lugha ya biblia, iwe ni kiingereza au Kiswahili haimaanishi vile inafaa kumaanisha. Eee, ni kama hiyo lugha sasa sio ile ya kawaida maana ni ya kiroho. Hii ni kweli? Ni kwa nini hawa waalimu wanajibidiisha kubadili maana ya lugha Fulani eti tu kwasababu imetumika kwa biblia? Manabii, na mitume wote ambao waliongea na kuandika wakiongozwa na Yesu kuptia kwa roho takatifu– 2 Petro.1:20-21, walionya vikali kuhusu watu watakaokuja wakitumia akili zao kujaribu kutafsiri maandiko (ambayo Kristo mwenyewe anatuambia haiwezekani) huku wakidai eti ni ufunuo wa kiroho. Hao, tunafaa kuwaangalia wasije wakatutega nyara na madhanio ya akili zao fupi-Mat.24:5; 2Pet.3:15-16; 1Tim.1:6-7; Juda.1:19; Mhubiri.12:12; wakolo.2:8. Hao watu ndio wanaotumiwa na Shetani , “….kuwadanganya watu kwa maneno yao yenye onyesho la unyenyekefu-Warum.16:17”. Lakini Mungu, kwa upendo wake mkuu, ule ule aliokuwa nao akimtoa mwanae Yesu, yu hapa tayari akionyesha njia ya wokovu kwa wote wanaotaka kuziepuka nyavu za hawa maagenti wa shetani. Je, wewe ni mmoja wao? Kama ndiyo, tunakusihi utahadharike na kuuusoma huu ujumbe kwa makini sana, huku ukiwa na biblia yako mkononi kuthibitisha kila unachokisoma, maana haya ndiyo maelezo ya pekee ya kukuwezesha kuuepuka, “…ufisadi ulioko duniani sasa hivi kwa sababu ya tamaa za mwili-2 Petro.1:4”. Ni kwasababu ya hawa wafisadi wa kiroho, kifungu kimoja cha biblia kinaweza kuwa na tafsiri nyingi kama vile wanachokitafsiri walivyo wengi. Kwa hivyo, ningeomba sasa, hali tukiwa na hiyo tahadhari, tuendelee na ujumbe wetu.
BIBLIA NI YA NINI?
Ni nini cha dhamana katika biblia hata tuwe na haja ya kuisoma kila wakati? Si ni kitabu tu kama vile vingine? Ya nini tukizingatie sana hivyo? Kama muumbaji mwenye hekima, Mungu alipotuumba, alimwelezea Adamu kwa undani, kusudi la kuumbwa kwetu, na kile tunapaswa kuwa tukifanya katika haya maisha, hata na kile tutakuwa mwishowe. Hii alifanya kwa kuongea naye hana kwa hana, na baadaye akaongea na watu aliowachagua (manabii), maana anasema, “kwa njia mbalimbali, Mungu zamani aliongea na baba zetu kwa njia ya manabii- Waeb.1:1”. Baada ya kuona vile wanadamu walivyo wasahaulifu, na wa kugeuzwa na Shetani kwa haraka( ujumbe wetu, “Huyu ni shetani” unao maelezo Zaidi), Mungu aliwaagiza hawa manabii na kuwaambia, “Haya, enendeni mkayaandike, myachore kwa kitabu, ili yawe ushuhuda kwa vizazi vyote milele-Isa.30:8”. Yanakuwa ushuhuda upi? Kama vile tulivyoanza kuona, sisi ni bidhaa ya muumbaji mwenye hekima, maana anasema, “Mimi niliiumba Dunia, na kumuumba mwanadamu juu yake- Isa.45:12”. Kwa hivyo, fahamuni ya kuwa biblia ni maelezo ya Mungu kwa wanadamu kuhusu maisha aliyowaumba waishi kwayo, na vile yanapaswa kufuatiliwa. Mungu mwenyewe ndiye alianzisha uandishi wa biblia kwa kuandika vifungu vile vya kwanza juu ya mawe huko mlima Sinai, maana, “alipomaliza kuongea na Musa pale mlima Sinai, alimpa zile tembe mbili za ushuhuda, tembe za mawe, ambazo aliziandika kwa kidole chake mwenyewe-Exod.31:18”. Ni kutoka Kwa hivi vifungu kumi (amri kumi), manabii, Na baadaye mitume, walizifafanua zikawa biblia nzima. Kuthibitisha kwamba biblia ndio mwongozo wa maisha yetu, Bwana wetu anasema, “…ni uhai kwa wale wazishikao; maisha marefu yamo kwa mkono wake wa kiume, na kwenye mkono wa kushoto humo utajiri na heshima….; ni mti wa uzima; wingi wa masiku na miaka, wema wa maisha zitakupa-Mith.4:22; 3:16,18,2”. Mbona ahadi nyingi za wema mtupu katika hizi amri za Mungu? Kwa njia rahisi ni kwamba, Mungu anatuambia, “Niliwaumba muishi vile ninavyowaeleza katika maandiko ya biblia”, maana anazidi kusema, “ Mimi ndimi Bwana Mungu wako, akufundishaye kufaidi, akoungozaye kwa ile nja ikupasayo kuenenda kwayo-Isa.48:17”. Kufikia hayo maelezo, sidhani sasa kunaye kati yetu ambaye bado haamini kuwa maandiko ni mwongozo wa maisha aliotupa muumba wetu. Hali tukiyajua hayo basi, ni nini kiroho cha haya maandiko? Eee, kiroho cha biblia ni gani?
