KUISHI BILA VIKWAZO

Tumewahi kushangaa ni kwa nini akili ya mwanadamu ufikiria, na kuwaza juu ya mwanadamu mwenzake au vitu( mali) kila wakati? Tumewahi kujiuliza ni kwa nini hatuna mambo yoyote ya kufikiria nje ya mwanadamu na mali? Watu wengi kati yetu ujihuzisha katika fikira na mipango ya kimaisha lakini hawakui waangalifu wa kufuatilia na kuelewa chanzo na matokeo ya fikira na matendo yao. Huku kutokuwajibika vilivyo utuwacha tukiishi maisha ya huzuni, hasira, chuki, woga na hata vita.Maisha yetu leo yamejawa na vikwazo vya kila aina. Je, kunao vile tunaweza kuishi bila hivyo? Eee, kunayo njia ya kuishi tusiwe na vikwazo vyovyote vile? Kama ipo, tutaielewaji? Ili tuweze kuifahamu, inatubidi kwanza tuelewe vikwazo ni nini na huwa vinaletwe na nini. Kikwazo ni kuchukizwa na tamshi, tendo au tukio fulani ambayo inahusu anayekwazika. Hiki uja wakati matarajio yanakuwa kinyume. Basi kama ni hivyo, tunawezaji kuwa na msimamo ambao, unatuwacha tukihusiana na hivi vya kukwaza bila kukwazika? Sisi sote tunakubaliana kwamba, chochote tutendacho huwa na lengo la kufikia goli fulani. Hii inaturudisha kwenye maswali letu la mwanzo, tuliposhangaa ni kwanini mwanadamu ujifikiria, kufikiria wanadamu wenzake na mali. Kwa kila jambo tutendalo kila wakati, lengo huwa ni kutaka kuishi. Basi tuelewe kwamba, kuishi ni kutenda mambo, na yale mambo mtu uyatenda yanaonyesha yale maisha anayotaka kuishi, maana, mnawajua kwa matendo yao-Mat.7:16.

                                                                 AINA MBILI YA MAISHA

Basi, ni hapo wakati, kile mtu anachotaka kufikia kinapopata upinzani ambao unasababisha kisifanyike, ndipo mtu ukwazika. Kunayo aina mbili ya maisha, na kila moja inayo njia yake tofauti na ile nyingine. Aina moja ni ya kimwili, na ya pili ni ya kiroho( soma ujumbe wetu uitwao, “miti miwili”, kwa maelezo Zaidi. Utaupata kwenye tovuti( website) yetu ). Sisi zote tuliumbwa tukiwa kwenye kiwango hiki cha kimwili-1 Wakor.15:46, lakini kusudi la Mungu haikuwa kudumisha haya maisha yake(ya mwili). Tunao ujumbe uitwao, “ Kusudi la mwili”, wenye maelezo Zaidi. Mungu anataka mwanadamu aliye kama yeye-Mwa.1:26, na hili aliwezekani pasipo uhuru wa kuchagua kuwa hivyo, kwa hiari ya mtu binafsi. Basi wandugu, tuelewe ya kwamba, haya maisha ya kimwili  ni wakati Mungu ametuwekea wa kufanya uamusi, na kujifunza kuishi kulingana na yale maisha anayoamua mtu. Kwa wale wanaoamua kuishi maisha ya Mungu, yeye uendelea kuwaumba kwa kuwapa roho yake ambayo ushuhudia( utupa ufahamu) pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu wana wa Mungu-Warumi.8:16. Huu ufahamu nao utuwezesha kuwa na kitu cha kutenda, maana, tunaumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli-Waef.4:24. Kwa wanaochagua kuasi maelezo ya Mungu kuhusu vile wanavyopaswa kuishi, na ni kwa ushauri wa muasi mkuu( Shetani), wao ubakia kwenye hiki kiwango cha kimwili( ujumbe wetu uitwao, “ mfumo unaobomoka”, unayo maelezo kamili), wakiyaelewa mambo ya kimwili peke yake, maana, wale waufuatao mwili uyafikiri mambo ya mwil-War.8:5. Wandugu wapenzi, tunakubaliana sisi zote kuwa, Adamu alidanganywa wakati alipopewa na Mungu nafasi ya kuchagua kati ya haya maisha mawili, maana baada yo kuagizwa kwamba, matunda ya miti yote( ukiwemo mti wa uzima) anaweza kula( hiyo ni aina ya maisha ya Mungu), lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya(aina ya maisha ya shetani-Ona Warumi.8:2), asikule-Mwa.2:16-17, Adamu alimgaidi Mungu na akachagua maisha(kula tunda) aliyokatazwa-Mwa.3:4-5, na papo hapo, akatengwa na Mungu hali akiwa kwenye hiyo akili ya kimwili-Mwa.3:24. Ukisoma, utaona kwamba roho ile iliyoingia akilini mwake kumpa ufahamu wa namna ya kutenda( kuishi), ni ya Shetani, roho yule atendaye kazi katika wana wa kuasi-Waef.2:2.

