Kama tungeulizwa ni kwa nini tuliumbwa katika huu mwili wa nyama na damu, tungepeana sababu gani? Tujiulize; ni kwa nini tuliumbwa katika huu mwili na tunapaswa kuwa tukifanya nini sasa ili tuifikie hilo lengo? Kabla hatujaanza kutoa majibu, ni vizuri kwanza tuwe na mambo mawili kwa akili zetu. Ya kwanza: wasomi katika utafiti wao wamegundua kwamba, uhai ni lazima utokane na uhai mwingine. Kitu kisicho hai akiwezi kukifanya kingine kiwe na uhai. Pili: Kwamba, kila jambo ina chanzo chake. Kwa hivyo, kila kitu tuonacho, kusikia, kushika,na ata sisi wenyewe, tunao kile kilituanzisha tukawa viumbe hai( na hapa, nawakaribisha msome ujumbe uitwao, “ Mungu wa keli wa pekee” kwa maelezo Zaidi). Basi, hali tukiwa na hayo mawili kwa akili zetu, hebu sasa turudi kwenye somo letu. Huu ujumbe ni kwa wote waaminio kwamba kunao Mungu mbinguni, na ndiye tunayehusika naye, na ndiye anayeongea hapa. Mungu ndiye, “….aliyeumba vitu vyote-Waef.3:9; Matendo.17:24”. Hii ni kusema kwamba, ule uhai ambao ulisababisha uhai wote, ni Mungu. Kwasababu vitu vyote vinahuzisha ata na mwanadamu, basi huyo Mungu anasema alituumbia huu mwili kwa nini? Hebu tufuatilie, na kama ilivyo kusudi la huu ujumbe, hebu kila mmoja wetu ajichunguze anapoendelea kuusoma, ili kuthibitisha kama kweli tunaishi kulingana na kusudi la Mungu la kuumba huu mwili. Akithibitisha tunachosema hapa, Mungu anasema, “ ni mimi niliumba dunia, na kumuumba mwanadamu juu yake- Isa.45:12”. Wa nini?
KATIKA ULIMWENGU WA SHETANI
Wakati Mungu alikuwa akimuumba mwanadamu, Shetani na malaika wenzake walikuwa wameasi tayari( ujumbe wetu uitwao “shetani ni nani?” una maelezo Zaidi. Utaupata katika Website yetu, www.endtimecog.org). Mungu alikuwa ameuondoa ufalme wake hapa duniani na kumwachia Shetani aendelee kuitawala, na mpaka sasa, bado ni shetani anayeitawala-soma waef.2:2; Ayubu. 9:24; Waef.6:12. Hivyo basi, katika mpango wake wa kuurudisha ufalme wake hapa duniani, “Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake, ili, aweze kuitawala dunia- Mwa.1:26-7”. Tunaelewa kuwa, mwili huu wa nyama na damu hauwezi kuingia wala kuurithi ufalme wa kiroho- 1 wakori.15:50; Yohana.3:3. Kama ni hivyo, mwanadamu atawezaji kuutawala ufalme wa Mungu akiwa wa asili ya mwili? Rafiki, eleweni na kufahamu ya kuwa, tuliumbwa viumbe wenye uhuru wa kuchagua, na hivyo tunao uchaguzi wa kufanya katika kila hatua tunayochukua. Kufuatana na hayo, basi inambidi kila mtu achague kama atapenda kuwa kama Mungu kabla Mungu hajamfanya kuwa kiumbe wa kiroho. Kwa sababu ya huku kuchagua, Mungu alimwacha Shetani aendelee kuitawala dunia, kwa ajili yetu, “ Ili kwa yeye, amjaribu mwanadamu, aone kama atamtii au la- waamuzi.2:22; Kumbukumbu.8:2; Mat.4:4,7,9(mfano wa Yesu)”. Basi jueni kwamba, ni kwa sababu ya huku kujaribiwa na kufanya uamuzi, huu mwili uliumbwa( soma maelezo ya ndani kuhusu hili jambo katika ujumbe wetu uitwao, “Msingi wa milele”). Ni kwa njia gani huu mwili unasaidia mwanadamu kufanya uamuzi na kuumbika taia?