MWANZO MBAYA
Mungu alimuumba mwanadamu awe mshirika wa jamii yake, yaani, awe mtoto wa hiyo jamii, akiwa mungu kama vile Mungu alivyo-Yohana.10:34. Lakini mwanadamu alidanganyika kabla Mungu hajamaliza kumuumba. Hivyo basi, kwa kufuata uongo, mwanadamu alijitenganisha na Muumba wake, na akaanza kuishi maisha ya kudhania tangu hapo mpaka sasa hivi ninavyoandika huu ujumbe. Ni maisha gani hayo ya kudhania? Mwanadamu alikubali uongo wa kuwa, “….yeye ni kama Mungu-Mwa.3:4-5”. Kulingana na huo uongo, mtu ni mkamilifu, Mungu amemuumba kikamilivu,; kwa hivyo ana maumbile na ufahamu wa kumwezesha kuishi vile Mungu huwa anaishi bila kumtegema. Baada ya mwanadamu kuukubali huu uongo, Mungu alimkumbusha akamwambia, “Mtu awaye yote asijidanganye.Mtu akijifikiria kuwa mwenye hekima (kwamba anajua) katika hiki kizazi, na ajijue kuwa mjinga (akubali hajui), ili apate kuwa na hekima(aweze kusoma)-1 Wakori.3:18-19”. Mungu anaendelea kuthibitisha kwamba ufahamu wa kweli upatikana kwa neno lake peke yake, maana nje ya hiyo neno, anashangaa, “ Mtawezaji kusema, ‘sisi tu wenye hekima’…….ikiwa wamezikataa amri za Mungu, basi wanao hekima gani-Yerem.8:8-9?” Ni kwanini kusiwe na hekima nje ya amri za Mungu? Hii ni kwasababu maisha yameumbwa kulingana na vile hizo amri zinaelezea na hivyo, hakuna mahali pengine tunaweza kupata maelezo yake, maana, “…hizi amri ndizo hekima na ufahamu wako”; kwa maana, kumcha Mungu ndio hekima, na kuwacha dhambi ndio ufahamu-Kumbu.4:6; Ayubi.28:28”. Sheria ya Mungu ndiyo maelezo ya vile mtu anaweza kufanya, ndio awe mwenye hekima, na kwa hivyo, kuzitii ndio thibitisho pekee yakuwa mtu ana hekima na ufahamu. Wakati adamu alizikataa Na kukubali kuwa ako sawa pasipo kuzifuata, ilimbidi, aukatae ule msingi ambao aliumbwa juu yake na kujijengea wake mwenyewe. Sasa niambie tafadhali; mtu akijaribu kubadilisha msingi wa nyumba iliyotayari, ni kitu gani kitafanyika? Ni wazi kwamba ,lazima aibomoe hiyo nyumba kwanza. Hivi ndivyo Adamu alifanya na ndivyo wote wasiofuata neno la Mungu katika kuishi kwao wanavyofanya; jambo ambalo limechangia kuleta ule uovu tunaouona duniani leo. Hii ndio sababu Mungu anatukumbusha kwamba, “…baba zetu walirithi uongo, maisha ambayo ndani yake hamna faida yeyote, ni uharibifu mtupu-yerem.16:19-20”. Basi hii inamaanisha kwamba, kila kitu mwanadamu atendacho, na kufanya akidai ana ufahamu kinatokana na huu uongo. Kulingana na huo uongo, mtu hafi, ni kama Mungu. Na watu wote (isipokuwa wale wachache ambao wanaendelea kufumbuliwa macho) wameuamini huu uongo. Hii ndio sababu, Kwa mazishi utasikia wahubiri wakisema kuwa, wanayemzika pale ameitwa na Mungu, na kwa hivyo, hajakufa; ameama kutoka huu mwili na hii dunia akaenda Mbinguni. Na kwa vile Shetani ni mjanja, na anao uwezo wakujibadilisha, na kujipa sura au sauti ya wale waliokufa, basi ametumia huu uwezo kuthibitisha uongo wa kuwa mtu hafi- 1 Sam.28:11. Pia, kulingana na uongo huo, inaaminika kwamba mtu ni kuwili, yaani ni kiumbe wa kimwili na pia roho; kwamba huu mwili ni nyumba ya huyo wa roho. Na kwa vile basi mtu ni kama Mungu, kufuatana na huu uongo ,anao uwezo wa kujitengenezea ufahamu bila kufuatilia