VIKWAZO

                           Basi, tuelewe ya kwamba, ulimwengu wa leo umejengwa juu ya haya maisha ya kimwili, ambayo akili yake uelewa, utafuta na, utenda mambo ya kimwili peke yake. Ukitaka kuyathibitisha hayo, wasikilize viongozi wa mataifa yote duniani leo, matajiri, wasomi, wazee kwa watoto, maskini , eee, kila mtu uyaongelelea na kung’ang’ania mambo ya kimwili, maana, mambo ya kiroho ni upusi kwao-1 Wakor.2:14. Hii ndiyo sababu watu wote, wakristo kwa wapagani, matajiri kwa maskini, viongozi kwa wanaoongozwa, wote ufikiria, kunena, kupanga na kutenda wakiwa na wazo la, mtu binafsi, watu wanaomzunguka na vitu, kwa akili zao. Eeee, nje ya hivyo vitu, akili ya kimwili haielewi chochote. Basi, kulingana na hayo maisha, Shetani alimdanganya mwanadamu kwamba yeye ni kama Mungu-Mwa.3:5. Hii inamaanisha kwamba mwanadamu ni mkamilifu, na hivyo, kila afikiriacho, kusema na kutenda ni cha haki na kweli( kumbuka, huu msimamo ameufikia mwanadamu baada ya kukubali uongo). Je, huu  msimamo umemletea mwanadamu maisha gani? Akijaribu kisichowezekana, yaani kutaka kufanya uongo uwe ukweli, eee, kuvuna maembe kutoka kwa mchungwa-Mat.7:16, amejiletea vikwazo chungu nzima. Hebu tuelewe.Mungu ni roho, ni wa milele, ni mkamilivu, mwenye hekima na nguvu kuliko wote, mmiliki wa vyote( mwenye mali yote); taja kila aina ya ukuu, na utakuta kuwa hakuna anayeweza kumfikia Mungu. Hata hivyo, Mungu hajigambi kwa sababu ya ukuu wake, wala haishi hayo maisha akitaka kuonekana, kusifiwa, kusujudiwa, kuheshimiwa au kuogopewa na yeyote. Yeye uishi hivyo maana kwa hakika, ndivyo alivyo, na pia, ndivyo apendavyo kuishi.

