Ni wazo gani uja kwa akili zetu tonaposikia hili neno la kukesha ama kuwa waangalifu? Inaweza kuleta wazo la kuangalia kitu, kumakinika, au, kujihadhari na kitu Fulani. Mungu katika neno lake na kwenye vifungu vingi anatuihimiza kuwa waangalifu, au kujihadhari katika maisha yetu. Ni kitu gani hasa ambacho Mungu anataka tukeshe kwacho? Wakati tunatazama au kuwa makini kwa kitu Fulani, huwa ni kwa ajili ya kuelewa. Lakini wakati tunakuwa waangalifu au, katika hali ya tahadhari, huwa ina maana ya usalama. Kwa vile kwa yote mawili, neno ni kukesha, basi, ni vizuri tuwe na ufahamu kamili wa kile muumba wetu anataka tuelewe ili tuweze kuhusiana nacho kwa uangalifu. Na kama kawaida yetu, kila wakati tunataka kuelewa jambo kwa ukweli, ni lazima tufuatilie kutoka chanzo chake.
Basi, kwa vile Mungu ndiye muumba vyote-Isa.40:28, ni wasi kuwa alimuumba mwanadamu akiwa na lengo Fulani. Ni lazima basi iwe, kile anachotuambia tuwe waangalifu nacho kinahusiana na hili lengo. Zote tunakubaliana kwamba, kilicho cha muhimu sana katika akili ya Mungu sasa hivi ni kuurudisha ufalme wake hapa duniani, na hilo atalifanya kwa kumtumia mwanadamu, maana wakati alimuumba alisema, na tumfanye mwanadamu aliye kama sisi( kwa mfano na sura yetu) akaitawale dunia-Mwanzo.1:26. Lakini, ili tuweze kutumika kuitawala, ni lazima kwanza tuwe viumbe wa kiroho kama Mungu mwenyewe( ujumbe wetu uitwao, “ Kusudi la mwili”, unamaelezo).
Hii inamaanisha kwamba, lengo la maisha ya huu mwili ni kufanyika viumbe wa kiroho. Kwa hivyo, kuishi kwetu na bidii zake zote zinafaa kutuelekeza kwenye kufanyika kuwa roho. Basi je, kama anachotuambia Mungu tuwe waangalifu kwacho kinao kusudi la kufanyika viumbe wa kiroho, je,Sasa hivi tunaishi kwa hiyo nia ya kuifikia hiyo goli? Hebu kila mtu ajichunguze moyoni mwake kabla ya kujibu hili swali. Ni kitu gani kimejaa moyoni mwako, ambacho ndicho unashughulikia kila wakati, na ndicho unakuwa mwangalifu kukilinda kisikuponyoke?
KIZAZI KIPOFU
Yeyote ambaye haoni kwamba kuna kitu Mungu anachoendeleza maishani mwake wakati huu ni kipofu. Kwa nini nasema hayo? Maana ikiwa tunakubali kuwa Mungu alituumba tuwe viumbe wa kiroho ili tuutawale ufalme wake, na sasa hivi tunaona wasi kuwa sisi ni miili ya nyama na damu, ambayo haiwezi kuungia ufalme wake wa kiroho- 1 Wakor.15:50, basi ni wasi kwamba,bado Mungu anaendelea kutuumba, maana atakapomaliza, tutakuwa watakatifu, na roho, kama alivyo yeye-Walawi.19:2; 1Yohana.3:2.
Ikiwa basi bado tuko kiwandani, mikononi mwa Mungu akiendelea kutuumba-Yerem.18:6, ina maana kwamba tunachofanya sasa hivi kama namna ya kuishi, na ambacho ndicho tunapaswa kuwa waangalifu nacho kinapaswa kuwa kile Mungu anachofanya kama njia ya kuendeleza uumbwaji wetu. Ni kitu gani hicho basi? Sasa hivi, kila mtu ulimwenguni ako mbioni, akitafuta mali, umaarufu, na starehe. Kile tunachokuwa waangalifu nacho sasa hivi, ni kuhakikisha kwamba hatujapoteza nafasi ya vitu au watu wanaotusaidia kuvipata hivi. Pia, tuko waangalifu dhidi ya kitu au yeyote anayepinga au kuzuia hizi nafasi za kupifikia. Hapa ndugu zangu ndipo upofu unaokujia.