mwongozo wa neno la maandiko(mwongozo wa pekee wa maisha). Hii ndio sababu, hatuoni watu, ata wengi wa wakristo, wakiwa na bidii ya kuyasoma maandiko katika jitihada la kufahamu vile wanapaswa kuishi na kutenda mambo. Kama vile tumeona, kile watu ufanya ni kudhania, na kuishi kulingana na hayo madhanio. Baada ya kutumia hayo madhanio, mwanadamu uenda hatua nyingine ya kudai eti hayo madhanio ni ufunuo wa Mungu kupitia kwa roho takatifu iliyo ndani yao. Basi hii uwafanya pia, wakubali uongo wa kuwa, mtu akiisha ingia kwenye hivi vikundi wanaita makanisa, kwa vile amekuwa kiumbe wa roho, basi ameokoka na pia amezaliwa mara ya pili, huku wakitumia vibaya kifungu kile yesu alisema, “kilichozaliwa na roho ni roho-Yohana.3:6”. Haya yote ni madhanio na ndio sababu huwezi kuyapata katika maandiko. Ni kwa sababu hii, hawa wahubiri wamejaribu kuyaunganisha madhanio yao na vifungu vya maandiko, ikiwa ni jitihada la Shetani ya kudanganya watu kuwa, hayo madhanio yako kwa biblia, na ni maisha ya Mungu.
UJANJA WAFUNULIWA
Akili ya mwanadamu haikuumbwa na ufahamu, wala haina uwezo wa kufahamu pasipo kufundishwa. Lazima ipate ufahamu kutoka mahali, kasha huo ufahamu uhifadhiwa katika roho( sio roho takatifu) ya akili zetu, na huu ufahamu ndio utumika katika kila jambo afanyalo mtu; ndio sababu Yesu anasema, “Mti ujulikana kwa matunda yake( yaani, akili ujulikana kwa ule ufahamu ulio ndani yake)…..maana kutoka ndani ya moyo, mtu uongea(na hivyo, mwili utenda ya moyoni pia)- Mat.12:33-34”. Hali tukiyajua hayo, fahamuni na kuelewa kwamba, wakati Adamu aliumbwa, hakuwa mtakatifu wala muovu. Alikuwa afanyika kile atachagua- ndicho kingeumba ufahamu ndani yake. Hapa, akili yake ilikuwa tupu, lakini ikiwa tayari kupokea ule ufahamu utakaotokana na kile atachagua (ujumbe wetu, “Kusudi la huu mwili”, unao maelezo Zaidi, usome tafadhali). Ijapokuwa kunao roho ndani ya mwanadamu, hiyo roho aitengenezi ufahamu-Ayubu.32:8. Kazi yake ni kuhifadhi ufahamu ule mwanadamu anaopata kutoka nje, iwe ni kwa kufundishwa na mtu, kujisomea kwa vitabu au kwa Experimenti. Hii uleta uwezo wa kumbukumbu katika akili ya mtu( na ndio tofauti iliopo kati ya akili ya mtu na ya mnyama). Kwa hivyo, kile Adamu alichagua ndicho kilihifadhiwa katika akili yake, na ndicho kilimpa ufahamu alioutumia kuishi vile aliishi. Ile roho ambayo uingia katika akili ya mwanadamu baada ya ameichagua kwa kupenda kwake, ndiyo uunganika na roho ya akili yake, na ule ufahamu utokanao na hiyo roho, huo ndio humpa mwanadamu kuishi vile anaishi, maana imeandikwa, “ni roho yenyewe ishuhudiayo pamoja(ikiunganika) na roho zetu…..Warum.8:6”. Ijapokuwa hiki kifungu kinaongelelea kuhusu roho ya Mungu, hii ufanyika tu kwa wale ambao wamechagua kuongozwa na Mungu. Lakinii pia, hii ufanyika kuhusiana na roho ya Shetani kwa wale wanaochagua maisha yake, maana pia wao upokea roho ya Shetani ambayo uunganika na roho yao kushuhudia kuwa, wao ni, “… wana wa kuasi- Waef.2:2”. Kumbuka, bila roho nyingine kuunganika na roho ya mwanadamu ili impe ufahamu, mwanadamu hana ufahamu mwingine wala maisha yake mwenyewe; hii ndiyo sababu( kulingana na uchaguzi wetu), “ aitha sisi ni watumwa