UNAFIKI

Basi, mwanadamu akidanganyika na kuanza bidii ya kuwa kama Mungu, huku bidii zake zikikosa kumfikisha kwenye nia yake, alianza kuendeleza huo uongo, na amekuwa mpaka sasa akifanya hivyo kwa kujifunika ngozi ya mwana kondoo ( kufeki maisha ya Mungu kwa muonekano wa macho tu)-Mat.7:15. Pia, katika huo uongo, anaamini kwamba, kwa vile mtu aliumbwa mkamilifu, basi hapaswi kutenda makosa. Kwa hivyo, wakati wowote mtu anapomkosea mwezake huwa anafanya maksudi, eee huwa anafanya ujeuri. Hivi ndivyo vikwazo vilianzia, ama huanza. Kwa vile ni kama Mungu, basi, chochote mtu afikiriacho na kusema huku akitenda, kinapaswa kukubalika, kuungwa mkono, na hivyo, kufuatwa na wote. Hii mipango na mambo yote kwa ujumla, yanafanyika kwa kutumia akili ambayo huona, kusikia na, kuelewa mambo ya kimwili peke yake. Kulingana na hii akili, kukamilika ni kuwa na mali, kupata uongozi, kusoma sana, kuwa na afya nzuri, na nguvu ya kutisha, kiasi kwamba hakuna yeyote awezaye kukutisha( kama Mungu), na mengine kama hayo. Mtu akisha vifikia hivyo viwango, basi yeye ufikiria moyoni mwake, “ Eee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba ya miaka mingi; pumzika basi ule, unywe, na kufurahi-Luka. 12:19”. Kwa vile watu wote wako katika hii akili ya kimwili, wanaomwona huyu tajiri pia, ufikiria yeye amepanda kiwango cha ukamilifu, na kumsifia kwa hayo anaojitendea-Zab.49:18. Katika hiki kizazi kilichoanzishwa na kufundishwa na Adamu, watu huuona ukamilifu kwa njia ya kimwili, ambao ni kupitia kwa watu na vitu. Eee, ujisifu wenyewe, huku wakijilinganisha wao kwa wao-2 Wakor.10:12. Kwa hivyo, kila mtu ujibidiisha machoni pa wenzake( sio machoni pa Mungu, maana mambo ya kiroho hawayaelewi), wakipokeana, na kupeana utukufu wao kwa wao-Yohana. 5:44. Tofauti na Mungu ambaye hayaishi haya maisha kwa kutaka chochote kutoka kwa wanaomwona, wanadamu wanaishi kujipendekeza kwa wengine; kumaanisha wao sio kama Mungu. Basi, kila wakati mtu anapojipima na mwenzake na kuona hajamfikia, yeye ukwazika. Kila wakati tunapoona wengine hawajatutambua na kupongeza juhudi zetu, tunakwazika pia. Hii inazaa wivu, chuki, fitina, masengenyo( bidii ya kumpaka mtu matope ili kumzusha akilini mwa wanaomsifu), vita na hata kufikia mauwaji. Na haya yote utendeka watu waking’ang’ania kushikilia uongo, ambao unaonyesha kusudi la maisha kuwa ni kudumisha mwili na mali, ambao Mungu amesema wasiwasi kuwa, haya tunayoyaona kuwa mafanikio na ukamilifu, yataishia kaburini-Warumi.8:13. Kristo akiyathibitisha hayo, anakiambia hiki kizazi, “mpumbavu wewe-Luka.12:20. Unaitanisha mali, sifa za watu, na uongozi( vyeo vya kimwili) kwa jina lako, usitambue kwamba kaburi ndiyo miliki yako peke yake-Zab.49:11; kwamba utakufa na hivyo vyote utawaachia wengine-Zab.49:10?” Basi je, kama ni hivyo, kuwapi kukamilika? Na kama hakuna kukamilishwa na hivi vitu, kwa nini tunakwazika tunapovikosa au, kutotambuliwa na wenzetu? Kwa sababu tuliamini uongo kuhusu kusudi la Mungu kutuumba na kuendelea kutuweka hai katika huu mwili, na hiki ndicho chanzo cha vikwazo vyote. Angalia kila mtu kila mahali; wakubwa kwa wandogo, maskini kwa tajiri, viongozi kwa wanaoongozwa, wasomi kwa ngumbaru; utaona bidii ya kila mmoja ikiwa ni kutaka kuonekana kuwa kitu cha heshima, kutambulikana, kukubalika kuwa mkuu kuliko vile alivyo, kuogopewa, na mambo kama hayo. Tajiri anataka kuonekana kuwa tajiri Zaidi; kama ni Raisi wa taifa, anataka kama angekuwa Raisi wa ulimwengu mzima; kama ni mchungaji katika kanisa, anatamani angekuwa mkuu wa kanisa lote; eee, kila mtu hatosheki na ile hali aliyonayo. Maana yake, anataka kuthibitisha kuwa, ule uongo alioupokea kwamba yeye ni kama Mungu, sio uongo, mbali ni kweli( yaani kudanganyika zaid). Hivyo basi, hii inazaa mashindano, kujigamba, kudharau wengine, kudanganya, ambapo, vyote hivi vinaleta kile kinaitwa unafiki( yaani, kujionyesha vile ambavyo hauko kwa hakika), huku Mungu akizidi kutuonya na kutuambia kuwa tabia hii ni ya kukosa akili ( maana akili inayotumika hapa ni uongo)-2 Wakor.10:12, na ni kujidanganya wenyewe-Wag.6:3. Kristo anatushangaa akiuliza, kwa nini mnaniita mwamrishi( Bwana) wenu, huku mkiendelea kutii amri za mwingine? Mbona amri zangu mwaziweka kando, na kutii za Shetani( mila zenu)- Luka.6:46; Marko.7:8-9? Huu ndio unafiki ndugu zangu, na ndio mama wa vikwazo vyote. Je, umekubaliana na neno hili litokalo kwa Bwana muumba wako? Unataka kuishi maisha yasio na vikwazo?