Maana ikiwa jitahada zetu, na uangalifu wote ni kuhakikisha tumeumbika kuwa roho, je, mali, umaarufu, na starehe vitatufanya kuwa viumbe wa kiroho? Eee, nauliza hivi, hivi ndivyo ambavyo Mungu anatuambia tuwe waangalifu kwavyo? Hasha ata kidogo. Kwasababu, kinyume na hiyo, Mungu anasema kuwa wenye kujiwekea hiyo goli ya hivi vitatu ni, wajinga-Luka.12:20-21; zab.49:13,6-7; maana wanaona wote walioifikia hiyo lengo la mali,umaarufu, na starehe, hufa na kuwaachia wengine hizo mali; pumzi zao utoka, nao uenda kaburini na kuwa mafumbi-Zab.49:10;146:3-4. Na baada ya kuona wenzao wakifa baada yakuvipata hivyo, na kuwaachia wengine, wao wanaendelea kuving’ang’ania.
Kweli ndungu zangu, kama hawa sio vipofu, ni nini?Ninachosema hapa ni kwamba, ulimwengu wa leo hauwi waangalifu kulingana na agizo la Mungu. Kuthibitisha hayo, waangalie wote matajiri wa zamani, na wakuu wenye umaarufu Zaidi, aina ya Hitla, Musolini, Kennedy, Taja wafalme na matajiri wote waliokuwa vizazi vya nyuma. Sasa hivi wote wako wapi? Makaburini. Hii inaonyesha kwamba, uangalifu wa namna hii hautokani na Mungu, maana ungelikuwa hilo agizo lake, hawa wote waliofaulu wangelikuwa viumbe wa kiroho saa hii. Hii ndio sababu tunasema kuwa, hiki kizazi ni kipofu.
TUNACHOPASWA KUANGALIA
Ikiwa kunaye mtu ambaye anataka tuishi na kufaulu katika maisha, ni Mungu aliyetuumba, maana, ana haja na kazi ya mikono yake, ili kutimiza kusudi lake-Ayubu.14:15. Pia, ikiwa kunaye mtu ajuaye tunachopaswa kuangalia, ni Mungu. Basi je, anasema kuwa hicho cha kuangalia na kulinda, ambacho ndicho cha kutafuta kwa bidii zetu zote, ni nini? Fahamuni na kuelewa kwamba, hakiwezi kuwa ni kitu kilicho kando na mpango wake wa kumkamilisha nwanadamu. Basi anasema kuwa ni nini? Sikiliza kwa makini tafadhali. Linda moyo wako kuliko vyote uvilindavyo, maana ndiko zitokako chemichemi za uzima-Mith.4:23.
Ndugu zangu, ikiwa tutatii agizo la Mungu la kukesha, au kuwa waangalifu, basi hapa ndipo pa kuanzia. Kwa nini tuanzie mioyoni? Kumbukeni kwamba, goli la Mungu la kutuumba, ndilo linapaswa kuwa goli letu la kuishi sasa hivi. Tunajua kwamba, hii miili tulionayo sasa, ni hatua ya kwanza ya uumbwaji wetu( soma undani wake katika ujumbe, “ mchakato wa uumbwaji wa mwanadamu”), maana ni, huu wa udongo kwanza, halafu baadaye, uje wa kiroho- 1 Wakor.15:46,9. Basi je, ni kitu gani tunapaswa kuwa tukifanya sasa kama namna ya kuishi, ambacho kitatufikisha kwenye goli letu la kuwa viumbe wa kiroho ( ujumbe wetu uitwao, “kusudi la huu mwili”, unao maelezo Zaidi)?Moyo ndio kiti cha akili, na ndio hifadhi ya ufahamu na maarifa, ambavyo utumika kuishi vile mtu uishi.
Mungu Hakuiumba mioyo yetu ikiwa na huo ufahamu wala maarifa ya yale maisha tunapaswa kuishi katika hii miili. Kama hatua ya pili ya uumbwaji wetu, na ndio chanzo cha uumbwaji wa kiroho, Mungu anakusudia mwanadamu apate roho nyingine, iingie na kukaa katika moyo wake ili kumpa ufahamu na maarifa ya kuishi. Kwa hivyo, kupata ufahamu na maarifa ndio chanzo cha uumbwaji wa kiroho, ikiwa ni hatua ya kwanza ya kufanyika kiumbe wa kiroho. Shetani naye aliye mtawala wa sasa wa hii dunia anapinga vikali huu uumbwaji wetu ( soma ujumbe wetu uitwao “Miti miwili”). Kwa hivyo, anataka kutega mioyo yetu nyara, kwa kuweka roho yake ndani yetu, ili atupe ufahamu na maarifa ya uongo kusudi, tuutumie kama namna ya kuishi ili tufe. Hii ndio sababu mioyo yetu ndiyo kitu cha kulinda kwa nguvu zetu zote, maana tusipokuwa waangalifu, tutadanganyika kupokea roho ya shetani, ambayo kile inatupa kama ufahamu na maarifa ni cha kutuharibu.
TUUENDEE UZIMA
Je, wewe ni mmoja wa wale wameitikia wito wa Mungu wa kukesha, au kuwa waangalifu? Jichunguze tafadhali kabla ya kujijibu. Katika hili goli la kuwa viumbe wa kiroho, tunachojishughulisha nacho katika haya maisha ni kuwa watakatifu kama Mungu alivyo-1 Petro.1:15-16. Utakatifu ni maisha ya Mungu, na ndio namna yake ya utendaji. Hayo maisha pia ndiyo anatueleza katika neno lake, maana, neno lake ni kweli-Yohana.17:17; Zab.119:160; ni takatifu na la kiroho-Warumi.7:12,14; ni maisha ya milele-Yohana.6:63; 1 petro.1:25.Basi, ili tuweze kuanza kuishi kama Mungu, ni lazima kila mmoja afanye uamuzi wa kuwa kama Mungu kwa hiari, yaani, kuamua mwenyewe bila shurutisho lolote. Ni hapo tu tunapofanya huu uamusi, Mungu naye uingia mioyoni mwetu(kwa njia ya kuweka roho yake mioyoni), na kuanzisha hii kazi ya kutuumbia ufahamu-Yohana.14:23, kama alivyoahidi akisema, nitaziandika sheria zangu mioyoni mwao, na katika akili zao, nitazitia-Yerem.31:33.
Kwa vile ufahamu ndio utupao namna ya kutenda, na hapa ufahamu tulionao ni hili neno la Mungu, basi uangalifu wa mioyo yetu ni kuhakikisha kwamba, kile kilichojaa humo, na ambacho ndicho tunatumia kuishi, ni neno la maandiko, maana, ndio uhai wa mwanadamu-Mith.4:22; 3:16, 15,17. Elewa basi kwamba, kama wewe goli lako ni lile la Mungu la kukufanya kiumbe wa roho, hautakuwa na ufahamu mwingine wowote ule isipokuwa neno lake-kumbukumbu.4:6, na hili ndilo litakuthibitishia kuwa roho iliyo moyoni mwako ni ile ya Mungu- 1 Yohana.3:24; 2:3.Je, wewe huko na roho ya Mungu? Je, maandiko ndio ufahamu unaotengeza tabia na matendo yako yote? Hebu ujichunguze tena kabla hujajibu. Mtu ambaye ufahamu wake unatokana na roho ya Mungu hatetei huu mwili wala faida, au tamaa zake, maana anaufahamu kuwa, bure-Wag.6:3, kuwa adui ya maisha-Warum.8:6-7, na, usio na thamani yeyote- Mwa.18:27; Yakub.4:14; Isa.40:6-7. Kwa hivyo, uangalifu wake huko katika kukamilishwa ili aweze kufanyika kuwa kiumbe cha dhamani, yaani, kuvaa utukufu, heshima, kutokuharibika, na uzima wa milele-Warum.2:7.
Kwa sababu hii, mali, umaarufu, na starehe hazina tena, thamani ya kutamanika kwake kabisa. Zimekuwa bure kabisa, sawa sawa na mavi-Wafil.3:8. Kwa nini? Maana havimsaidii kuifikia goli lake la kuwa kama Mungu. Ni mtu ambaye amegundua kuwa, faida za mali,umaarufu mbele za wanadamu wenzake, na starehe za huu mwili, ni zamuda mfupi-Ayubu.14:2-3; Waeb.11:25, na baada yake ni kufa. Amegundua pia kwamba, sio yeye anayejiumba; kwa hivyo, namna ya pekee ya kuulinda na kuutetea huu mwili ni kuutegemeza kulingana na maagizo ya Mungu, kitu ambacho mwili wenyewe haufurahii, maana, ni uadui kwake-warum.8:7. Hapa ndipo uamuzi unahitajika, maana, huku roho ya Mungu ikituelekeza kufurahia sheria ya Mungu katika mioyo yetu-Warum.7:23, Shetani naye akitumia mapenzi ya mwili analeta ushawishi wake, mawazo ambayo hayataki kutii hizo sheria ambazo ni maandiko ya Mungu-Warumi.7:23 sehemu ya mwisho.
Ndugu zanguni, hapa ndipo utakapokuwa na uhakika wa yule roho anayeujaa moyo wako, maana kama ni wa Mungu, utachukizwa na huo ushawishi wa mawazo ya shetani na kumpinga-1 Petro.5:8. Tunao mashahidi waliotutangulia katika haya maisha, eee, waliochukua huu uamuzi wa kuuendea uzima. Tunaelewa kwamba tendo la ngono ni la kufurahisha sana, lakini linapaswa tu kufurahiwa ndani ya ndoa. Basi, Yusufu, hali akiwa katika harakati za kuuendea uzima, Shetani alimjia kupitia kwa mke wa pontipali aliye kuwa mrembo hajabu; akamwambia, lala nami-Mwa.39:7. Kwa vile yule roho aliyeujaa moyo wa Yusufu ni yule wa Mungu ambaye anasema, usizini-Kutoka.20:14, eee ambaye anachukia maisha ya Shetani, basi alimpinga mara moja na kumuuliza, nifanyeje ubaya huu mkubwa nimosee Mungu wangu-Mwa.39:9?Akakumbuka kile Bwana wetu Kristo anatuambia anaposema, ukiuokoa huu mwili kwa kuutoshelezea mapenzi yake nje ya amri za Mungu, utaupoteza-Mat.16:25.
Hii ni kwasababu, mwili utamani maisha yanayopinga yale ya Mungu- Wagal.5:17 ambayo ndio uhai peke yake. Kwa hivyo mtu yeyote akiushikilia, anatafuta kifo, ee, kujiharibu-Warumi.8:12-13; Waef.4:22. Kwa vile Mungu ndiye aliyeuumba huu mwili, basi yeye peke yake ndiye anajua vile unapaswa kutunzwa. Basi naye anaelezea namna ya kuutunza kwa njia ya sheria zake. Hii ni kwa sababu, hizi sheria ndizo uhai- yaani kule kutenda kutakaotuelekeza na kutufikisha kwenye uzima.
Turudi mioyoni sasa. Je, yule roho aliye mioyoni mwetu anafurahia kuishi kulingana na sheria za Mungu au anatamani kuufurahisha mwili, lakini kwa sababu tumejifanya kumwamini kristo, tunaonyesha tu utiivu wa nje huku mioyo ikiugua ikitamani umwili? Mtu anayetii agizo la Mungu, ya kuwa mwangalifu, ambaye anakesha, uifurahia sheria ya Mungu, na ndiyo mawazo yake mchana na usiku-Zab.1:2. Kwa hivyo, chochote atendacho, uangalifu wake mkuu ni kuhakikisha ametenda kulingana na vile Mungu anasema, maana analengo la kukamilishwa na kuwa kama Mungu. Hii uwezekana tu, ikiwa yule roho aliye moyoni ni yuyo huyo aliye yaandika maandiko ya biblia.
THIBITISHA IMANI YAKO
Tusisahau kile Mungu anachotufunulia hapa, yaani kukesha, eee, kuwa mwangalifu. Tumeona vile uangalifu uja kwa ufahamu. Nao ufahamu uja kutoka kwa roho inayoujaa moyo. Tukaona basi kuwa, ikiwa roho inayoijaa mioyo yetu ni ile ya Mungu, basi ufahamu tunaoutumia kuangalia, ni maandiko, maana Bwana anasema kwamba, utatunza njia zako kwa kutii ukilitenda neno lake-Zab.119:9. Je, tumethibitisha kwamba roho aliyetujaa kutupa ufahamu wa kukesha( kuishi katika kweli) ni yule wa Mungu?Tujichunguze tena, huku tukifahamu jambo hili; la kwamba, mtu hatendi kilichojaa moyoni mwake kwa kulazimika, mbali kwa kuwa, ndicho apendacho kuliko vyote. Kwa hivyo, hana masharti yoyote ya kufanya hivyo, mbali, anatenda kwa kuwa ndivyo alivyo na hawezi kubadilika. Tunasema kwamba uangalifu wetu ni ule wa Mungu ambaye habadiliki kamwe. Na hii ni kwasababu, roho aliye mioyoni mwetu ni huyo wake.
Kwa hivyo, hata kuwe nini,kuje nini, tabia zetu, matendo, nia za mioyo, na hata maongeo yetu yatakuwa ni yale ya Mungu.Sisi zote tunazielewa tabia za roho wa Mungu, ambazo ndizo tabia za Mungu mwenyewe, na ndizo anaumba ndani yetu, maana anataka kutufanya kama yeye. Je, hizi ndizo tabia zako; yaani, upendo,furaha, Amani, uvumilivu, utu wema, , fadhili, uaminifu, upole na, kiasi-Wagal.5:22-23? Kumbuka, haya ni matunda ya roho aliyeujaa moyo. Kwa hivyo, huyu mtu hana ufahamu mwingine; hivyo hana mapenzi mengine isipokuwa yale ya huyo roho, maana Bwana anasema, kutoka moyoni, mtu uongea, na kutenda.
Haiwezekani moyo uliojaa roho wa Mungu ukatoa tabia za roho wa shetani, au wa shetani ukatoa tabia za Mungu- Mat.12:34-35; 7:17-18.Ili kuwe na uwezekano wa kuumba hii tabia yake ndani yetu, Mungu alituumbia mwili wenye nia za kishetani( pata maelezo Zaidi katika ujumbe wa, “kusudi la mwili”), na pia akmwacha Shetani aendelee kuitawala hii dunia ili,akupime na kuona kama kweli umeamua kuishi kama yeye-Waamuzi.2:22; Yakubu.1:3-4. Basi wewe uliye na roho ya Mungu yenye kutenda wema mtupu bila masharti yeyote, hapo shetani anapokujia na mawazo yake yapingayo hayo ya Mungu, wewe ujibu kwa ufahamu wa Mungu ama unatumia mwili kutumikia nia zake? Usiwe wa haraka kusema ndiyo. Jiangalie kwa uwasi. Saa hii mtu akikuchapa, au akutukane, akunyanganye mali yako- ndio, akufanyie madharau ya kukuahibisha mbele ya watu, wewe utamfanyia nini? Ikiwa kweli, roho aliye moyoni mwako ni yule wa Mungu, hautakuwa na kingine cha kumfanyia isipokuwa ule wema uliojaa moyoni mwako.
Hii ndiyo sababu, wale waliotutangulia wako na huu ushuhuda: Tukitukanwa, twabariki,tukiudhiwa twastahimili, tukisingiziwa twasihi; tumefanywa kama takataka za dunia-1 Wakor.4:12-13. Kwa nini wasijiteteena kuwapiga hawa? Sababu, akili zao uyaelewa maisha kwa njia iliyo tofauti na hiyo ya watezi wao; na kwa vile lazima mtu atende kulingana na ufahamu ulio ndani yake, basi wao utenda ufahamu ulio mioyoni mwao, huku nao hawa wanaowafanyia maudhi wakitenda ufahamu wa roho aliowajaa. Hii ndio sababu tunashauriwa, kutokushindwa na ubaya, mbali tuushinde ubaya kwa wema-Warumi.12:17-20. Ni kwa nini tuishi kwa kile, kwa mtazamo wa kibinadamu, kinaonekana kama kujiachilia? Maana, tunachokifuata, tunachotaka kupata, hakipatikani kwa njia ya kujilinda kama wanavyofanya walimwengu. Hakipatikani kwa, wala kuzuiliwa na, mali, umaarufu, au starehe.
Hakilindwi na kupigana, kuchukia au kudhulumu wanaokupinga. Goli yake uwezeshwa na Mungu kwa yeyote yule ayafuataye maagizo yake. Hii ndio sababu, wale waliotutangulia kuuendea uzima, hawakuweka dhamana yao kwa huu mwili, kwa watu, au mali. Ndio sababu walikataa maisha ya kifahari- Dan.5:17; Waeb.11:25-27,35-38; Mat.22:16;2:24. Walielewa vizuri sana kuwa, kusudi la kuumbwa sio huku kuishi kwa sasa, mbali, kuishi kwa sasa ni kwa kujitayarisha kwa hiyo kusudi ambalo ni kuufikia ukamilivu, na ni hapo watakopo badilishwa kuwa roho, maana wanasikika wakisema, maana wenyeji wetu huko mbinguni, na kutoka huko, tunamtazamia mwokozi, atakaoubadilisha huu mwili wetu wa unyonge, Ufanane na ule wake wa utukufu-Wafilip.3:20-21.
Mpaka hapo tutakapoufikia huo, hatuoni kitu chochote hapa katikati, na thamana yetu yote iko uko, maana kila aliye na roho ya Mungu ndani yake, anao ufahamu wa kuwa, yuko hapa duniani kuumbika mpaka awe kama Mungu, ili aurithi na kuutawala ufalme wake-Mwa.1:26. Ufahamu na tabia za ufalme wa Mungu, na kufaulu kwake ni pembeni tufouti na ule wa ulimwengu huu. Hii ndio sababu uangalifu wetu, ni kuongozwa na neno lake kutumulikia njia zetu, na kutuwezesha kuona-Zab.119:105. Huku ndiko kukesha, na kuwa mwangalifu. Je, tunakesha? Tunakuwa waangalifu? Ni mwokozi wako Kristo yesu akikuamsha ili uendelee na safari hata uifikie goli analokusudia kukufikisha, kwa ujumbe huu, kupitia kwa mtumishi wake.