MAUMBILE YA SHETANI
Hii miili tulionayo tutaifananisha na nini? Tutaifananisha na chanjo, ambayo daktari uwachanja watu ili kuzuia kuambukizwa ugonjwa Fulani. Kile daktari huwa anatumia kuchanja kama dawa, huwa hasa ni viini vya ugonjwa wenyewe; ndivyo anaweka ndani ya mwili. Hivyo viini utahadharisha na kuzoeesha mwili kupigana kasi kwamba, ugonjwa wenyewe ukijaribu kipenya, mwili tayari unauelewa na unaupiga mara moja. Labda hatujawahi kuelewa hivyo, lakini sasa, jueni kuwa kusudi ya huu mwili ni kutuzoesha kupigana na Shetani. Hakuna vile tutamdhihirishia Mungu kuwa tunataka maisha yake ikiwa hakuna aina nyingine ya maisha yanayotuvutia, huku yakipingana na hayo ya Mungu. Twajua ya kwamba, shetani ni mpinzani wa chochote kiitanishwacho na Mungu. Kwasababu hii, Mungu aliuumba huu mwili ukiwa na hayo maumbile ya shetani ya upinzani, maana anatuambia, “…. Ni mwili wa mauti- Warumi.7:24; ….kuwa, hakuna kitu chema ndani ya huo mwili-Warum.7:18; kuwa ni uadui kwa Mungu na hauwezi kumtii-Warum.8:7; ……..kwamba, kila aamuaye kuishi maisha ya Mungu uanza vita na huo mwili-Waef.5:17”. Hata hivyo, Mungu alimweleza adamu, na mpaka saa hivi, huu ujumbe ni jitihada zake za kutueleza hayo. Basi ,baada ya kumuumba Adamu, alimwachia nafasi ya kuamua, akamwekea hayo maisha mawili mbele yake; maisha ya uzima wa milele( mti wa uzima) na maisha ya mauti(mti wa ujuzi wa mema na mabaya). Baada ya hapo alimuonya akisema, “ lakini siku ile utakula ya mti(kuishi kama shetani) wa ujuzi wa mema na mabaya, hakika utakufa-Mwa.2:17”. (pata maelezo Zaidi kutoka kwa ujumbe uitwao, “miti miwili”). Ijapokuwa Mungu hajasema waziwazi kuwa huu mwili umeumbwa kwa hizo tabia za dhambi, kunao vifungu vinathibitisha hayo maana, Bwana anatuambia, “kuiweka akili yako katika mwili ni mauti; Na tena, haiwezekani kumpendeza Mungu mtu akiishi kuufuata mwili.-warumi .8:6,8”-linganisha hayo na Mwa.2:17. Lakini kwa nini Mugnu atushikanishe na mwili wa kutuuwa? Kila ninapotembea nikihubiri, hili ni swali nimekumbana nalo kutoka kwa wengi. Eee, wengi ushangaa ni kwa nini Mungu hakumwondoa Shetani baada ya kumuumba mtu?
KUUMBIKA TABIA
Tunajua kuwa, Mungu anao ule mpango anaoutumia kumuumba mwanadamu ata amfanye kiumbe wa roho. Huu mpango unachukua hatua tatu. Ya kwanza ni huu mwili tulioumbwa nao. Ya pili ni ni kuumbwa akili na tabia za Mungu wakati wa haya maisha ya kimwili, nah ii ni baada ya mtu kuchagua kuishi kama Mungu. Ya tatu na ndio ya mwisho ni kuubadili huu mwili wa nyama na kupewa wa kiroho, na hii ni kwa wale tu watakaofaulu kuumbika hii akili na tabia ya utakatifu wakati huu wa mwili wa nyama. Kila mtu ambaye , kwa hiari yake mwenyewe ameamua kuishi haya maisha ya Mungu, ameingia kwenye hatua ya pili ya kuumbwa kwake. Kwa hao, Mungu ameweka roho yake ndani yao, ili awape nguvu ya kuelewa na kuishi hayo maisha, ambayo, kwa kusizitiza, hayo maisha yanakuwa mazoea, na kwa njia hiyo, tabia inaumbika. Kuanzia hapa,inampasa kila mmoja wetu kuwa macho,na kujiangalia na kuona ni njia gani anaenenda kwayo; kama ni ile ya kimwili ambayo itakuuwa, au ni ile ya kiroho ambayo itakupa uzima wa milele, maana Bwana anatuambia, “kuweka akili katika mwili ni mauti, mbali kuweka akili katika roho ni uzima, na Amani- Warumi.8:6”. Mungu yuko vile alivyo maana aliamua kuwa hivyo kwa hiari yake. Ili mwanadamu awe kama Mungu, inambidi achague kuwa hivyo kwa hiari yake mwenyewe, achague kati ya mwili, kati ya watu wanaomzunguka( yeye na watu wakiongozwa na Shetani- ‘mti wa ujuzi wa mema na mabaya), na uzima( roho) kama anavyoongozwa na Mungu katika neno lake(mti wa uzima-mithali.3:18). Punde tu anapochagua uzima tunapopokea hii roho takatifu,na vita vinaanza, maana, “mwili utamani ukipigana na roho, na roho ikipigana na mwili, maana hivi viwili upingana-Waga.5:17”. Kama unataka kujua, basi elewa kuwa, huu uamuzi ni jambo la kila wakati. Katika kila tufanyacho, kila upande unaleta mawaidha yake, na ni lazima tuchague ni waidha gani tutatumia(kama ni ya mwili au roho), maana, “kila natakao kutanda mema, maovu unizingira. Kwa sababu natamani amri ya Mungu kwa roho yangu(waitha la kiroho), lakini naona sheria nyingine katika mwili wangu(waidha la kimwili) ikipingana na ile ya roho- Warumi.7:21-23”. Ule uamuzi tufanyao kati ya haya mawili ndio uonyesha zile tabia tutaumbika, “ iwe ni za dhambi ziletao mauti ,au za utiivu ziletao uhaki na uzima-Warumi.6:16”. Tuna jua matunda ya kuishi kimwili vizuri sana– ona wagalatia.5:19-21. Hii nawaambia ili tusiwe na kubaatisha kuhusu kile tumechagua ambacho uonekana kwa zile tabia tunazoonyesha kwa maongezi, mafikira na matendo yetu ya kila siku, kwa kila tutendacho. Hata kabla hatujaendelea, naamini sababu ya Mungu kumwacha Shetani aendelee kuwa mtawala wa Dunia imeanza kuwa wazi, ikiwemo pia sababu ya kuuumba huu mwili.
KUTEZEKA NA KIFO
Wandugu, Mungu anatupenda sana kiasi kwamba hataki tukose uzima wa milele. Anataka kuishi nasi kama watoto wake milele. Basi, anatufundisha katika kila hatua ile namna ya kutuumba hata tuifikie lengo lake ambayo ni ya kutufanya viumbe wa kiroho kama yeye. Je, si ni hajabu, Mungu kuwa anataka tuufikie uzima halafu anatuumbia mwili ambao mtu akiufuata atakufa? Sio hajabu ata kidogo ikiwa tunaelewa jinsi tabia anavyoumbika. Ili tabia iumbike, ni lazima kwanza mtu achague kupenda na kuumbika hiyo tabia. Baada ya kuchagua, ni lazima tuanze kutenda tukijizoesha kuishi hivyo.Hii huitaji adabu, ambayo inao kujizuia kwingi, maana Mungu anatuambia, “Ni kwasababu ya adabu tunapaswa kufumilia……..Mungu anatuadabisha kwa faida yetu wenyewe, ili tuweze kushiriki utakatifu wake. Kwa sasa, kila kuadabika kunakuwa kuchungu badala ya kufurahisha; baadaye uleta matunda ya uhaki na Amani kwa wale ambao wameadabika-waeb.12:7-11”. Je, tutaifikia Amani kwa njia gani tunapopitia njia kali namna hii? Amani, furaha, na hata Baraka za kimwili ni matunda yajao kwa kutii amri za Mungu.Hii itawezekanaji ilhali tuko katika hii miili isioweza kutii? Jueni na kuelewa kuwa, furaha yetu uja kwa njia ya hayo matezo, maana, “…utulivu wetu uja wakati tu tunapo fumilia mateso- 2 Wakori.1:6”. Matezo yapi? Kama vile tulivyoona, kila wakati tunatii roho(amri za Mungu), mwili uwa unatezeka ukitamani kutimiziwa haja zake. Tukikumbuka kwamba, maisha ambayo tuliyaishi awali ni yale ya uongo wa Edeni, ambao ulitufanya kudhania sisi ni miungu; hii ilitufanya tujipangie njia zetu za maisha, ambazo ni kulingana na, “ tamaa za mwili(kinyume na roho), tukifuata mwili, na tukawa wana wa gadhabu-Waef.2:3”. Kwa hivyo, tunapomtii Mungu, hatujipingi sisi wenyewe tu, mbali tunajikuta tukienenda kinyume na wote waliokuwa marafiki katika mwili, na, “…. Wao utuchukia- 1 Petro.4:4”. Huu mwili unapenda ushirika na kuungwa mkono, ambako kunapatikana tu ikiwa mtu atakubaliana na mwili, au na wale wanaomzunguka( Agiza ujumbe wetu uitwao, “siri ya kushinda”, upate maelezo ya ndani Zaidi. Utaupata katika Website yetu, www.endtimecog.org, au kwenye vituo vyetu vya usambazaji). Lakini mtu akimgaukia Mungu, hawa wote umgeuka, kumtenga, kumnena vibaya, hata kumnenea uongo. Hebu uwe wazi na uongee ukweli. Je, Tunakuwa na furaha wakati tunatukanwa, kuitwa mashetani, na kulaumiwa kwa vitu ambavyo hatukufanya? Kwa kweli hatuwezi kufurahia. Inauma kweli kweli. Lakini sasa, njia ya pekee ya kuepukana na hayo maumivu ni, kuungana na hawa katika njia zao kunyume na Mungu. Pia ni kuenenda kuufuata mwili ambao vile tumeona, hauwezi kumtii Mungu. Lakini sasa, sisi ni watu ambao tumechukua uamuzi wa kujifunza kuishi kama Mungu. Kwa hivyo, ni lazima tuupinge mwili, na hata watu wanaotudhulumu, na kumtii Mungu. Huku kupingnana na mwili na watu ndiko kunaleta maumivu lakini katika raha kuu itokanayo na roho takatifu iliyo ndani yetu- waga.5:23. Wandugu, kama hatutaukana mwili(ubinafsi) kuishi katika roho hakuwezekani. Huku kujikana ndiko kunaleta matezo katika mwili, lakini kukileta pia furaha ambayo uwa wakati tunaendelea kuushinda na mabayo haiwezi kufananishwa na ile ya kimwili-Zab.4:7. Hivi ndivyo tunavyoubika tabia, maana, “…tunafurahia katika tumaini letu( tukitazamia ahadi za Mungu) letu la kushiriki utukufu wa Mungu. Zaidi ya hayo, tunafurahia matezo yetu…Warumi.5:3”. Je, mtu awezaji kufurahia katika matezo? Ndugu; tuko vitani, tuko katika chumba cha mtihani. Sasa niwaulize hivi; ‘ ni yupi kati yetu ambaye hafurahii wakati anafaulu katika mtihani? Au, ni yupi kati yetu ambaye hafurahii anaposhinda adui katika vita? Lakin hatutaweza kufurahia ikiwa hatuujui huu mwili kuwa mbaya, wenye kudanganya katika nia zake, na wenye kutupotosha, hivyo kuona haja ya kuusulubisha- wagala.5:24. Kwa hivyo, hii miili ni kitu tunapaswa kuogopa na kukipinga,na kuisababisha itezeke( kwa kutokufuata tamaa zake), huku tukifurahia tunapoishinda na kuendelea kutenda yale mema, maana kwa kuendelea kuushinda, tunaendelea kutenda ya kiroho na kuumbika hiyo tabia ya Mungu. Hii ndiyo sababu Bwana wetu anatuambia, “…tukijua kwamba, kutezeka kunaleta uvumilivu( hakuwezi kuwa na uvumilivu,isipokuwa kwanza kuwe na mvuto unaopinga ule wema tunaotaka, na huu mvuto ndio tunaoupinga, kwa uvumilivu tukiendelea na wema-Warumi.2:7), na uvumilivu uleta (nini?) tabia, nayo tabia ikija utuletee tumaini—Warumi.5:3-4”. Je, tunataka kufaulu katika hii shule ya kuuendea uzima? Kama ndio, husiuunge mwili mkono, maana huu ndio adui yako mkubwa, ambaye anatumika na Shetani kukuhifadhi katika uharibifu ili mwishowe ufe. Labda unafikiria hatujui tusemacho? Unadhania tunafundisha kinyume na ile injili Yesu alifundisha? Yeye mwenyewe hakuwa na dhamana na huu mwili, hakuwa na haja na mambo ya watu, wala, hakuona haya wakati wanamtukana, kumdharau au kumtenga, maana alijua upofu wao. Aliujua huu mwili vizuri, na kwa hivyo, hakushikamana nao, maana, “….alitezeka katika mwili- 1 Petro.4:1”. Ni kitu gani kilisababisha hayo matezo? Huu mwili unao starehe zake; unapenda heshima za watu, kuungwa mkono, kutukuzwa N.K. Lakini kwa vile alimtii Mungu, hivyo kuukana mwili ambao wote wanaomzunguka wanaishi katika huo, basi, “…walimchukia kwa kuwa aliwaambia matendo yao( furaha za mwili) ni maovu-Yohana.7:7”. Kwa vile, kulingana na uongo wa Edeni, mwanadamu ni kama Mungu, basi kwa kuwaambia wao sio miungu mbali ni mavumbi, waliona hiyo kkuwa madharahu na matusi. Kwa sababu hiyo walimpinga kwa kila namna. Kwa hivyo, ilimbidi, “… kuvumilia uadui mkubwa kutoka kwa watu-Waeb.12:3”. Leo, watu wakikuita Shetani, sidhani kama utawahi kuwaongelesha tena, maana katika huo uongo wa Edeni, mtu upenda tu kunenwa kwa wema peke yake. Lakini, hebu mwangalie Yesu, “….Mafarisayo walimnena Yesu kuwa mwenye mashetani, aliye na wazimu, na anayetumia nguvu za shetani kwa uponyaji wake-Mat.12:24;yohana.10:20”. Je, aliwakasirikia? Ata kidogo, maana aliwaambia, “…mimi sina pepo mbaya, lakini namtukuza Baba yangu- Yohana.8:49”. Ni kitu gani kilimfanya Yesu hasiudhike na matusi yao? Maana lengo la maisha yake haikuwa kwa huu mwili wakujikweza( uaminio kuwa kitu na hali sio kitu-Wagal.6:3), ambao ndio uona uchungu unaponenwa vibaya. Alijua ujinga wao, na kwa hivyo, aliweza kuwavumilia huku akiwahurumia tu, maana hata wakati alikuwa msalabani akiwa karibu kufa, alisema, “…wasamehe, kwa kuwa hawajui walitendalo- “. Alituachia kielelezo tuweze kuiga, huku akituonya dhidi ya matezo ya mwili kama yake, aliposema, “Nimewaambia hayo, ili yatakapokuja, mkumbuke kuwa niliwaambia”. Vitu gani? “ Duniani mtapata dhiki, lakini jipeni moyo, maana nimeushinda ulimwengu- Yohana.16:4,33”. Pia, aliwaonya wale watapenda maisha ya mwili na starehe zake(kinyume na neno la Mungu) akisema, “maana atakayeiokoa nafsi(mwili) yake, ataipoteza, lakini aipotezaye( kwa kuinya tamaa zake) nafsi yake, ataiokoa-Mat.16:25”. Wandugu, hili ndilo kusudi la huu mwili, la kupinga roho ya Mungu ndani yetu, ili watakaofaulu kuupinga huku wakifuata maagizo ya roho, waumbike hio tabia takatifu. Kwa njia hiyo, tunaendelea kuumbika tabia ya Mungu tukibomoa ile ya mwili, ata kama ni kwa kufa, maana Kristo aliye mfano wetu pia aliuvaa mwili, “ kwa sababu ilimpasa, Yesu ambaye, kwa yeye, vyote viliumbwa, na kwa yeye vyote pia vyaishi, kwa kusudi la kuwalete wana wengi waufikie utukufu, aukamilishe wokovu wao kwa njia ya matezo. Kama vile hao wana wanao mwili wa nyama, ilimbidi pia yeye kuuvaa huo ili( kwa sababu gani?), kwa kupitia kifo…….heb.2:10,14”. Wandugu wapenzi na washirika wangu katika tumaini la utukufu ulio katika Kristo, sihitaji kudumu kwenye haya maelezo Zaidi maana naona kufikia hapo, uelewa wa kutosha umekuwa. Ninachosema ni kwamba, “ Tunao wingu la mashahidi, wale waliotutangulia katika haya maisha-Waeb.12:1”. Tukianzia na Yesu mwenyewe, walijaribu kumfanyia kila aina ya ubaya, kila aina ya aibu, matezo mpaka mwisho wakamuua, na hii yote ilikuwa ni bidii ya Shetani ya kumfanya akubaliane na mwili ili afe, na hivyo, asiweze kutufungua macho ili na sisi tuendelee kuufuata mwili na kufa pia. Lakini Kristo aliukana mwili, “……Huku akikumbuka furaha iliwekwa mbele yake, aliipuusa aibu, akaufumilia msalaba, na hivyo akafaulu kukaa mkono wa kuume wa baba kwenye kiti chake cha enzii- Waeb.12:2”. Hayo yote, aliyapitia ili atuonyeshe vile Shetani uutumia huu mwili kututoa kwenye mikono ya muumba wetu ikiwa tutaufuatilia na kuutimizia tamaa zake. Je, kama yesu, tutaukana mwili na Shetani , na tumfuate Yesu kwenye njia ya uzima wa milele? “Hakutenda dhambi yeyote; udhalimu haukusikika mdomoni mwake. Alipodhihakiwa( jambo la kumfanya mtu kuona haya na kujitetea), hakurudisha dhihaka; alipotezwa, hakutisha,….1 petro.2:21-23”. Baada ya Kristo, walikuja mitume ambao pia walifuata nyayo zake, na ambao hao ndio mababa wetu wa kiroho. Eeh, kama Yesu, “…tukidhihakiwa, twabariki, tukiteswa, twavumilia, tukisengenywa, twasihi….1 wakori.4:12-13”. Ndio, “…tumekuwa watu ambao ulimwengu hauwapendi kabisa- Waeb.11:38”. Kumbukeni kuwa, hawa mitume na manabii ndio mababu zetu kama kanisa, maana, “tumejengwa juu ya msingi wa manabii, na mitume, Kristo mwenyewe akiwa jiwe la pembeni-Waef.2:20”. Haya matezo yote waliyapata kwasababu ya kuukana mwili,ambao ndio hasa unaitanishwa na ulimwengu-1 Yohana.2:16. Ndugu yangu, je, unataka kuusikia ukweli, au unatak kile kitu umezoea? Huo mwili wako na aina yake ya maisha kama yanavyoelekezwa na Shetani, ndio ujumlishwa na kuitwa ulimwengu na ndio tunapaswa kupigana nao; na kwa vile watu wote uufuata mwili, basi kila aamuaye kuupinga “…ujifanya kuwa adui-Isaya.59:15”. “Au hamjui kuwa urafiki wa ulimwengu(mwili) ni uadui kwa Mungu? Kwa hivyo, kila apendaye kuwa rafiki wa ulimwengu uwa adui wa Mungu-Yakubu.4:4”. Kama ni hivyo, basi ni nani ataweza kuepuka na tumeumbwa kwa huu mwili-eee, sisi na huu mwili ni kitu kimoja?
KAZI YA MUNGU
Mungu anaelewa vizuri sana vile sisi ni mijengo ambayo bado ujenji wake haujakamilika-1 Wakori.3:9. Pia, anaelewa vile mjengo hauwezi kujikamilisha. Bwana Wetu Yesu anayathibitisha hayo akisema, “….bila mimi, hamwezi chochote- Yohana.15:5”. Basi, ikiwa tutakubali kwamba sisi ni mavumbi kama walivyokubali mababu zetu-soma Mwa.18:27; Zab.103:14; Ayubu.14:2-3, na tukubali unyonge wetu, na kujua hakika kuwa ni Mungu pekee awezaye kutukamilisha, tutawacha kabisa kujiongoza kulingana na mawazo yetu, na kumakinika na neno la Mungu. Ikiwa basi tumemruhusu Mungu aendelee kutuumba, tunapaswa kuwacha, “….. kutenda kulingana na vile aitha sisi au watu wanapenda, na kumtazamia Mungu kwa kila ushauri- Mith.3:5”. Ningekuomba uweze kusoma ujumbe uitwao, “Je, wewe ni Mkristo?”, upate maelezo Zaidi. Lakini sasa, Mungu yuko wapi ata tuweze kumwendea atupe ushauri? Kristo anasema, ;mmesha kuwa wasafi kwa ile neno nimewaambia. Hivyo basi, kaeni ndani yangu nami ndani yenu-Yohana.15:3-4”. Eti tukae ndani ya Yesu? Tutawezaji katika hii miili ambayo haiwezi kutenda mapenzi yake? Je, kweli tunatamani kukaa ndani yake, ili atukamilishe na kutufanya viumbe wa roho, hali ambayo itatuondolea udhaifu wote na kuangamiza kifo milele? Kama tunatamani, basi Mungu yu hapa akitufundisha na kutuonyesha njia. Msikilize tafadhali. “ Mwaweza kufaulu; si kwa nguvu wala uwezo wenu, mbali ni kwa roho yangu, asema Bwana-Zekaria.4:6”. Ni kwa nguvu za roho ya Mungu, ambayo kwa hiyo pia tuliumbwa, na ndiyo uhuisha vitu vyote-Waeb.1:3, na ndio pia sheria ya Mungu ikiwa mioyoni(yohana.6:63). Kwa hivyo, tukifuata maagizo ya hiyo roho, “..tutaziharibu ngome(tamaa za mwili). Tutavunja mabishano(mawazo pinzani-Warumi.7;23), na kila kujikweza kujikwezao dhidi ya ufahamu wa Mungu……na kuvishika mateka vimtii kristo- 2 Wakor.10:4-5”; “……ili matendo ya haki ya sheria yatimizwe kwetu sisi tusioenenda kwa kuzifuata tamaa za mwili mbali kwa kuzifuata nia za roho-Warumi.8:3-4”. Kunao maelezo yaliyo wazi, na dhahiri kupita haya? Ni Mungu aliyepanga kutuumba. Ana hamu sana ya kuimalizia kazi aliyoianzisha ikiwa tu, tutamruhusu. Hii ndiyo sababu sio kazi yetu mbali ni yake maana sis ni mpango wake. Kwa hivyo, yeyote atakaye, hebu na aje kwa Yesu, na Mungu naye atamuumba kuwa kiumbe wa roho. Sasa, tunamjua adui wetu aitwaye mwili, na tunaelewa vile huu mwili ni wakutujaribu ili tuthibitike kuwa wenye mapenzi kama yale ya Mungu. Basi, natumthibitishie Mungu kuwa tumeamua kuishi maisha yake. Hii tutafanya kwa kuamua kupigana na mwili( kwa maelezo Zaidi, tusome ujumbe uitwao, Siri ya kushinda). Basi je, wewe ni mmoja wa wasafiri wa kuuendea ufalme wa Mbinguni?. Kama ndio, usulubishe mwili na tamaa zake– Wagal.5:24.Mtazame Yesu, na ufuate nyayo zake, huku pia ukikaa ndani yake. Na kwa vile Imani ni kujua na kuwa na uhakika unajua, basi tujitahidi na kuhakikisha tuko ndani yake kila wakati. Tutawezaji kujua? “ na tunajua tunamjua, na kuwa ndani yake ikiwa tunazishika amri zake- 1Yohana,2:5-6; 3:24”. Mwenye masikio na asikie vile roho analiambia kanisa. Neema ya Bwana Yesu na upendo wake viongezeke kwa wingi mioyoni mwa wote wa hili zizi.
Hii sauti inawajia kuto kwa muumba wenu, kwa Yesu Kristo kupitia kwa watumishi wake,
KANISA LA MWISHO LA MUNGU. Pata anwani za mawasiliano kwa Website yetu, www.endtimecog.org, au upige nambari hizi; +254-795-034-978/ +255-753-359-179.
God is good