JIJUE UPYA

Wewe sio kile umeishi kujifikiria, na unachong’ang’ania kuwa, sicho unachopaswa kung’ang’ania wala, unachojibidiisha kupata, sicho ambacho unapaswa kutafuta (Ujumbe wetu uitwao, “Imani Gani?”, utakuadithia zaidi). Basi, tuanzie wapi, tukitafuta nini, ambacho kitatuondolea vikwazo vyote? Kunaye Mungu mbinguni, aliyeumba vitu vyote, ajuaye vyote, naye uwafunulia siri zote wale wemwendeao- Dan.2:28; Amosi.3:7. Huyu Mungu anatuthibitishia kwa hakika kwamba, tulichokirithi kama ufahamu ni uongo; kwa hivyo, ulimwengu mzima umedanganyika, na hivyo msingi unakosimama ni uongo-Yerem.16:19; Ufu.12:9. Tumeyakubali hayo kutuhusu sisi? Kama ndiyo, jambo la kwanza kabisa ni kujikana, na kutoa huo uongo tunaouita ufahamu-Mat.16:24; Waef.4:22.  Kama tumefanya hivyo, tumebaki akili tupu isiyo na ufahamu wowote. Sasa tuanze kama vile mtoto azaliwapo uanza-Mat.18:2.  Mungu anatuambia kwamba, sisi ni kama yeye kwa kiwango fulani tu. Gani? Mungu akamfanya mwanadamu kwa mfano wake peke yake-Mwa.1:27. Hii ina maana gani? Ijapokuwa muumba wetu anataka mtu mwenye mfano na sura yake-Mwa.1:26, anamfanya kuwa hivyo hatua kwa hatua, ya kwanza ikiwa ndio huu mwili tulionao-1 Wakor.15:46( pata maelezo ya kina kutoka kwa ujumbe wetu uitwao, “mchakato wa uumbwaji wa mwanadamu”). Sasa hivi, kila mmoja wetu anahitaji kuvaa sura ya Mungu katika uhaki na utakatifu wa kweli-Waef.4:24, ili kutimiza hatua ya mwisho ya uumbaji, ambapo, tutaivaa sura yake na hivyo kuwa kama yeye kikamilifu-1 Wakor.15:49. Eleweni basi na kufahamu kwamba, sisi katika huu mwili sio kama Mungu. Tukubali kwamba maisha ya huu mwili ni ya kutafuta kuwa kama yeye, ambao ni kwa njia ya kujifunza kwake( kupata ufahamu), na kuutumia huo ufahamu katika fikira, nia za mioyo, mipango na utendaji wote; eee, sisi ni mjengo wa Mungu, nyungu iliyo mikononi mwa mfinyanzi-1 akor.3:9; Yerem.18:6. Kama ni hivyo basi, ni nani awezaye kufahamu ile njia Mungu anatumia kuiumba hii sura yake ndani yetu hata afikie kutufanya kuwa kama yeye kwa kila namna? Kusema kweli, isipokuwa atuambie yeye, hakuna awezaye kufahamu. Kama ni hivyo, ni kwa nini basi, tunapokuwa katika hali fulani, hasa hasa ile isiyo ya kufurahisha, tunalalamika, huku tukifikiria ni kama Mungu ametusahau na amekosea mahali, na hivyo, badala ya kuwa makini kufuata maagizo yake, tunageukia mawazo mengine ambayo hayatokani na maandiko yake? Anatushangaa akituuliza; “ Ni nani huyu atiaye mashauri giza kwa maneno yasio na maarifa? Kwa nini mnapindua mambo? Je kitu kilichofinyangwa kimnenee anayekifinyanga-Ayubu.38:2; Isa.29:16?” Wapenzi, kama tutaishi bila vikwazo, ni lazima tuyashike sana haya ayasemayo Bwana hapa, na kuwacha kabisa kujifikiria wala kujijali kwa namna nyingine yeyoyote ile, isipokuwa kwa njia ya maagizo ya yeye anayetufanya kuwa kama yeye, maana anatuambia kwamba, mawazo yake sio yale yetu, na wala njia zake sio zile zetu-Isa.55:7-8.

MAISHA TOFAUTI YENYE GOLI TOFAUTI.

