Mungu ni jamii ambayo wanadamu wote ni washirika watazamiwa( kwa maelezo zaidi, soma ujumbe wetu, “ Jamii la Mungu….”). Lakini, ili mtu aweze kuwa mwenyeji kamili, ni lazima azaliwe na Mungu mwenyewe. Kama ni hivyo , basi ni muhimu tuelewe ni kwa jinsi gani mtu anaweza kuzaliwa katika hiyo Jamii. Tunasikia wengi wa wale wasemao ni Wakristo wakisema kwamba wamezaliwa mara ya pili, na kwamba wameokoka. Kulingana nao, mtu uzaliwa mara ya pili hapo anapomkubali,na kumwamini Yesu, na kupokea roho takatifu ndani ya moyo wake. Kwa vile tunajua kwamba biblia ndio ile neno ambayo Mungu utumia kujithihirisha yeye na maisha kwa ujumla kwa mwanadamu, je basi, tunaweza kuthibitisha hiyo imani tukitumia biblia, ya kuwa mtu amezaliwa mara ya pili punde tu anapopokea roho takatifu, na hapo huwa ameokoka pia? Je, ni mwalimu wetu Yesu aliyeyafundisha hayo? Ni nini hasa kunachochangia mtu kuzaliwa mara ya pili na hivyo kuokoka kulingana na mafundisho ya Bwana wetu Yesu, ambayo ndiyo maandiko ya Biblia? Mungu ni roho, pia maisha yake ni ya kiroho. Hii inamaanisha kuwa, hawezi kueleweka kupitia kwa hizi akili zetu za kimwili, maana anasema, “ Wale walio katika akili za kimwili hawawezi kuyaelewa mambo ya kiroho, maana hayo ueleweka tu kwa jinsi ya roho- 1 Wakori.2:14”. Mungu anaelewa hivyo. Hii ndio sababu alifanya mpango wakutuwezesha kuyaelewa ya kiroho wakati huu wa mwili, maana, anasema, “ Tangu kuumbwa kwa ulimwengu, mambo ya Mungu yasiyoweza kuonekana, yaani, uungu na utauwa, yamonyeshwa kupitia kwa vitu alivyoviumba-Warumi.1:20”. Kama ni hivyo basi, ni uumbaji gani ambao unaonyesha na kueleza vile Jamii ya Mungu ilivyo, na jinsi mtu anaweza kuzaliwa katika hiyo Jamii? Baada ya kuwaumba Adamu na Awa, Mungu aliwaamrisha na kuwaambia, “……Zaaneni mkaijaze Dunia-Mwa.1:28”. Wakati Yesu alikuwa Duniani katika haya maisha ya kimwili, alitujulisha Mungu kama, “….Baba wetu wa Mbinguni-Mat.6:9”. Hii inakubaliana nay ale Mungu alikuwa amemwambia Isaya akisema, “……nami nitakuwa baba kwao, nao watakuwa wana kwangu, wa kiume na kike, asema Bwana-2 Wakor.6:18; Hosea.1:10;isaya.43:6”. Kristo pia alikataza mtu awayeyote asiitwe baba hapa Duniani, ila Mungu peke yake, na ilhali, amepanga kwamba wanaume waitwe baba-Mat.23:9; Kutoka.20:12. Ni kitu gani anatufundisha hapa? Ni wazi kabisa,ikiwa kweli tumepewa kuelewa. Mungu alianzisha Jamii ya kimwili ili kupitia kwa hiyo, aweze kutufundisha kuhusu jamii yake ya kiroho ambayo watu wote watakaofaulu kuumbika uungu watakuja kuzaliwa ndani yake na kujiunga nayo, wakiwa miungu kama yeye- Yohana.10:34. Kwa hivyo, ikiwa tutaelewa kuzaliwa kwa kiroho, inatupasa kufuatilia hatua za kuzaliwa huku kwa kimwili.