wa dhambi iletao mauti au, ni watumwa wa utiivu uletao uhaki na Amani-Warum.6:16”. Mtu akiisha fanya uchaguzi, basi yule roho ambaye amechagua uweka ufahamu wake ndani ya akili ya aliyeichagua. Kuanzia hapo, hiyo akili upata uwezo wa kufahamu yale tu ambayo hiyo roho inailetea. Chochote kingine nje ya hiyo roho huwa akieleweki na wala hakikaribishwi, maana uchukuliwa kama uongo. Wapenzi, hiki ndicho kiroho cha biblia. Sio kile wengi huwa wanafikiria. Kiroho cha biblia ueleweka kuhusiana na ile roho ambayo imeunganika na roho ya akili ya mtu kuipa ufahamu. Ni huu ufahamu utokanao na ile roho iliyounganika na ile ya mtu ambao uamua kile mtu ataita uongo au ukweli. Ikiwa mtu amepokea roho ya Shetani, basi, hakuna kitu kingine kitakubalika wala kueleweka ndani ya akili yake isipokuwa kile roho ya Shetani itamfunulia. Kwasababu hii, utakubaliana nami kwamba, sio lugha ya biblia iliyo ya kiroho, au iliyo na maana tofauti na vile lugha umaanisha, mbali ,ni ule ufahamu mtu alionao unaotofautiana na ule ulioko katika biblia, ambao unamfanya asiukubali wa biblia, na wala asiuelewe maana tayari ana ufahamu mwingine uliyotofauti na huo wa biblia.
WACHA KUDHANIA
Kwa hivyo, wakati Adamu alimkubali Shetani, “…ile roho( iliyounganika na roho ya akili yake kumpa ufahamu) itendayo kazi katika wana wa kuasi-waef.2:2”, alikataa ufahamu wa Mungu, ufahamu kumhusu yeye mwenyewe, na kuhusu yale maisha anapaswa kuishi, chaguo ambayo wazao wake leo wanashikilia. Kwasababu hiyo, “… wakijidanganya kuwa na ufahamu, wamekuwa wajinga-Warum.1:22”. Maana Bwana wetu anayashuhudia haya anaposema, “…hakuna ajuaye, hakuna afahamuye; wote wamepotoka…warum.3:9-12”. Kwa hivyo, kiroho cha biblia sio kuhusu kile ile lugha imetumika kuiandika inasema, mbali ni kuhusiana na kama ile roho iliyo ndani ya akili ya mtu inayompa ufahamu ni ile iliyoandika ufahamu uliyo katika biblia. Maana kama roho ya biblia itakuwa tofauti na roho iliyo ndani ya akili, basi ufahamu wa Mungu, mwanadamu, na maisha kwa ujumla ambao unaelezwa katika biblia utatofautiana na ule ufahamu wa Mungu, mwanadamu, na maisha unaoelezwa na huyo roho wa udanganyifu. Tukiangalia Kwa macho yaliyofunuka, tutakubaliana kuwa Shetani hakuanzisha maisha yeyote Yale, na hii ni kwasababu, yeye hakuumba kitu chochote. Kile yeye ufanya, na ndicho alimfundisha mwanadamu ni kupinga kila kitu kitokanacho na Mungu (na hii ni katika jitihada la kumwelekeza mwanadamu vibaya ili ajitumie vibaya afe)-2 Wathes.2:3-4. Huu ndio ufahamu unaofanya kazi ndani ya mwanadamu, na hauwezi kufanya kitu kingine chochote kile isipokuwa kile kinapinga kila ufahamu wa biblia. Sasa fikiria na akili iliyo wazi ikiwa unaweza, na ikiwa wewe ni mmoja wa wale wanaofunuliwa, au wanaoendelea kufunuliwa macho. Kwa vile tunajua kwa kweli adamu alikubali uongo, na huo uongo ndio ulimwengu unatumia leo kama ufahamu kuishi vile unaishi, kweli, tunatarajia mwanadamu ajifahamu baada ya kukubali uongo kwamba yeye ni kama Mungu? Eee, baada ya kukubali kwamba yeye hafi? Atatumia roho gani ikiwa tayari amejawa na roho nyingine ambayo inapinga ile yenye ufahamu wa kweli? Kiroho cha biblia kinahusu kubadilisha ile roho iliyo