                       Ni vizuri sasa kwamba, kufikia hapa, tumetambua na kukubali kwamba hatujijui, hatujui tuendako, na wala, hatujui njia, kwa kuwa, tumegundua kwamba, yote tuliyorithi kutoka kwa baba zetu kama ufahamu wa kuishi ni uongo-Yerem.16:19. Kilichobakia sasa ni kuanza upya (soma ujumbe wa “Mfumo unaobomoka”), huku tukiwa waangalifu kuona kwamba, hatujafikiria, kutamani, kunena, wala kutenda kwa ufahamu mwingine wowote ule isipokuwa ule tunaopata kwa Mungu (neno lake)-Mith.3:5. Huu ndio mwanzo wa kumaliza vikwazo kabisa. Kwa njia gani? Hali tukijua kuwa, hatukuumbwa Kwa ajili ya haya maisha ya kimwili, basi hatuishi tena kuushughulikia mwili, tule nini, tuvae nini, tupate mali ya kutegemea wapi—-Mat.6:27, 32. Kwa hivyo, masumbufu au mazuri ya mwili hayatuingii kwa akili-Zab.62:10, mbali, kwa kila jambo, tunahusiana nalo kwa jitihada la kuutafuta ufalme wa Mungu na haki yake-Mat.6:33; Warumi.2:7; Waef.5:16-17. Kabla Mungu hajatufungua macho, tumeishi kwa kutafuta mali, na kuulinda na kuutosheleza mwili. Woga wetu, huzuni, hasira zetu ni wakati tunapoona tisho la kutokuwa na uwezo wa kuutunza mwili. Lakini sasa tumebadilisha goli. Tunaishi kutafuta na kuushughulikia mwili tulioahidiwa ambao auharibiki, na wenye uzima wa milele ndani yake-Warumi .2:7; Wafilip.3:21. Kwa hivyo sasa, woga wetu, huzuni, na hasira, umebadilika na kuwa, ni hapo tunapoona tukikosa kutumia ule ufahamu unaotuelekeza kwenye huo mwili mpya. Kama ni hivyo, kuwapi kukwazwa na mwanadamu mwenzako? Kuwapi kukwazika kwa kukosa kutambuliwa, kuwapi kukwazwa na madharau ya watu; eee, kuwapi kukwazika kwa sababu ya kukosa kufanikiwa kupata mali? Nawauliza, hivi vyote vinachangia nini, au kukozesha nini katika kuutafuta mwili usioharibika na uzima wa milele? Tuliona vile vikwazo uja, wakati mtu anapoona kizuizi kunachomnyima kuifikia Lengo Lake. Hapa, lengo letu sasa ni kuifikia goli la mwili wa kiroho. Basi je, hivi vya kimwili vinakunyima kuufikia mwili wa kiroho na uzima kwa njia gani, hata ukwazike? Na kama havikunyimi, kukosekana kwake kutakukwaza kwa njia gani? Ninachosema ni hiki: Enendeni kwa roho, na hivyo, hamtazitimiza tamaa za mwili. Maana kila mwenendapo kwa roho, mwaupinga mwili; hali mkienenda kwa mwili, mwaipinga roho-Wag.5:16-17. Tuangalie kila upande,tuangalie kila jambo katika maisha, na tutaona kwamba, vikwazo vyote ni katika mwili, yaani, tamaa za macho, tamaa za mwili, na kiburi cha maisha-1 Yohana.2:16. Eee, watu ukwazika anapodharauliwa, anaponyimwa anachokihitaji, anaposhindwa na wenzake, akikosa kufikia vile viwango vya kimaisha ambavyo wanadamu wameviweka. Hapa, tunathibitisha kwamba, vikwazo vyote utokana na maisha ya kimwili. Lakini sasa, sisi ni watu tumeukana mwili na maisha yake na tumeanza kuishi kiroho; kumaanisha, hatutafuti tena hivyo ambavyo vilikuwa vinatufanya tukwazike tunapovikosa. Ndio, hatutafuti kusifiwa na watu; kupanda viwango vya utajiri, kuheshimiwa au kuogopewa n. k.  Tuseme nini wandugu? Hatua ya kwanza kabisa ya kuishi bila vikwazo ni kujifahamu, na kukubali vile Mungu anasema kutuhusu. Anasemaje? Kwamba tuko hapa ili tuumbwe ufahamu, na tabia zake, tufanywe upya katika nia za akili zetu, na kuvaa utu upya-Waef.4:23-24. Kuumbika akili, au tabia hakuhitaji Mali, wala viwango vya uongozi, au sifa na kuungwa mkono na wanadamu. Kwa hivyo, kuwa na hivi vitu au kuvikosa hakuchangii chochote. Hii ndio sababu Mungu anatuambia, mali ikiongezeka, msiigeukie-Zab.62:10. Akaongezea Kristo akisema, msiweke mioyo yenu kwenye mali, ziishao na kuharibika-Mat.6:19-20.

TEGEMEO MPYA YENYE MAHITAJI MAPYA

Tukisha chukua hiyo hatua ya kwanza ya kuishi bila vikwazo ambayo ni kwa kuukana ufahamu wote wa kwanza, na ambao ndio mwili umejengwa juu yake, basi tunakuja kwenye hatua ya pili ambayo ni ya kumalizia vikwazo vyote vinavyobaki, na hivyo kuufikia uhuru uletwao na kuijua kweli- Yohana.8:32. Hatuko tena kwa ajili ya kufikia viwango vya kimaisha vya ulimwengu huu. Haya maisha tunayojifunza na viwango vyake ni ya ulimwengu ujao ambao tunahubiri juu yake-Waeb.2:5, ambao kwa huo, tuliumbwa ili, baada ya kuumbika kikamilifu na kuwa kama Mungu,tutapewa falme, mamlaka, na ukuu wa falme zote chini ya mbingu(duniani)-Dan.7:27. Baada ya kuugundua uongo ambao umetudumisha katika mwili, na tumeishi ndani yake miaka hiyo yote, tumeuwacha, na sasa tumekuwa na goli mpya ya kuufikia mwili usioharibika na uzima wa milele, ambazo zitatuwezesha kurithi utawala wa falme zote katika ufalme wa Mbinguni. Tunahitaji nini ili tuifikie na kutimiza hili lengo letu mpya? Mungu anatuambia, “tafuteni uhaki na utakatifu ambao bila huo, hakuna atakayemwona Mungu-Waeb.12:14(hakuna atakayeifikia hili goli)”. Katika hili goli mpya, uoga wetu, hofu,na huzuni huja tu, wakati tunajiona tukishindwa kutimiza haki na utakatifu, kulingana na vile zinaelezewa katika maandiko.