KUZALIWA MARA YA KWANZA
Mungu anao mpango ambao ataufuatilia kumfanya mwanadamu kuwa kiumbe wa kiroho mwishowe. Huu mpango unaanza na haya maisha tulionayo ya kimwili, maana anasema, “…..maana uanza na huu wa mwili, baadaye uja huu wa kiroho-1 Wakor.15:46”. Katika huu mwili, Mungu aliwaumba Adamu na Awa wakiwa na uwezo wa kuzaa watoto, ili kwa njia hiyo waweze kujaza watu katika Dunia, maana Mungu anataka wana wengi katika jamii yake y utukufu. Basi tunauliza; Je kuzaa kunachukua kunafanyika haji katika huu mwili? Mwanaume umjua mwanamke kwa njia ya gono. Hivyo, yae la uzazi la mume uingia ndani ya tumbo la mke, na kushikana na yae la uzazi la mke ndani ya tumbo lake. Mara tu hayo mayae yanaposhikana, mwanadamu uanza kuumbika na uhai unaanza hapo. Baada ya hapo muda wa miezi tisa upita, ukiwa ni wakati wa huyu mototo aliye tumboni kuumbika viungo ili akikamilika aziliwe ulimwenguni, akiwa kiumbe wa kimwili vili baba yake wa kimwili alivyo. Hivi ndivyo mtu uzaliwa mara ya kwanza. Hapo tu mimba inapochukuliwa wakati wa haya mayae kushikana ndani ya tumbo la mke, tunasema mototo amechukuliwa mimba, lakini hajazaliwa bado. Itachukuwa ule wakati wa miezi tisa, ambao Mungu aliweka katika mpango wake wa kuzaana kwa wanadamu. Ni wakati wa mototo kuumbika viungo na kukamilika kuwa mwanadamu, ili azaliwe akiwa mwanadamu kamili. Tunakubaliana kwamba, sio wote wachukuliwao mimba ambao mwishowe uzaliwa. Kwa sababu za itilafu za, labda magonjwa ya mama, au kuumia, watoto wengine uumia ndani ya tumbo na hiyo usababisha mimba kutoka kabla ya wakati wake, hivyo kukatiza huo mpango. Huu wakati wa mimba ni mfupi. Ni miezi tisa tu ambapo mototo aliye ndani ya mimba anafaa kuumbika, au kwa sababu ya hizo itilafu, mimba inaweza kutoka na hasizaliwe kabisa. Kila kitu Mungu afanyacho kina hatua mbili. Katika huu mpango wa kuzaliwa, hatua ya kwanza ni kuchukuliwa mimba na kuumbika ndani ya mimba, na baada ya hapo, hatua ya pili uja ambayo ni kutoka nje ya mimba, hivyo kukamilisha mpango wa kuzaliwa wenyewe. Tukisema mtoto amezaliwa akiwa angali ndani ya tumbo, tutakuwa tunadanganya maana ni lazima mtoto atoke ndani ya tumbo ndio awe amezaliwa, na atakuwa mwanadamu wa kimwili kama baba yake aliye mzaa alivyo, maana, “kilichozaliwa na mwili ni mwili…Yohana.3:6”. Basi, Mungu anatuambia; kwa namna yiyo hiyo “……tuliouchukua umbo wa kimwili, na vivyo hivyo, tutauchukuwa umbo wa kiroho- 1 Wakor.15:49”. Ikiwa basi huu mpango wa kuzaliwa kimwili ni onyesho la kuonekana la jinsi kulivyo kuzaliwa kiroho, basi je, tumezaliwa mara ya pili hapo tunapopokea roho takatifu?