ndani ya akili, ili hiyo roho jipya iweke ufahamu tofauti na ule uliopo, ambao ndio huu unaelezwa katika biblia(soma Waef.4:22-24). Kiroho cha biblia hakimaanishi kubadilisha maana ya lugha inayotumika, mtu akijaribu kuifanya iseme vile haijasema, hii ikiwa ni jitahada la Shetani la kuifanya biblia iseme ule uongo wake maana tayari, mtu ameukubali na ndio umejaa akilini mwake, na sasa, kwa kujaribu kugeuza vifungu vikubaliane naye, anataka kudanganya eti huo utofauti ni ufunuo wa Mungu kwa lugha hiyo ya biblia lakini yenye maana ya kiroho iliyo ya ndani Zaidi. Ukweli ni kwamba, hakuna maana ya ndani Zaidi, ya lugha yeyote ile. Lugha ni namna ya mawasiliano, na ni ya kujielewesha, na sio kujificha. Ukweli ni rahisi hivi; kunao maana iliyo wazi, iwe ni uongo, au ukweli katika kile lugha isemacho. Kwa hivyo, kama mtu amepokea roho ya uongo na kukubali huo uongo, atauita ukweli. Basi roho ya ukweli ikimjia kumfumbua macho ili ajione na kuwacha uongo, hatakubali. Atauita huo ukweli uongo mpaka siku ile atagundua kwamba amedanganyika. Hiki ndicho kiroho cha biblia; kwamba, kunao “roho (yule azipatiazo akili zetu ufahamu) ambayo uunganika na roho zetu kushuhudia (kutufahamisha) kuwa sisi ni watoto wa Mungu(na kama ni watoto wa Mungu, lazima tufundishwe na yeye-Yohana.5:19). Na vivyo hivyo, kunayo roho ya Shetani( ile ipatiayo akili zetu ufahamu wa uongo) ambayo uunganika na roho zetu kutudanganya kuwa sisi tayari ni kama Mungu( na kama Mungu, basi sisi ni wakamilivu, na hatuitaji Mungu wala neno lake kuishi). Tunajua kuwa, Mungu alituumba tuwe watoto wake, na kwamba, bado hajamaliza kutuumba. Pia, Mungu anaelewa kwamba tunahitaji roho yake ili tuweze kumwelewa, kuyaelewa maisha yake, tuweze kujielewa, na kuyaelewa yale maisha alituumba tuishi kwayo. Anayathibitisha haya anaposema, “hakuna mtu awezaye kuyafahamu mawazo ya Mungu isipokuwa roho ya Mungu- 1 Wakor.2:11”. Sasa jameni, huyu ni nani anataka kufanya yasiyowezekana; Kujaribu kutumia roho ya Shetani kuyaelewa mambo ya Mungu? Ama hatujui kuwa maandiko ya biblia ni neno la Mungu mwenyewe aliyotumia watu kuiandika, ambao waliokuwa wakitumia roho yake-2 Pet.1:20? Tafadhali, amkeni, mtoke usingizini, na mwache farakano, na kumwomba “..aliyeagiza nuru iwe, ili aagize hiyo nuru iweze kuangaza mioyoni mwenu, angao, nuru ya injili ya utukufu ya Kristo iweze kufunuliwa kwenu- 2 Wakor.4:6”. Kwa maana kweli, Mungu ananena wazi wazi kuwa, “ Ni lazima tupokee roho ya Mungu ili tuweze kuyaelewa yaliyo ya Mungu(biblia)-1 Wakor.2:12”. Sasa, kwa vile ni Mungu aliyoyaandika maandiko akiwatumia watu ambao walikubali kupokea roho yake, ambayo ndiyo “..akili ya Kristo-1 Wakor.2:16”, basi, kila mtu ambaye amepokea roho ya Mungu atayaelewa maandiko na kuyakubali kikamilifu bila jitihada lolote ile la kujaribu kuyageuza, maana nje ya hayo maandiko, huyu mtu hawezi kuwa na ufahamu mwingine, kwa njia lile ile ambayo mwenye kupokea roho ya uongo hawezi kuwa na ufahamu mwingine isipokuwa huo uongo. Tukiyakubali hayo, basi utakuta biblia ni kamilifu na ni wazi kabisa na haiwezi kuhitaji nyongeza yoyote( somo letu liitwalo, “wapi pa kuanzia”, litakuelezea kwa undani).