VIFAA VYA KIROHO

Katika goli letu la awali, tulikuwa tunaondoa vikwazo, kwa kuhakikisha, tumepata mali, kuheshimiwa na watu, kuwa juu ya wengine, kuwa na uwezo wa kunywa na kula, kuvaa vizuri, eee, kutimiza viwango vyote vilivyowekwa na wanadamu vya kuonyesha kwamba mtu ameendelea, amefaulu. Sasa hivi, tumeufia mwili; hatuko tena kuishi kwa faida lolote lake, maana tumefufuliwa( kuanza upya) pamoja na kristo( kwa kukubali maisha ya maandiko), akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho-Waef.2:6. Huu ulimwengu wa roho ni gani? Kusudi la Mungu la kutuumba, na kuendelea kutuweka hai, ni kutufanya viumbe wa kiroho kama yeye, ili baada ya hapo, atupe falme zote chini ya mbingu- Mwa.1:26; Dan.7:27. Huu mwili na maisha yake ndio uwanja, na wakati wa mazoezi, maana, ijapokuwa tuko katika huu ulimwengu, katika huu mwili, hatuishi kwa kutenda kulingana na mwili- 2 Wakor.10:3( pata maelezo ya ndani katika ujumbe uitwao, “ kusudi la mwili”). Katika hayo maisha ambayo tumeyaacha (ikiwa kweli tumeanza maisha ya kiroho), tulikuwa tumeukabidhi mwili wetu na viungo vyake kutumike kwa uchafu na uasi, na katika kuasi- Warumi.6:19. Ndiyo, tulikuwa hatujui kama kuna goli nyingine isipokuwa hiyo ya kufikia viwango vya ulimwengu wa sasa. Kwa vile sasa tumehamisha akili zetu huko, na kuziweka kwenye hii goli mpya itokanayo na kuufahamu ukweli, basi sasa hivi, tumeukabidhi mwili wetu na viungo vyake kutumika kwa haki katika jitihada la kuoshwa (kutakaswa)Warumi.6:19, sehemu ya mwisho. Kuoshwa nini? Kutoa kabisa ule ufahamu wa uongo, nia zake, maongezi yake, na tabia zake, na kuwacha kabisa kutumia vile vifaa vya kimwili tulikuwa tunatumia kuifikia hiyo goli. Vifaa gani hivyo? Mali, kukubalika na kuidhinishwa na watu, ukuu, viwango vya ki-elimu, na kujihuzisha na vile vistareheshavyo mwili nje ya maagizo ya kweli. Wandugu wapenzi, tukifanya hivyo, tutagundua kwamba, katika kila hali, iwe nzuri au mbaya, tunayo neno la Mungu linalotufundisha vile tunapaswa kutenda- 2 Tim.3:16-17; Isa.48:17; neno ambalo, kila unapolitumia, hauwezi kukosea maana, uendapo, hatua zako hazitazuiliwa, wala ukipiga mbio, hautajikwaa- Mith.4:12; eee, hakuna vikwazo, maana hili neno ni taa, na ndilo linatuchunga-Zab.119:105,9.

MTIHANI

Kufikia hapo wandugu, vikwazo vimetuishia kwa sababu tunatembea katika kweli, tunatenda kulingana na ufahamu na sio uongo; kwa hivyo, matokeo yake ni Amani na uhaki; ni kutembea kwa njia yenye nuru ing’aayo(kuongezeka kwa ufahamu), ikizidi kung’aa mpaka kufikia mchana mkamilifu(kuwa kama Mungu)-Mith.4:18. Hata hivyo, ijapokuwa tumeamua na kuanza kuishi njia isiyo na vikwazo, tunaishi  katika ulimwengu uliojengwa( kama vile tumeona) juu ya uongo ambao ndio unaoleta vikwazo, na tumezungukwa na watu ambao bado wanaongozwa na mwenye kuuanzisha na kuuendesha, ambao, mungu wake( Shetani) amepofusha akili zao( bado wanauishi huu uongo)-2 Wakor.4:4. Na pia huyu mungu wake ambaye ni Shetani anahusiana na hii miili yetu-Wag.5:17 kama vile tuliona( soma ujumbe wa, “ Wa ulimwengu gani?”, kwa maelezo Zaidi), kupitia kwa akili yake-Warumi.7:22-23 ambayo pia ufanya kazi ndani ya hii miili yetu. Sasa, kwa mioyo yetu yote, tumejitoa kuishi kulingana na kweli kama anavyotufundisha Mungu kupitia kwa neno lake. Lakini huyu hapa mke, au Bwana, jirani, m-ajiri wako, mwalimu, eee, mtu yeyote unayehusiana naye ambaye bado anaishi kuufuata huu uongo. Saa yote anakujia kutaka mshirikiane kwenye hayo maisha uliyoyaacha. Anapinga bidii zako za kutenda haki. Shetani naye, kupitia kwa hii miili yetu, anaamsha hiyo akili yake inayohusiana na hii ambayo inatumika na hawa wanaokujaribu-War.7:23. Utakuta kwamba hii hali inaamsha vikwazo huku tukijipa sababu ya kuvikubali, kwa kuwalaumu hao ambao vinakujia kupitia kwao. Utasikia tukisema, huyu ndiye alinikasirisha, ananidhulumu, amenitukana ameninyang’anya………..na kunifanya nikosee. Tunapofikiria kwa njia hiyo, je, tunaongea ukweli? Hilo fikiria iliokufikisha kwenye kukasirika baada ya kukosewa ilitoka wapi? Kwa neno la Mungu ambalo ndilo unaitumia sasa kufanya chochote ufanyacho? Asha hata kidogo.