KUZALIWA MARA YA PILI
Kuumbwa kwa mwanadamu kulipangwa kuwe na hatua tatu kabla hakujakamilika. Hatua ya kwanza ni hii ya kimwili ambayo tumeleza hapa juu. Hatua ya pili na ambayo ndiyo mwanzo wa kuzaliwa mara ya pili inaanza na kupokea roho takatifu hapo mtu anapoamua mwenyewe kuishi kama Mungu. Hii roho umfanya mtu apate ufahamu wa Mungu unaotuwezesha kuyaelewa maisha yake, na hivyo kuanza kuyaishi. Ni kwa njia hii ambapo, Mungu uanza kuumba tabia yake ndani yetu. Ni hapa ambapo, mpango wa hatua ya kuzaliwa mara ya pili uanza. Huku kupokea roho takatifu kunafananishwa na yae la mume likiungana na yae la mke ndani la tumbo la mke. Na kama vile uhai wa mtu uanza punde tu haya mayae yanaposhikana, huku huyo mtu akiwa ni mtoto wa wazazi wake ijapokuwa bado hazaliwa, na vivyo hivyo, katika huu mpango wa kuzaliwa mara ya pili. Hapo mtu anapopokea roho takatifu, yeye uanza kumwuita Mungu baba, maana imeandikwa, “ Na kwa kuwa mmekuwa wana, Mungu ametuma roho ya mwanae katika mioyo yetu, aliaye, ‘Abba-Baba-Waga.4:6”. “ Maana wote waongozwao na roho ya Mungu ni watoto wake- Warum.8:14”. Baada ya kupokea hii roho, Mungu anasema kwamba, “….wewe ni mwanangu; leo hii nimekuchukua mimba-Zab.2:7”. Kama kweli tuna haja ya kuelewa, neno “kudunga mimba” ina maana ya mwanzo wa mpango wa uzazi na ufanyika ndani ya mimba na sio nje. Tuseme nini basi? Mtu anapopokea roho takatifu, uhai wa kiroho uanza ndani yake, na mpango wa kuzaliwa mara ya pili uanzia hapo. Huyo mtu hajazaliwa bado, lakini ni motto wa Mungu aliye ndani ya mimba ya kiroho, maana, Bwana wetu anatuambia, “……sasa tu wana wa Mungu, lakini haijabainika vile tutakavyokuwa, ila, tunaelewa kwamba, atakapokuja, tutakuwa kama yeye, maana tutamwona alivyo-1 Yohana.3:2”. Kwa nini hatujui tutakavyokuwa kwa sasa? Maana bado tuko ndani ya tumbo. Hatuwezi kuona kunachoendelea kuumbika pale, kwamba ni kike au kiume. Lakini kwa vile Kristo alikuja na akazipitia hatua za huu mpango hata akaufikia ukamilivu, basi tunajua tutakuwa kile alifanyika baada ya kukamilika. Basi,ukweli ukishaa fanywa wazi hivyo, ni kwa nini watu wanachanganyikiwa wasitofautisha katika ya kuchukuliwa mimba na kuzaliwa? Hakuwezi kuwa na sababu nyingine isipokuwa kwamba, “……mungu wa Dunia hii akili zao,wasielewe, na kuuona huu mwangaza wa ijnili tukufu la Kristo Yesu-2 Wakor4:4”. Kristo anaongea kwa lugha ilyo wazi kabisa akisema, “…usipozaliwa mara ya pili, uwezi kuuona wala kuuingia ufalme wa Mungu-Yohana.3:3; 1 Wakor.15: 50”. Hapo, Kristo anaelewa kuhusu kuzaliwa mara ya kwanza ambao tumeelezwa juu yake vizuri sana, ambao ni kwa kimwili, kutokana na baba wa kimwili. Sasa, anaongelelea kuhusu kuzaliwa kwa mara ya pili, ili itimie iliyosemwa kwamba, “Na kama vile tulivyouchukua umbo wa kimwili(kupitia ule mpango wa uzazi tumeona), na vivyo hivyo, tutauchukua umbo wa kiroho(kupitia kwa huu mpango tunaoendelea kuelezwa hapa)- 1 Wakor.15:49”. Tunaona akiendelea kufafanua zaidi alichomaanisha kuhusu kuzaliwa kwa pili, eee, akionyesha wazi yale maumbile mtu atakuwa akizaliwa hii mara ya pili, maana anasema, “……….kile kimezaliwa na roho ni roho….”. Na ili haakikishe tumemwelewa vizuri, anatoa mfano akisema, “upepo uvuma upendavyo na sauti yake twaisikia, lakini hatuuoni, hatujui utokako wala uendako. Hivi ndivyo alivyo mtu aliyezaliwa na roho- Yohana.3:6-7”. Kama vile hatuwezi kuuona upepo, na vivyo hivyo, Mwalimu wetu anasema kuwa, hatuwezi kuuona ufalme a Mungu, wala kuwaona wale ambao wamezaliwa mara ya pili maana ni kama upepo. Je wajua ya kwamba, tumesingirwa na mabilioni ya malaika? Lakini hatuwezi kuwaona kwa haya macho ya kimwili, kama vile hatuwezi kuuona upepo.