CHAGUA SASA
Sisi zote tumeelimishwa katika huu uongo wa Shetani, na kwa hivyo, tunajua vile asemavyo kutuhusu na kuhusu maisha yetu. Huku kumjua kumewesekana kwasababu tulipokea roho yake, ikatufundisha huo uongo wake, “….maisha ya uongo ambayo yamefarakana kwa sababu ya tamaa za mwili( soma ujumbe uitwao “ kusudi ya mwili”, upate maelezo kamili)-Waef.4:22”. Kwa hivyo, ikiwa tunataka kufuata maisha ya muumba wetu kama yanavyoelezwa na biblia, eleweni kwamba, hakuna kitu tunaweza kuchukua kwa hayo maisha ya Shetani na kuchanganya na hayo ya biblia. Hii ni kwasababu, yamejengwa juu ya ufahamu ambao “…..umetiwa giza(hauna ufahamu) na kutenganishwa na Mungu kwasababu ya upuusi ulio ndani yake,na kwa sababu ya ugumu wa mioyo uletwao na huyo roho wa upinzani- waef.4:18”. Rafiki zangu, je, kweli tunataka kuwa watu wa kiroho, na kuyaelewa mambo ya roho wa kweli? Kama ndiyo, basi tuwache kujaribu kubadilisha maana ya vifungu katika maandiko. Yakubali vile yasemavyo, na ukijikuta hauambatani na vile yanasema, husijaribu kuyabadilisha, jibadilisha wewe; usijaribu kuyabadilisha maana hautaweza, kwa kuwa, ni rahisi mbingu na nchi kupita kuliko nukta moja ya torati kubadilika-Mat.5:17. Basi je, tumefikia wapi? Kiroho cha biblia ni gani? Ni rahisi hivi; kubali vile isemavyo, maana ukitaka kuthibitisha kuwa huko ndani ya Yesu, au unamjua, au unaongozwa na roho, “ jiangalie kama unachokishika ni amri zake-1 Yohana.2:3, 5-6, 24; 3:24”;Yakubu.1:24-25. Na hii uwezekana tu kwa wale ambao akili zao zimepokea roho ya Mungu, roho ile ile ambayo iliyaandika hayo maandiko. Hii ndiyo ramani aliyotupa Mungu, ambayo inayo maelezo ya kina kuhusu maisha yetu. Iliandikwa na watu wakijawa na roho ya Mungu- 2 Petro.1:20. Kwa hivyo, ikiwa umepokea roho yiyo hiyo, thibitisho ni maandiko yayo hayo yalioandikwa na hiyo roho. Hivyo basi, tukiishi kwa hayo, tunao uhakika wa kukaa mikononi mwa muumba wetu, na kumruhusu aendelee kutuumba mpaka atufanye viumbe wa roho kama alivyo. Kwa ujumla, huu ndio ukweli ambao umewekwa wazi kwa yeyote yule aupendao. Ni kupokea yule roho aliyeiandika biblia, ambaye utuwezesha kupata ufahamu huo huo unaoelezwa na maandiko, na hivyo kutupa upendo wa kuyaishi hayo maandiko; na hii uonekana kwa tabia zetu maana anayeyafuata uanza kuumbika tabia za kiroho, hivyo kuthibitika, maana bwana wetu anasema, “… mtawajua kwa matendo yao-Mat.7:15-16”. Na kwa vile sasa tumeyajua hayo, hebu sasa tuelewe tafadhali. Wakati Mungu alituumba katika hii miili, alituambia, “…wewe ni mavumbi… na huu mwili ni wa kufa; siku zako ni chache( isipokuwa ukubali niendelee kukuumba ili uwe tofauti), umejaa shida,; wewe ni kama nyasi tu, na maisha yako ni kama ua la kondeni; usipokubali hivi ili uone sababu ya kuanza kutafuta kuumbika kiroho; ukianza kufuata huu mwili,, hakika utakufa( somo letu, “kusudi la mwili”, litakuhadhithia Zaidi)-Mwa.3:19; Ayubu.14:1-3; Mwa.2:17”. Hivi ndivyo Mungu anavyotufundisha kuhusu huu mwili na vile aliuumba, na ndivyo wale wenye roho yake wanaelewa na kukubali. Huku kukubali hayo maelezo katika maandiko pia ndio thibitisho kwamba roho aliye ndani ya mwenye kukubali hivyo ni ya Mungu. Lakini kama vile tuliona, mwanadamu alipokea roho ya upinzani, ambayo ufahamu wake ni kinyume na ule wa biblia. Hii ni kwa sababu, maelezo ya huo ufahamu ni, “ Hakika hautakufa, wewe ni kama Mungu, yaani kiumbe wa kiroho; huu mwili ni nyumba yako ya mtu wa kiroho aliye ndani. Wakati( kile biblia inaita kufa) unasemekana umekufa, huwa ujafa; Mungu huwa amekuita maana amekupenda Zaidi kiasi kwamba, anataka ukae karibu naye huko mbinguni-Mwa.3:5”; Isa.14:13-14. Hebu tuambiane ukweli tafadhalini. Tumeona wazi wazi vile Mungu anasema kutuhusu na kuhusu haya maisha ya huu mwili tulionao kwa sasa. Je, tutaweza kusimama baada ya kuujua huu ukweli, na kuanza kuupinga huku tukisema eti huu upinzani ni lugha ya ndani ya kiroho ya kueleza yayo hayo ambayo Mungu anasema kwa maandiko? Nani haoni kuwa haya ni mafundisho yenye upinzani wa wazi kabisa? Je, kunao upofu ulio mkubwa kushinda huu? Kila jitihada jingine la kuyapindua maandiko uanza kwa kukubali huu uongo wa Edeni. Maana mtu akiisha kuukubali, ni lazima sasa pia ajaribu kugeuza maandiko yajaribu kusema vile amepewa kufahamu na hiyo roho wa uongo, na hii inafanya biblia kuonekana kama kitabu kinachojipinga; eee, ndio sababu sasa, biblia inaonekana kama kitabu ambacho akiwezi kueleweka na kumbe sivyo. Hii ni kwasababu, mtu anaisoma vizuri sana kwa lugha inayoeleweka; na, badala ya kufuata vile imemwambia, anatoa macho yake hapo, na kutazama wale wanaojionyesha kuikubali na kumbe ni hawa waongo maana ndio wengi Zaidi. Basi kwa vile wanadai eti wanachofanya ni ufunuo wa maandiko wa ndani Zaidi kiasi ya kufanya lugha iwache kumaanisha vile inasema, wewe pia, kwa kuona walivyo wengi na wanakubaliana na huo uongo, wewe pia unabebwa nao. Badala ya kuamini maandiko, unaanza kujishawishi ukishangaa, “ Kwa kweli, watu hawa wote wanaibeba biblia wanaweza kuwa hawajaielewa?” Hayo yote, unayawaza ukisahau kwamba, “ hawa ni manabii wa uongo, maajenti wa Shetani, wanaojionyesha kumtumikia yesu. Na sio ajabu, maana Shetani mwenyewe(kwa sababu ni muongo) ujionyesha kuwa malaika wa nuru- 2 Wakor.11:13-14”, na kwa sababu umesahau ile onyo la Yesu, unakosa kuuelewa ujanja wao, na unadanganyika kuanza kujiona ni kama hujaielewa biblia, maana inatofautiana na yale wanafundisha na kutenda. Lakini sasa, unatarajia iweje? Ikiwa yote wanayofundisha na kufanya ni yale walisoma kwa Adamu, ambaye alijifunza kwa Shetani, si hiyo inamaanisha kwamba, yule roho aliye ndani yao ni yule ambaye hawezi kukubali yale roho wa biblia anasema? Sasa, kama mtu amekubali uongo na kuuita ukweli, atawezaji kuugundua, na huo ndio ule ufahamu ulio kwa akili yake? Yafikirie hayo kama unaweza tafadhali. Pia ukumbuke vile Bwana wetu alitaadharisha kuhusu huu wingi wa waliodanganyika, kwamba, “ hawa waongo watadanganya wengi( wengi ni wale waendao njia yao; wachache sana ndio uienda njia ya kweli- Luka.13:24; Mat.7:13-13)-Mat.24:5”; Anazidi kuonyesha kuwa, “..Shetani ameudanganya ulimwengu wote-Ufu.12:9”. Kwa watu kuukubali huu uongo wa Edeni, Shetani amefaulu kuyafanya haya maisha ya kimwili yakose maana kabisa, na hii imewaacha watu kuishi bila lengo lolote. Kwa nini? Kwa maana, mtu akiisha kubali kwamba tayari yeye ni kama Mungu, basi ina maana kwamba yeye ni mkamilivu, na mwenye ufahamu kamili. Ni kitu gani kingine atakuwa amebakisha isipokuwa sasa kutumia huo ufahamu na kujifurahisha maishani? Kwa vile furaha kamili upatikana tu, wakati mtu anaishi kulingana na ile ramani aliyochorwa(aliumbwa) kwayo, na sasa, huyu mtu hapa ametolewa kwenye hiyo ramani, basi kile wanaita furaha ni nini? Huku wakikosa kufahamu kusudi la Mungu la kutuweka katika huu mwili( soma ujumbe wetu uitwao, “kusudi la mwili”; unapatikana kwenye Website yetu- www.endtimecog.org) ambalo ni la kuumbika akili ya Mungu ili itupe ufahamu wa kuishi kama yeye na kuumbika hiyo tabia yake ya utakatifu( soma ujumbe wetu usemao, “tafuteni heshima”), watu wamegeukia kile wanaita furaha ambacho ni, tabia za kujiharibu, tabia ambazo tunaziona kila mahali duniani, watu, “ wakilewa, kufanya uisherati, kupigania kuwa viongozi wakitafuta heshima, kutafuta kuwa na mali nyingi( maana mtu anafikiria ndiyo itampa maisha marefu), na ni utafutaji ambao unahuzisha, wizi, ukora, udanganyifu, na mengine mengi kama hayo”. Sasa, kwa vile hizi tabia zote ni uongo wa Shetani akijibidiisha kumuua mtu, badala ya kuleta furaha, zimefanya maisha kuwa magumu Zaidi, na mwishowe, kila mtu ufa kabla hajaifikia ile raha ameishi kuitafuta. Angalia kutoka kila upande na utakubaliana nami kwamba, kile watu wanaita kiroho(kuongozwa na roho), ni jitahada la Shetani akifanya kazi kwa hiyo roho yake iliyo ndani ya akili zao, la kubadilisha biblia ili iweze kusema huo uongo wake, “wakiyageuza maandiko vile wafanyavyo na kujiletee uharibifu”. Kwa nini? “ Kwa maana wameukataa ukweli( kwa kukubali roho ile ya upinzani), na kuanza kufuata hadhithi za uongo (maisha ambayo hayana lengo(mwelekeo)-2 Tim.4:3-4”. Kukubali ule ukweli ambao unaelezwa kwa maandiko, ambayo ndiyo ile ramani tulioumbwa kwayo(ndio maelezo ya maisha ya kweli), kunamfanya mtu kuwa na goli la kufuatilia(lengo la maisha). Ni goli gani? Kufanywa kuwa miungu( shetani amewadanganya eti tayari mkekuwa) ili tuweze kufanyika kuwa watoto wa hiyo jamii ya kiroho, na kuitawala dunia milele na milele. Hiki ndicho kiroho cha biblia. Tukiwa na huu ufahamu, maisha yanakuwa na maana na tunakuwa na kitu cha kufuatilia, ambacho ni kuumbika akili na tabia za Mungu, kama vile inavyoelezwa kwa lugha iliyo rahisi na ya kueleweka katika biblia. Kama hukubaliani na hili lengo anayofundisha Mungu, basi, biblia itakuwa kitu kisichoeleweka kwako na gumu yenye kufuruga akili. Sasa ndugu yangu, ni uchague kati ya haya maisha mawili. Aitha uchague, kufuata ile akili yako kama unavyodhania( ambayo utokana ni uongo wa Edeni), au kile biblia inasema(ambacho ni ufunuo wa Mungu kwako kuhusu vile alikuumba uishi). Hauitaji kubadilisha maandiko. Unahitaji kuchagua aitha kuyafuata yalivyo, au kuyakataa. Kama umechagua maandiko ya biblia(Mungu) fuata vile yasemavyo; kama umechagua uongo wa Eden(Shetani) basi, usiharibu wakati ukifungua wala kuishika biblia maana haikuzaidii, haina hayo mafundisho. Fanya tu jambo la heshima; fuata madhanio yako- “.. Roho yule atendaye kazi katika wana wa kuasi”; …roho ya sheria ya dhambi-Waef.2:2; Warum.8:2”. Wacha kufanya kile yesu Bwana aliwaambia wale waaminio akisema hakiwezekani, “kutumikia mabwana wawili-Mat.16:23”, huku ukijaribu kuunganisha roho ya Shetani na ile ya Mungu (maandiko). Jueni na kuelewe kuwa, kiroho cha biblia sio kuhusu ustadi wa lugha inayotumika, mbali ni kuhusu yale maisha hiyo lugha inaelezea. Maelezo yote (iwe ni ya Mungu au ya Shetani) utumia lugha. Cha muhimu ni kile hiyo lugha inaelezea sio ule undani lugha yenyewe imewekwa (kiwe ni madhanio yako- akili ya Shetani, au maandiko- akili ya Mungu). Lakini maajenti wa Shetani(kwa vile kazi yake ni kudanganya) wanajaribu kugeuza maandiko yasema vile wanadhania ili wajihesabie haki katika uongo, na kwa njia hiyo, wametumia vibaya maandiko, na Jina la Yesu na ya Mungu kudanganya wengi. Basi kwa hayo maelezo yaliyo wazi, “Simameni katika njia kuu, mkaulizie yale mapito ya zamani yaliyo mema(neno la Mungu-Warum.7:14) ile njia nzuri; mkaipitie hiyo, ili mzipatie nafsi zenu pumziko-Yerem.6:16”. Yeye aliye na masikio, na asikie vile roho inavyoliambia kanisa. Nehema ya Mungu wetu, ifanyayo kazi kwa wingi ndani ya Kristo wetu ikae kwa wingi ndani ya wote wenye kuchagua kiroho cha biblia. Haya yanawajieni kutoka kwa muumba wenu, akiongea ndani ya Kristo Yesu, kupitia kwa Radio yake,
ENDTIME CURCH OF GOD; WEBSITE> www.endtimecog.org; EMAIL >endcog@gmail.com;
TAHASISI LA KISWAHILI >BARUAPEPE >ukweliwabiblia@yahoo.com; Pata maelezo Zaidi kuhusu afisi zetu za mawasiliano kutoka kwa Website