LINDA MOYO WAKO

                       Tuliona vile Mungu uishi maisha yake bila masharti yoyote; vile anaishi maana ameyapenda kuliko mengineo yoyote yale. Kwa vile anataka kutufanya kuwa kama yeye, basi ni lazima tufikie huo ufahamu ambao utatuwacha pia tukiyapenda kama yeye; sio ili tuonekane, wala kutuzwa kwa namna yeyote ile mbali, kwa kuwa tumeyagundua kuwa mema kuliko mengineo yoyote yale, hatuna mengine ya kubadilishana na hayo. Hii ndiyo sababu alimwacha Shetani na hawa maajenti wake wawe pamoja nasi hapa duniani, ili kutujaribu, kwa kutushawishi tuungane nao katika hayo tulioyaacha-Yakubu.1:2; ili ajue kwa hakika kama tumeamua kwa vyovyote vile kuishi kama yeye, kwa kumtii huku tukikataa ushauri wowote wa Shetani kupitia kwa hii miili yetu, au hawa wanaotuzunguka-waamusi.2:22.  Kumbuka vile tulianza kuona, vile haya maisha ya kimwili, yana goli ya kupata mali nyingi kushinda wote, kuwa juu kushinda wote, kuheshimiwa na kusifiwa huku tukihithinishwa na wote, n.k. Tukaona vile, tunapokosa kuonekana au kutendewa hivyo, tunakwazika. Basi, kila mmoja wetu na afahamu na kuelewa kwamba, kila unapojiona ukikasirika, kuchukizwa, kuona haya, na mengine mengi ya aina hiyo ambayo ndiyo chanzo cha vikwazo, fahamu kwamba saa hiyo, umetoka kwenye ile akili ya kiroho, na kurudi kwenye ile ya kimwili ipiganayo vita na hiyo ya kiroho-Wagal.5:17. Wakati huo, umeanza kung’ang’ania ile goli uliyoiacha ya ukuu wa ulimwengu huu. Mungu akiyaelewa hayo, huyu hapa akitutahadharisha tulinde mioyo yetu kwa nguvu zetu zote, maana huko ndiko uzima unakotoka-Mith.4:23. Tutafaulu kufanya hivyo kwa njia gani? Ndugu zangu, tukumbuke kila wakati kwamba tunayo goli mpya ambayo vifaa vyake na utajiri wake ni vya kiroho. Hii ndio sababu Kristo anatushauri tuweke hazina yetu  mbinguni( mahali tumeketi pamoja na kristo-Waef.2:6), ambapo kutu, nondo wala wezi( hakuna umwili unaweza kuifikia) haviwezi kufika, na kuharibu, maana hazina lako lilipo ndipo moyo wako ulipo-Mat.6:20. Tukifanya hivyo, tutakuta kwamba tunachopigania ambacho tukikikosa, kitatukasirisha, kutuhudhi, kutuchukiza, kutuogofya, n. k, ni kuishi kwa kutii neno la Mungu ambalo ndilo maisha na tabia tunayoumbika sasa. Hivyo basi, hatutakubali akili au mioyo yetu itumike nje ya hilo neno maana hatuna ufahamu wala maisha mengine. Hali saa yote tukiwa kwenye ufahamu wa kuwepo kwa Shetani katika miili yetu, katika wanadamu walionasi hapa, tutakuwa waangalifu kila wakati tunapofikiria, kutamani, kupanga na kutenda, au kuongea. Tutajitahidi Kuona kwamba tumefanya hivyo kwa kutumia neno la Mungu-Zab.119:9. Mtu amekunyang’anya, amekutusi, amekudharau hata kukuaibisha mbele za watu, yako itakuwa kung’ang’ania kutumia hiyo hali kujifunza kuishi kama Mungu kwa kukumbuka vile asemavyo, ambavyo ndivyo unapaswa kufanya kumtenda huyo mtu. Tutakuta kwamba mtu ufikiria na kutenda kulingana na ile akili iliyo ndani yake. Walimwengu wako na akili ya Shetani yenye vikwazo chungu nzima, ile itendayo kazi katika wana wa kuasi-Waef.2:2. Sisi tunaoifuatilia hili goli la kiroho tunayo akili ya Mungu-1 Wakor.2:16, ile iletayo Amani na uhaki, ambayo utokana na, kuangalia kutenda sawasawa na sheria yote( neno la Mungu), bila kuiacha mkono wa kuume au kushoto, upate kufanikiwa