MIMBA YA KIROHO
Wandugu wapenzi, kila mtu ambaye amepokea roho takatifu ameingi kwenye hatua ya pili ya uumbaji wa mwanadamu, ambayo ni ya kiroho na inahusiana na kuumbika akili na tabia za Mungu. Hata hivyo, watu hawa bado ni mwili na damu, ila hawaishi tena kwa kufuata akili ya kimwili, maana, “ Ijapokuwa tunaishi katika mwili, hatuenendi kimwili….2 Wakor.10:3”. Yeyote ambaye amepokea roho ya Mungu, “…ameingizwa ndani ya Kristo(neno) pia…… hivyo, ameanza kuenenda katika upya wa maisha- Warum.6:3-4”. Kristo ndiye “….kanisa ambalo ni mwili wake-Waef.1:22-23”. Sasa, kwa lugha la mavumbo, hili kanisa ambalo ni Kristo ndiyo mama yetu ambaye tuko ndani ya tumbo lake, maana, “…Yerusalemu wa juu ako huru, na ndiye mama yetu-Wagal.4:26”. Hili kanisa, ambalo ni Kristo ndio neno la Mungu ambalo tuliwekwa ndani yake(yaani tunaishi hayo maisha ya neno).(ujumbe wetu uitwao, “Msingi wa milele una maelezo zaidi. Uangalie katika Web yetu, www.endtimecog.org). Kwa hivyo, maisha ya ukristo, ambayo ni hatua ya pili ya uumbaji wa mwanadamu, ambao unahusu kuumbika akili na tabia za Mungu, utawezekana tu, ikiwa tutabaki kukaa ndani ya Kristo(ndani ya maandiko yakiwa ndiyo maisha yetu),maana ndio ile mimba inatulea, maana nje ya hapo, “….hatuwezi chochote(mimba itatoka)-Yohana.15:5”; Tena, “….tunashiriki katika Kristo ikiwa tunabaki ndani yake mpaka mwisho-Waeb.3:14”. Eleweni kama mnaweza tafadhalini. Kwa namna lile ile ambayo motto aliye ndani ya mimba hawezi kutoka akatembea nje baadaye akarudi, kwa nmna lile ile ambayo huyo motto hawezi kujipa chakula, mpaka apate kilicho tayari kutoka kwa mama kupitia kwa kitovu, na vivyo hivyo, walio ndani ya mimba la kiroho. Tunafananishwa na tawi ambalo nilazima lishikilie kwenye shina, la sivyo, litakauka(nyauka)-Yohana.15:3-5. Katika haya maisha ya ambapo tuko ndani ya tumbo, hatuna uhai wetu sisi wenyewe. Tunapokea kila wakati kutoka kwa Yesu kupitia kwa roho takatifu ambalo ndio mfano wa kitovu. Hii ndiyo ile hatua iliyo na hatari nyingi zaidi katika uumbaji wa mwanadamu. Kama vile mtoto aliye ndani ya tumbo hana uhakika wa kuzaliwa, vile ana hatari ya mimba kutoka au mama mwenyewe kufa kabla ya kuzaliwa, na ndivyo alivyo yeye aliye ndani ya roho. Kwa sababu hii, mtu yeyote aliye ndani ya roho, na ambaye anatuambia ameokoka, ni sawa na kutuambia kwamba huyu motto aliye ndani ya mimba ana uhakika wa kuzaliwa ulimwenguni. Je, huyu mtu anaongea ukweli? Tuko katika vita vya kiroho(hatari ziwezazo kufanya mimba itoke), “……tukipigana na gome za giza, mamlaka na pepo waovu katika ulimwengu war oho-Waef.6:12”. Tukiongea kwa namna ya kimwili, katika vita, kunaouwezekano wa kupigwa risasi na kufa. Utawezaji kusema umeokoka ilhali ungali vitani? Ni uongo wa hali ya juu kwa yeyote Yule, wakati huu wa kuchukuliwa mimba anadai kuwa amezaliwa au kuokoka, maana tunaona watu ambao wamechukuliwa hii mimba ya kiroho(kupokea roho takatifu), “….. wakaonja kipawa cha mbinguni, wakawa washiiki war oho takatifu na kuonja uzuri wa neno(maisha) la Mungu, Na nguvu za ulimwengu ujao; wakitenda dhambi ya kukufuru, haiwezekani kwao tena kutubu-Waebr.6:4-6”. Ndugu zanguni, hawa ni watu ambao wamechukuliwa mimba ya kiroho; ile hatua ya kuumbika kiroho ikaanza ndani yao; lakini sasa wako hapa, hawajazaliwa. Kwa nini? Tukiongea lugha ya kimwili ni kwamba, hii mimba yao imetoka kabla hawajakomaa tayari kuzaliwa. Sasa, kama walikuwa wanadai kuzaliwa, wanadai kuokoka, ni nini imefanyika tena? Jihadharini na manabii wa uongo. Maana sis zote ambao tumechukuliwa hii mimba ya kroho( tunaoishi maisha ya kikristo), tunayo hii hatari ya kukosa kuzaliwa; eee ya hii mimba kutoka. Hii ndio sababu sasa hivi, hatujazaliwa mara ya pili, na wala hatujaokoka, maana katika hii vita ya kiroho, tusipokuwa waangalifu, kunayo hatari ya kukufuru roho ya Mungu, dhambi ambayo haiwezi sameheka. Mwalimu wetu, hali akiyaelewa hayo anatusihi, “…..tuangalie mtu yeyote asikose kuipata neema ya Mungu, kusijetokea roho ya uchungu ikaleta shida,…….Waebr.12:15-17”. “Mpige vita vizuri vya imani(ng’ang’anieni kuumbika tabia za Mungu)——1 Timotheo.6:12”. “maana yeye ambaye kwa uvumilivu, huku akiendelea kutenda wema, anatafuta heshima, utukufu na kutokuharibika, Mungu atampa uzima wa milele-Warumi.2:7”(soma ujumbe uitwao, “Tafuteni Heshima”, na, “Je, wewe ni Mkristo?” Utazipata katika web yetu,www.endtimecog.org). Hii ndiyo hatua ya kwanza ya mpango wa kuzaliwa mara ya pili, ikiwa pia ni mwanzo wa hatua ya pili ya uumbaji wa mwanadamu ambayo ni ya kiroho. Eee, huu ndio mfano wa ule wakati wa miezi tisa ambao motto uchukuliwa mimba, na ndio sababu mwalimu wetu anatuambia, “….kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu Yesu- 2 Petro.3:18”; “ Vaeni utu upya unoumbwa kwa sura ya Mungu katika utakatifu na uhaki wa kweli-Waef.4:24”. Kama vile tumeona, ni wakati unahitaji uangalifu maana umejawa na hatari za kutoa mimba kabla ya kukomaa kiasi cha kuzaliwa. Tutaponaji basi? (ujumbe wetu uitwao, “siri ya kushinda” unao maelezo).
MFANO WETU
Kwa wale ambao watafaulu kuumbika hii akili na tabia ya Mungu, Mungu atawapeleka kwenye hatua ya tatu ambayo ndiyo ya mwisho ya kumuumba mwanadamu. Ipi? “Atakayevumilia mpaka mwisho ataokoka-Mat.24:13”. Atakayeendelea mpaka huu mwisho, atazaliwa mara ya pili kwa kupewa mwili wa kiroho, na hapo ndipo ataokoka. Tumekuwa na manabii ambao waliishi mwaka mingi kabla Kristo hajaj ulimwenguni, na mabao waliishi katika roho wakikutazamia huku kuzaliwa mara ya pili. Je, walikupata hapo kwenye mwisho wa maisha yao? Hebu sikia lile jibu Mwalimu wetu anatupa tafadhali; “Hawa wote walikufa kabla hawajaipokea hiyo ahadi, ila waliiona kwa mbali…..Waebr.11:13”. Ni ahadi gani hii walioitazamia, ambayo walikufa kabla hawajaifikia? “Na hiki ndicho alichotuahidi; uzima wa milele-1 yohana.2:25”. Hapa, ni dhahiri kwamba walikufa kabla hawajauingia ule ufalme wala kufanyika viumbe wa kiroho maana walikuwa bado hawajazaliwa mara ya pili. Katika maisha yote ya imani yao, waliishi tu kama watu walio ndani ya mimba-watoto wa Mungu ambao hawajazaliwa bado. Hii ndio sababu Yesu alipokuja Duniani muda mrefu baada ya hawa manabii, aliishi na kuufikia ukamilivu na akaitwa mzaliwa wa kwanza. Ikiwa kwa kweli, kpokea roho takatifu ndio kuzaliwa mara ya pili, basi Kristo hangekuwa mzaliwa wa kwanza. Manabii wangekuwa, maana walikuwa mbele yake. Basi je, ni mfano gani tulionao wa kile kinaachilia mtu kuzaliwa mara ya pili, hatua ambayo inamfanya mtu kuwa ameokoka kutoka kwa adui wetu mkubwa, ambaye ni kifo? Hakuwezi kuwa na mfano mwingine ule isipokuwa Yesu mwenyewe, maana anatuambia, “ …..Nimewaachia kielelzo ili mfuate nyayo zangu- Yohana.13:15”. Anazidi kuthibitisha hayo kwa kinywa cha Paulo akisema, “…Kristo ndiye mtangulizi na mkamilishaji wa imani yetu-Waer.122”. Kwa hivyo, ili tuzaliwe mara ya pili na hivyo, tuweze kuoka, ni lazima tupitie hatua zote zile Yesu alipitia. Kristo alichukuliwa mimba kwa nguvu za Mungu mwenyewe(roho takatifu), ndani ya tumbo la Mamake Mariamu- Luka.2:35. Alikaa miezi tisa ndani ya tumbo kawaida ya kila mtu. Baada ya hapo, alizaliwa katika haya maisha ya kimwili kama ilivyo kawaida ya kila binadamu. Alipozaliwa katika huu mwili, hakuitwa mzaliwa wa kwanza wa Mungu, mbali, ……..aliyechukuliwa mimba(Kiswahili hakina neno la kueleza ile neno la kiingereza ambalo ina maana ya kuchukuliwa mimba-yaani “begotten(not born)-Waeb.1:5”. Kama vile tuliona kwamba, sisi tuliumbwa tukiwa na uhuru wa kuchagua yale maisha tupendao kabla hatua ya pili haijaanza, ambayo uanza kwa kupokea roho takatifu, Kristo alichagua maisha ya Mungu na akapokea roho takatifu- Mat.3:17. Kwa hivyo, Mungu alianza hatua ya pili ya kumuumba, “na Yesu akakua katika hekima,kwa umbo, huku akipata kibali mbele za Mungu na mbele za wanadamu-Luka.2:52”. Alipigana na shetani, vile vita vya imani-Waef.6:12;Mat.4:4,7,9. Alijaribiwa kwa kila namna vile tunavyojribiwa sasa, lakini aliusimamia ukweli, huku akikataa kila ushauri wa Shetani-Waeb.4:15, maana, “ Ijapokuwa alikuwa mwana, alijifunza utiivu kupitia kwa yale matezo aliyoyapata, huku akimtegemea Mungu kikamilivu kwa wokovu-Waebr.5:7-8”. Baada ya kung’ang’ana mpaka mwisho, hapowalipomsulubisha, alikamilika katika akili na tabia za Mungu-Waeb.5:9. Walipomuua, baada ya siku tatu, alifufuka akiwa na mwili wa kiroho na hapo Mungu alikamilisha uumbaji wake kwa kumpa huo mwili wa kiroho. Ni wakati huu baada ya kufufuka akiwa na huu mwili usioharibika wa kiroho, ambapo Yesu alizaliwa mara ya pili, na kufanyika kuwa mzaliwa wa kwanza, maana anatuambia, “…alifanywa kuwa mwana wa Mungu kwa uwezo, kulingana roho wa utakatifu, hapo alipofufuka kutoka kwa wafu-Warum.1:4”. Je, ni nani mwingine ambaye amewahi kuzipitia hatua zote za uumbaji kama Kristo, ata kufikia kunyanyika kiumbe wa kiroho? Ndiyo, nani mwingine ambaye amewahi kuzaliwa akawa roho kama yeye, na kutimiza neno alilolisema kuwa, “kilicho zaliwa na roho ni roho-Yohana.3:6”? Hakuna awaye mwingine Yule; sio manabii, na wala sio mitume; yeye peke yake. Baada ya Mungu kumkamilisha, Kristo anaishi leo akiwa kiumbe war oho kama vile baba aliyemzaa ni roho, na ndiye wa kwanza kuzaliwa hivyo, huku tukitazamia wengine wengi wazaliwe baadaye, ikitegemea kama watafaulu hivi vita na kushinda-Ufu.3:21. Pia, ni yeye peke yake ambaye ameokoka maana, hali akiwa kiumbe wa kiroho, “….mauti hayana nguvu kwake tena, wala hawezi tena kujaribiwa na dhambi- 1 Wakor.15:55”. Kama vile tumeona, ijapokuwa manabii na mitume waliitimu, hawakukamilishwa kama Yesu, maana, “…….wote walikufa kabla ya kuifikia hiyo ahadi-Waeb.11:13”. Kama ni hivyo basi, ni lini basi tutazaliwa mara ya pili na kuifikia ahadi hiyo, huku tukipewa miili ya kiroho, wakati pia mabapo mauti hayatkuwa na nguvu juu yetu, yaani-wakati tutakuwa tumeokoka? Ni wakati, “…..huu mwili wa kuharibika utavaa kutokuharibika, wakati huu wa kufa utavaa kutokufa, wakati( Yesu) itatimia neno, ‘….mauti yamemezwa na uzima- 1 Wakori.15:54”. Hii itakuwa lini basi? “ wakati wa tarumbeta ya mwisho; maana tarumbeta italia, na wafu watafufuliwa wasiwe na kuharibika, nasi tuylio hai tutabadilishwa(tupewe miili ya kiroho kama Yesu)- 1 Wakor.15:52”. Ndio, ni wakati wa mwisho, hapo huyu Yesu tunayemngojea atakapokuja, “…..na kuibadilisha miili yetu ya unyonge ifanane na ule wake wa utukufu-Wafilip.3:21”. Kunao kitu kilicho wazi kushinda hiki? Hatuwezi kuwa tumezaliwa mara ya pili mpaka wakati ule tutakuwa tumefanywa kuwa viumbe wa kiroho. Hatuwezi kuwa tumeokoka mpaka wakati huo, baada ya kufanywa viumbe wa kiroho, wakati ambao, mauti hayatakuwa na uwezo juu yetu, ambao pia, ndio wakati tutakuwa na uzima wa milele(kutokufa) ndani yetu. Wewe unayedai kuwa umeokoka, au umezaliwa mara ya pili, bado unataka kuendelea na huo uongo ata baada ya maelezo yaliyo wazi namna hii? Eee, baada ya kumsikiliza mwalimu wako Yesu Kristo, ambaye peke yake ndiye ajuaye, na ndiye peke yake awezaye kukuokoa, bado unataka kufunga macho na kuendelea na giza? Mwenye masikio na asikie vile roho analimbia kanisa. Huyu ni mwokozi wako Yesu Kristo akiongea kupitia kwa kanisa lake, THE ENDTIME CHURCH OF GO,