kila uendapo,….Joshua.1:7-8. Hayo yote tunafanya, maana goli letu sasa ni kuufikia ule mwili usioharibika na wenye uzima wa milele ambao ndio bidii yetu yote, maana, twaugua tukitamani kuvikwa, ili huu uharibikao umezwe na uzima( wa kutokuharibika)-2 Wakor.5:6. Kukosa mali kutakuzuia kuifikia hiyo goli? Madharau na aibu za wanadamu, uongozi na heshima za watu, vina mchango wowote katika kukuwezesha au kukuzuia kuifikia au usiifikie hili goli mpya? Wapenzi, ikiwa kweli tumekufa pamoja na kristo, na tunaishi naye kwa kuishi yale maisha anayoishi kule mbinguni-Wakolo.3:1-3; wafilip.3:19, basi, hatuna kingine cha kulinda na kutetea isipokuwa kuishi amri za Mungu.  Katika huku kuishi, atung’ang’anii, wala kupigania kujiimarisha kimwili, maana mawazo yetu yamehamia kwenye huu mwili wa kiroho ambao tumeahidiwa, na maisha na bidii zetu zote zimehamia huko. Hii ndiyo sababu pia, kung’ang’ana na kupigana kwetu sio dhidi ya watu, wala hatutumii silaha za kimwili. Vita vyetu viko ndani ya akili zetu-War.7:23; tunapigana na Shetani na malaika wenzake-Waef.6:12.  Kama ni hivyo, viwapi vikwazo vitokanavyo na wanadamu, mali, au huu mwili wetu? Haiwezekani kabisa kukawa vikwazo vyovyote kwa mtu ambaye goli lake ni kuufikia huu mwili wa kiroho, na uzima wa miele, maana ufahamu, nia, fikira, mipango, matendo na hata maongezi yake, vyote vimehamia huko kwenye huo ulimwengu unaokuja-Waeb.11:10; 1 Petro.2:11; 2Petro.3:13. Kile kitu mtu wa aina hiyo anachopigana nacho, ambacho umuogofya, ni kuhakikisha hajatenda chochote nje ya neno la Mungu. Akisha fanya hivyo, anafahamu kabisa kuwa, mengine ya kimwili, Mungu atayafanikisha kupitia kwa zile kazi afanyazo, maana, kazi ya Mungu ni kumshughulikia mtu wa aina hiyo; na tena, chochote afanyacho ufanikiwa-1 Petro.5:7; Zab.1:3. Haya yote yanakubaliana na alichokinena kristo akisema kwamba, tukiutafuta ufalme na uhaki wa Mungu( yaani, tukiendelea na haya maisha ambayo kwa ajili yake tuliumbwa), vitu hivi vya kimwili vita kuwa vyenu pia, maana Mungu aliviumba vitumike na huu mwili, lakini ndani ya neno lake-Mat.6:33. Namalizia kwa kuwakumbusha kuwa, kila aina ya kikwazo uja wakati mtu amerudi katika mwili na kuwacha kufuata maagizo ya kiroho, maana Mungu ananena wasiwasi kwamba, wana Amani kuu wale wazishikao amri zake; hakuna cha kuwakwaza-Zab.119:165.  Ikiwa kwa hakika tunatafuta kuifikia hili goli la kiroho, basi, mioyo yetu itajawa ne fikira, nia, na mipango ya vile tutaifikia. Na kwa vile hiyo mipango ni neno la Mungu, basi, hili ndilo kile kifaa ambacho tutapigania kuwa nacho moyoni ( silaha ya kiroho-Waef.6:17) ambacho kwetu, kina thamani kuliko fedha na dhahabu; eee, hakuna kitu chenye faida inayolinganishwa na hili lake- Zab.119:72; Mith.8:18-19.  Unataka kuishi bila vikwazo; kuishi maisha yaliyo huru, yenye furaha na Amani, shika amri za Mungu, maana haya ndiyo maisha yakupasayo kuishi-Isa.48:17. Ni sauti ya muumba wako, ikinena katika Kristo kupitia kwa mtumishi wake, KANISA LA MWISHO LA MUNGU: TOVUTI(WEBSITE)  >www.endtimecog.org:BARUAPEPE>endcog@gmail.com:  Kwa anwani Zaidi kuhusu maeneo mengine ya mawasiliano, fungua website yetu, kwenye faili ya MAWASILIANO.

 

 

 

 

 

                      

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *