Ni kitu gani tunachokishuhudia katika ulimwengu wa leo? Eeeh, tunaona nini katika jukwaa la kimataifa? ……uovu ambao ni kama mahali palipobomoka, palipo tayari kuanguka kama ukuta mrefu, ambao kuvunjika kwake uja ghafula mara moja. Naye atapavunja kama chombo cha mfinyanzi kivunjwavyo, akikivunjavunja asiache kukivunja, hata kusipatikane katika vipande vyake kigae kitoshasho kutwaa moto jikoni, au kutega maji kisimani- Isa.30:13-14. Haya yanakubaliana kabisa na matukio mengine ambayo yataufanya huu mfumo………. kuvunjwavunjwa vipande vipande, hata viwe kama makapi ya viwanja vya kupepeta wakati wa hari; na upepo utavipeperusha hata pasionekane mahali pake;-Dan.2:35. Ni nani kati yetu ambaye amejaliwa kuuona huu uharibifu unavyoanza sasa hivi?
Jusi, Mtangazi mmoja wa Saudi Arabia, Bwana Khashogi aliingia kwenye ubalozi wa Saudia huko Uturuki na akapotelea humo ndani. Rekodi za video zilionyesha nyakati zake za mwisho kuonekana akiingia, ambapo baadaye iligunduliwa kwamba aliuliwa humo ndani kwa maagizo ya Serikali ya Saudia. Punde tu baada ya hayo matukio, viongozi wa mataifa mbali mbali walianza kutaka kuelewa alivyopotea huyo mwana habari. Wengine kama Marekani na Uturuki walijisema kuwa na ufahamu wa vile alivyopotea na kuuwawa ndani ya ubalozi huo. Hawa viongozi wote walionyesha kusimamia na kutetea haki na ukweli wakitaka Saudia ielezee hali ilivyo. Kwa upande mwingine, Serikali ya Saudia nayo ilianza kutafuta kila aina ya ujanja na uongo wa kujitetea huku wakijaribu kujiondolea lawama mbele ya hawa viongozi wenzake, hivyo, kukana kwamba walimuua Khashogi. Naomba tushangae kidogo hapa. Ijapokuwa Marekani na Uturuki walisema kwamba wanao ushahidi thabiti kwamba Serikali ya Saudia ilimuuwa huyu mwanahabari, Hawakuonekana kuusimamia huo ukweli na uhaki wanaojionyesha kuutetea. Baada ya kutishia kuadhibu Saudia kwa hicho kitendo cha unyama, Saudia nayo iliwatishia kuhujumu biashara zao zilizoko kwenye nchi yake.Baada ya Marekani na Uturuki Kuyasikia hayo matishio ya Saudia, waligeuka mara moja; wakawacha kutetea uhaki na ukweli, na badala yake, wakaanza kutetea mali na kazi zao zilizoko Saudi. Badala ya ule uthabiti waliojisema kuwa nao kuhusu kitendo cha Saudia, waligeuza msemo na kuanza kuongea mambo ya kufanya uchunguzi; eee, wakakana walichokifahamu kwa ajili ya mali. Kwa nini? Walichagua kuokoa mali zao na uhusiano wao na Saudia, badala ya kutetea uhaki na ukweli, wakatimiza alichokisema Mungu kuhusu kizazi cha leo, kuwa, miguu yao ukimbilia mabaya, nao ufanya haraka kumwaga damu isiyo na hatia; mawazo yao ni ya uovu, ukiwa na uharibifu zaonekana katika njia zao. Hukumu imeanguka na kusukumwa nyuma, na haki inasimama mbali sana; maana kweli nayo imeanguka katika njia kuu( yaani hakuna anayeitumia); na unyofu hauwezi kuingia-Isa.59:7,14. Je unafuatilia anayoyasema Mungu hapa? Kwa kupendelea mali zao, na uhusiano wao wa kibinadamu katika haya maisha ya udanganyifu, wanaukataa ule msingi wa pekee, ambao juu yake, uhai na maisha yote vimejengwa. Hii ndio sababu, ni lazima huu mvumo ubomoke na kuanguka kwa kishindo kikubwa.
KUJIFANYA MIUNGU
Haya yote yanatendeka kwasababu, mwanadamu hakujiumba, na hivyo, hawezi kujipangia vile ataishi. Baada ya kuukubali ule uongo wa Edeni, kwamba yeye ni kama Mungu-Mwa.3:4-5, Kila mmoja anajaribu kuthibitisha huo uongo kuwa ni ukweli kwa njia ya, kujaribu kumchusha mwanadamu mwezake kwa kumvinyilia, kumtawala, kumkalia na kumthibiti. Na kila mmoja pia anajaribu kujionyesha mbele ya mwenzake kuwa mwenye haki, kwamba kila anachopanga na kufanya ni cha kweli (kama Mungu). Mwanahabari Khashogi aliuliwa katika jitihada za Saudia kuficha maovu yao, ili kujihesabia haki mbele ya wanadamu wenzake. Hili lilitokana na Khashogi kutoa siri ya vile Serikali ya Saudia inavyokeuka haki, na kwa huko kukeuka haki, vile wanavyounganisha majeshi huko Yemeni na kuuwa raia wasio na hatia, bila kusahau vile inawadhulumu na kuwaua raia wake huko nyumbani. Baaada ya Saudia kuona Khashogi anavyowaweka wazi mbele ya ulimwengu, katika bidii ya kuficha uovu wao ili waendelee kuonekana wenye haki, huku wakizidi kutenda uovu, walimnyamazisha kwa kumuua, wakatimiza anachokisema Mungu kuhusu hiki kizazi, kwamba, kweli imepunguka kabisa, na yeye auwachaye uovu(kama Khashoggi), ajifanya kuwa mateka( anayewindwa)-Isa.59:15. Kwa vile uovu hauwezi kuzaa wema, baada ya Saudia kujaribu kugandamiza ukweli na haki, matunda yake hayajakuwa haki, kuthibitisha kwamba kweli, huu ni mfumo wa uongo na uharibifu. Kufikia wakati huu tunapoandika huu ujumbe, Saudia imepoteza mabilioni ya madola kwa njia ya biashara zake kuzuziwa na mataifa mengine, na pia inatishiwa vikwazo Zaidi, vikiwemo kutengwa. Kwa hivyo, wakidhania kupata haki kwa kutenda mabaya, walipata mabaya. Kwa hakika ule ufahamu (uongo) wanaoutumia walimwengu hauwezi kuwaongoza kwenye njia ya Amani wala kuifahamu-Isa.59:8. Kwa ujumla, huu mfumo umejengwa juu ya uongo, na mwanzilishi wake alikuwa, na mpaka sasa anayo kusudi la kuwaangamiza wanadamu wote. Angalia na kuona vile viongozi wa mataifa ya sasa wanaoutumia huu uongo kufanya. Kwasababu ni uongo, kila kiongozi anajifanya mbele ya viongozi wenzake, na watu anaowaongoza, kujionyesha kutaka ukweli na haki vidumu,ihali, anachokiendeleza ni kampeni za kupendekeza, na kuhalalisha mapenzi yake yakubalike na wengine, yote hii ikiwa ni kwa faida zake mwenyewe. Mfano: Kunayo kampeni inayoendeshwa na viongozi wote wa ulimwengu ya kila taifa kuharibu zana hatari za kinuklia. Lakini pale nyumbani, kila taifa inaendelea kufanya utafiti utakaowawezesha kutengeza silaha zenye nguzu Zaidi. Marekani na Urusi wamejikabidhi vilivyo, kuungana katika harakati za kuleta Amani huko Syria. Lakini tunachokiona ni kwamba, Urusi imeungana na majeshi ya Serikali ya Syria na wanawaua mamilioni ya raia walio kwenye maeneo ya waasi, huku wakijidai kuondoa waasi. Marekani nayo imeungana na waasi kupigana na majeshi ya Serikali, na kuwauwa pia mamilioni ya raia huku wakidai kuondoa utawala dhalimu wa Asadi( Raisi wa nchi hiyo). Niambie sasa tafadhali. Hawa wawili wanaojifanya kutafuta amani, si wako kwenye vita wao kwa wao wakijifanya kusaidia? Ni kwa nini wanajifanya kutafuta amani huku kila mmoja akitisha na kumpinga mwenzake? Maana Ufahamu wanaoutumia kupanga serikali zao na maisha kwa ujumla ni wa uongo, na wenye lengo la kuharibu, kama anavyothibitisha Mungu akisema, mashujaa wao wanalia nje,wajumbe wa amani wanalia kwa uchungu-Isa.33:7. Kwa nini? Kwa sababu, chochote kinachokubalianwa kati ya hawa viongozi ni kujifanya tu, huku kila mmoja akidanganya mwenzake, kumpumbaza, maana baada ya kukubaliana, maagano yanavunjwa, miji imedharauliwa, ushahidi umepuuzwa, hawawajali wanadamu tena, na kwa sababu hii, njia kuu zimekuwa ukiwa, mashujaa wa vita wamekoma. Nchi imelegea na kuomboleza-Isa.33:7-9. Ukiangalia kwa makini, utaona kwamba, hakuna hatua ata mmoja wanayopiga hawa viongozi ambayo inalenga kuleta Amani, mbali yote wafanyayo yanaleta vujo na vita Zaidi. Haya yote ni kwasababu, mwanzilishi wa huu mfumo analenga kuharibu, na mwanadamu ambaye hajagundua hilo siri ameukubali. Hii ndio sababu muumba wetu anasema, ulimwengu wote umedanganyika-Ufu.12:9. Ndani ya akili zao, hawa viongozi wa ulimwengu wa leo wanadhania kuwa, kwa kuutumia huu uongo, wanaweza kuufanya ulimwengu kuwa mahali pazuri, lakini matokeo yake ni kinyume ijapokuwa hawagundui kuwa ni matunda ya huo uongo, maana, wanatafuta nuru, na badala yake, wanapata giza; wanatafuta mwangaza, lakini wanapata giza kuu; hawana tofauti na vipofu-Isa.59:9-10. Je basi, hili sio jambo wazi kuwa sisi sio miungu, na kwamba hatuna ufahamu wowote kuhusu maisha? Hili sio thibitisho kwamba tunachokitumia kama ufahamu ni uongo, na ndio sababu matokeo yake yanaleta maovu Zaidi? Je, wewe ni mmoja wa wale wameugundua, au wanaendelea kuugundua huu uongo na mahali unakowaelekeza wanaoutumia kama ufahamu?
JITENGANISHE NAO
Mungu anayo mipango kwa wanadamu wote, mipango ya Amani wala si ya ubaya, kuwapa nyinyi tumaini katika siku zenu za usoni-Yerem.29:11. Lakini tukiangalia kwa sasa, kutoka kwa kiwango cha jamii hadi cha kimataifa, mpango unaoendelea, sio huo wa Mungu, maana matukio tunayoyashuhudia ni maovu na ya kuharibu. Kama tunakumbuka, Mungu alimuumba mtu awe kama yeye; na hivi sasa, anatufundisha kuishi hayo maisha yake, ambayo, kunyume na haya ya sasa, mtu akiyaishi kwa kutii amri zake, yanampatia, …wingi wa siku na miaka ya uzima na Amani; ndio, matokeo ya kuyaishi ni, maisha marefu kwa upande mmoja, na ule mwingine, utajiri, hekima na Amani-Mithali.3:3:2,16; Zab.119:165, na mwisho wake, kwa vile hiyo neno ambayo ndio maelezo ya hayo maisha inadumu milele-1 Petro.1:25, basi wale waitiio pia watadumu milele maana Mungu amewaahidi, uzima wa milele-1 Yohana.2:25. Je, wewe ni baadhi ya walioyaamini anayoyasema Mungu hapa katika Kristo? Kama ndio, inamaanisha kwamba, wewe umeugundua huu uongo ambao umeishi kwake mpaka sasa, na uko tayari kuuwacha, huku tukiwacha kabisa chochote kile ambacho tulijifunza kwa huo uongo, maana tumegundua kwamba, Mungu ako tayari kuung’oa kama vile aliahidi katika kile kifungu tulianza kusoma-Isa.30:13-14; Dan.2:35, ambao hapa anauita mti-Mat.15:13. Kama tunavyogundua, matokeo ya kutii uongo wa shetani yako kila mahali, uovu kila mahali mpaka, hata hao viongozi tunaowatazamia watuletee suluhisho wanahuzunika kwa hofu kuu, na katika hiyo hofu, wamebakia kubabaishana wao kwa wao huku kila mmoja akitisha kupiga mwenzake. Mungu anayaona hayo Shetani anayokusudia kuyafanya akiwatumia hawa viongozi,na ameahidi kutomwacha ayatimize, maana anasema, kwa sababu ya wale ambao wameamua kuishi maisha ya kweli, Mungu ataingilia na kuufupisha wakati wa huu uovu-Mat.24:22. Hapa ndipo Mungu ataanza kuung’oa ule mti( maisha), ambao hakuupanda na ataanza na kumng’oa, mwanzilishi wake, maana, atamtuma malaika wake na mshika shetani na kumfungia kuzimu-Ufu.20:2-3. Basi wandugu, eleweni na kujua kwamba, uungu ama ukristo ni kutoa kabisa huu utu uharibikao na wenye kudanganya-Waef.4:22. Bwana wetu anatuagiza kwamba, tutoke kati yake, tukajitenge nayo- 2 Wakor.6:17, maana wakati wa kuung’oa kabisa hata pasionekane tena mahali pake-Dan.2:35 umefika. Ndio, wamchao Mungu ambao ndio kanisa lake ni watu ambao wameisikia hii sauti ya, tokeni kati yake enyi watu wangu msije mkashiriki dhambi zake, nakuyashiriki mapigo yake-Ufu.18:4-5.
NJIA YA KUTOKA
Maisha ni kile Mungu anaelezea katika neno lake- Mith.4:22.Pia ni kwa yule mtu , ambaye amependa mwenyewe, na kwa hiari yake, akaamua kuyaishi( Tunao ujumbe usemao, “kusudi la mwili “, upatikanao katika website yetu, www.endtimecog.org, wenye maelezo ya ndani Zaidi). Kwa ajili ya huu uchaguzi, Mungu alituumba wenye miili yenye maumbile yale ya Shetani, na pia akamruhusu Shetani aendelee kuishi hapa Duniani ili autumie huu mwili, kujaribu kututoa katika maisha ya kweli. Mwanadamu katika huu mwili anao uwezo wa kuelewa mambo ya kimwili peke yake. Hapa ndipo ulimwengu wote na viongozi wake pamoja na wasomi wake walipo; yaani, kuelewa na kuishi kimwili peke yake-tamaa za mwili, tamaa za macho, na kiburi cha maisha-1Yohana.2:16( ujumbe uitwao, Mchakato wa uumbwaji wa mwanadamu”, unao maelezo Zaidi). Baada ya kukubali kuwa kama Mungu, ilhali, wao ni wanadamu wa kimwili, wenye uwezo wa kuelewa ya kimwili peke yake, yaani- wanadamu wenzao, mali, na utukufu unaotokana na hayo, mwanadamu amebakia kuishi katika lengo la kutafuta hivyo vitu na kumthibitishia mwanadamu mwenzake kwamba yeye ni mtu mkubwa( kama Mungu). Huu ndio mpango Shetani anaoutumia kujaribu kuwafanya wapigane mpaka wamalizane. Huu mpango wa Shetani ndio Mungu anaouelezea kama, Sheria nyingine, inayopinga sheria ya Mungu iliyo katika akili yangu-Warumi.7:23. Kwa vile huu mwili, kama vile tuliona ni, mwili wa mauti-warumi.7:24, basi,Yeyote atakaye kujitenga na kile Mungu atang’oa ni lazima aanze kwa kuukana, kujiepusha na tamaa zake ambazo upigana na roho-1 Petro.2:11. Hiki ndicho Kristo alimaanisha aliposema kwamba ukristo(uungu), uanzia kwa mtu kujikana mwenyewe-Mat.16:24. Ndiyo, ni lazima yeyote ambaye ameanza hii njia ya “kutoka kati yake”, awache kabisa kupokea amri kutoka kwa hiyo akili iliyo ndani yetu ipiganayo na akili ya sheria za Mungu.
GOLI MPYA
Je, tukiwacha kupokea amri na ushauri kutoka kwa hii akili ya kimwili, tutaanza kutumia akili gani? Eee, tutaamrishwa na nani? Kabla Mungu hajatuumba( katika huu mwili), aliumba vitu vyote ambavyo huu mwili unahitaji-Mwa.1:29-30. Kwa hivyo anasema, mimi uwapa wanadamu uhai na kila kitu walicho nacho-Matendo.17:25. Hii ina maana kuwa, tunayo mali, watu, sifa zitokazo kwa watu, nyathifa za uongozi, kukubalika na kuungwa mkono na watu- fikiria chochote kile cha kimwili na utaona kipo. Basi utagundua kwamba, kwa vile watu walidanganyika wakiwa kwenye hiki kiwango cha kuona, kuelewa na kutegemea kimwili peke yake, utaona kwamba, wao uchagua kushikilia vya kimwili ikiwa kushikilia uhaki na ukweli kutawanyima hicho. Wakati wowote ule ambapo, mali yao, uongozi, kukubalika au kuungwa mkono, vinahatarika mtu akisimama na ukweli na haki, karibu watu wote uchagua kuwacha ukweli na haki, na kutetea hivyo vya kimwili. Basi angalia vizuri na uelewe tafadhali. Tunazo nyathifa za uongozi ambazo zinatufanya tuwache haki na ukweli. Tunao watu wanaotuunga mkono na kutusifu, huku wakituheshimu na kutuogopa, na wanatufanya tuende nje ya ukweli ili kuwafurahisha waendelee kutuunga mkono. Lakini hatuna uzima wa milele, na hivi vitu vyote haviwezi kutusaidia kuupata, maana, ingawaji tunavyo, mali hazifaidii kitu wakati wa gadhabu-Mith.11:4. Wenye hekima, wajinga, matajiri na maskini, wote pamoja ufa na kuwaachia wengine mali zao. Ijapokuwa wao uitanisha mali kwa majina yao na kusifiwa na wanadamu wenzake, kaburi pekee ndiyo makao yao-Zab.49:10-11,17-18. Tuseme nini basi? Wandugu wapenzi, tuko katika haya maisha ya kimwili, na Mungu anaendelea kutupa uhai kila siku. Anatuwacha tuendelee kuishi kwa kusudi gani? Anaendelea kutujalia uhai ili tuendelee kutafuta hivi vitu ambavyo tayari viko hapa duniani? Asha ata kidogo. Tuko hapa ili, kwa subira, tuendelee kutafuta utukufu, heshima na kutokuharibika, maana, atakayevipata hivyo, Mungu atampa uzima wa milele-Warumi.2:7. Je, tufanye nini ili tuwe tunatafuta utukufu, heshima, na kutokuharibika? Eleweni kwamba, amri ya Mungu ni takatifu na tukufu- Warumi.7:14. Wale ambao wameamua kujikana na kuitii, hao ndio watavikwa kutokuharibika-1 Wakori.15:52-53. Tuliona pia urefu wa maisha na wingi wa miaka uja kwa kutii hizi amri-Mith.3:1-3. Na hii inakubaliana na kile yesu anashuhudia akisema, maana uhai wa mtu hautegemei wingi wa mali aliyonayo-Luka.12:15. Tunamaanisha nini? Hii goli mpya ambayo ni ya kuufikia uzima wa milele haiwezi kufikiwa kwa kupata utajiri, uongozi, elimu au kuungwa mkono na kusifiwa na watu; na wala, haiwezi kuzuiliwa na ukosefu wa hivyo vitu. Eee, haichangiwi kabisa kwa vyovyote vile na mapato ya kimwili. Hii upatikana kwa kitu rahisi kabisa. Gani? Ukitaka kuingia uzimani, zishike amri; kasema Kristo-Mat.19:17. Hivyo basi, tunapaswa kuelewa kwamba, hii goli mpya utegemea vitu mpya ambavyo sio vya kimwili mbali vya kiroho. Wafalme na watu wa huu mfumo hawawezi kuvielewa, maana wangevielewa, hawangemsulubisha Kristo. Lakini kama ilivyo, ni vitu ambavyo, ‘sikio halijawai kusikia, jicho halijawai kuona, wala akili kuelewa-1 Wakor.2:8-9. Mungu anataka mwanadamu aliye kiumbe wa roho kama yeye-Mwa.1:26. Katika haya maisha ya kimwili, anaendelea kuwaumba wale wanaoamua kufundishwa naye, ili wawe na ufahamu na tabia zake. Huu ufahamu na tabia zake ndivyo vinavyoelezewa na amri zake, maana hizi amri zake ndizo kweli-Zab.119:151; Yohana.17:17; ndizo haki-Zab.119:172; na ndizo uzima-Yohana.6:63.
ISHI NA KUTENDA KIROHO
Shetani alilielewa hili lengo la Mungu vizuri sana, na kuwadanganya wanadamu huku akiwatoa nje yake. Hii ndio sababu unaona wafalme na watu wote wa ulimwengu wanaipuusa na kupinga hukumu ya haki; haki imesimama mbali, na kweli imeanguka barabarani-Isa.59:8,14. Wanaomcha Mungu ni wale ambao wamefunuliwa macho na kugundua huu uongo na wameamua kuuwacha; hivyo basi, wamebadilisha tegemeo lao kutoka kwa mali, uongozi, sifa za kibinadamu, na kuanza kutegemea Mungu na neno lake. Hii ndio sababu, bidii yao kwa kila watendacho ni kuhakikisha wametumia ukweli na haki, maana kwa huo, wanao wingi wa siku mkono wao wa kuume, na utajiri na heshima mkono wao wa kushoto-Mith.3:16; hii inathibitisha anachokisema Kristo kuwa, tukiutafuta ufalme na uhaki, haimaanishi eti, tutavikosa hivi vya kimwili, maana, vitawafuata pia-Mat.6:33. Lakini utakuta kwamba, hawamtii Mungu ili kupata hivi vya kimwili, maana wameelewa vizuri sana kwamba, hivi vitu ni vya kutumika na huu mwili, nao huu mwili ni wakutumika kujifunza kuishi katika haki na kweli, na baada ya hapo, hivi viwili( yaani mwili na mal), Mungu ataviharibu-1 Wakor.6:13. Hivyo, wao uitumia miili yao kujizoesha kuishi amri za Mungu, na sio kwa ajili ya kushiba na kustarehe tu. Ina maana kwamba, kusudi la Mungu kutupa huu uhai wa kimwili sio kuudumisha, mbali ni kutupa nafasi ya kuumbika ule usiokufa, kuvaa kutokuharibika- 1 Wakor.15:53( tunao ujumbe uitwao, “kusudi la mwili”, wenye maelezo Zaidi). Ni huku kuelewa kusudi la huu mwili wa nyama, ambako kunamwacha mtu akijibidiisha kwa uangalifu mkuu kuenenda na kutenda kulingana na amri ya Mungu, yaani kujitahidi kuufikia uzima. Tuliona vile huu mwili uliumbwa wenye maumbile ya kupinga haki na kweli, na pia vile Shetani aliachwa hapa duniani ili kuutumia kujaribu, kukubali( Imani) kwetu kwa maisha ya Mungu( kwa kutuletea mawaitha yapingayo amri za Mungu), ili tunapomkataa, na kuendelea na utiivu kwa Mungu, tumthibitishia kwamba kweli tunataka uzima wa milele-Yakubu.1:2; 1Petro.4:12; waamuzi.2:22. Hii ndio kusudi la haya maisha ya kimwili, ambayo, karibu ulimwengu wote haulifahamu.
TUKO MAFUNZONI
Haya maisha tulio nayo sasa ni wakati tumepewa wa kujikabidhi mbele za Mungu ili aendelee kutuumba kiroho. Kwa hivyo, tuko Darazani la Kiroho ambayo mwalimu wetu ni Kristo, akiongea kupitia kwa neno lake ambalo ndilo hili tunalolisoma hapa sasa. Kumbuka, tunaye mpinzani wa yale tunayofundishwa na Kristo, yaani Shetani, ambaye, kwakutuletea mawazo pinzani, anatufanyia mtihani, kuthibitisha kukubali(Imani) kwetu kwa kile Kristo anatufundisha. Hii ndiyo sababu, kwa akili zetu, kunayo mawazo mara mbili ambayo yanawakilisha aina mbili ya maisha(sheria). Tunapojibidiisha kuishi kwa sheria ya Mungu(wazo la neno lake), tunaona sheria nyingine(wazo la Shetani, au mwili) ikipinga hilo la Mungu-Warumi.7:22-23. Kristo anatufundisha waziwazi kwamba, haya mawazo ni aina mbili za maisha ambazo mtu anapaswa kuchagua moja, yaani, sheria ya roho wa uzima(maisha ya Mungu), na sheria ya roho ya dhambi na mauti( maisha ya Shetani)-Warumi.8:2. Lakini Mungu anatushauri tuchague uzima-Kumbukumbu.30:15,19. Ukristo ni kuchagua na kuanza kuishi kwa hilo wazo la amri la Mungu huku ukilipinga lile lingine la Shetani linalounga mkono nia na tamaa za mwili. Kwa nini tufanye hivyo? Maana tumeelewa kwamba, tusipoishi kulingana na amri za Mungu, tutajiharibu hata kufikia kujiuwa, maana, tukiishi kwa kuufuata mwili, twatafuta kufa, mbali tukiishi kwa kufuata roho, twatafuta uzima-Warumi.8:13. Basi, hapa ni wazi kwamba, njia ya pekee ya kuufikia uzima ni kuishi kwa amri za Mungu.
JITENGANISHE NAO
Ulimwengu wa sasa umejengwa juu ya mwili, sheria ya dhambi na mauti-Warumi.8:2. Hii ndiyo sababu tunaona mipango yake yote ni ya fujo,kukosana, chuki, vita, kuvunjika kwa ndoa-eee, kila wanachofanya kinayo madhara makubwa. Mungu hapa anatuthibitishia kwamba, chochote kile ulimwengu utumiacho kama ufahamu ni uongo, ni hiyo sheria ya kifo-Ufu.12:9. Tegemeo zake zote hazina msaada wowote. Ni utajiri? Mali hazifaidii kitu siku ya gadhabu-Mith.11:4: Ni tegemeo la watu? Hakuna wokovu kwa binadamu; pumzi yake utoka, na saa yiyo hiyo, mipango yake yote uangamia-Zab.146:3-4; Hakuna awezaye kukomboa maisha yake, wala kumlipa Mungu fidhia ya uhai wake-Zab.49:7: Ni sifa na kupendekezwa na wanadamu? Kinachotukuka kwa wanadamu ni machukizo mbele za Mungu-Luka.16:15. Basi,kwa kuwa vitu hivi vyote watu ukimbizana navyo haviwezi kutupa uzima wa milele, na katika haya maisha ya Mungu, tunatafuta huo, inatupasa kwanza tujiepushe kabisa na kuvitegemea kama njia ya kuufikia, yaani, kudumisha maisha. Tutajiepushaji? Ni katika akili ambako kila namna ya kuishi uanzia. Ni papo hapo ambako yeyote yule apendaye uzima wa milele ataanzia kuujenga. Bwana wetu Kristo anatupatia namna ya kuanza. Sikia. Msijiwekee hazina duniani( kutegemea vya mwili), mahali nondo na kutu viharibipo; au wezi kuvunja na kuiba. Jiwekeeni hazina zenu mbinguni, mahali nondo au kutu, wala wezi haviwezi kufikia. Maana ilipo hazina ya mtu, hapo ndip roho yake ipo-Mat.6:19-20. Moyo ndio kiti cha akili ambako ufahamu, mawazo na nia zote uhifadhiwa. Hazina zilizowekwa hapa duniani umaanisha, akili iliyojawa na ufahamu wa kimwili, na hivyo, yenye kupanga na kutegemea vya mwili pekee-Warumi.8:5; Wafilip.3:19. Kama vile tumeshaona, hivi vyote vinapita; ni vya kuharibika. Kwa vile tumeelewa vizuri sana kuwa, huu mwili na hivi vitu ni vyakutumika tukiendelea na kujifunza maisha ya uzima, na baada ya hapo, Mungu ataviharibu- 1 wakor.6:13, basi, kama mtu akivitegemea, inamaana kwamba, vikiharibiwa, ataharibiwa pamoja navyo, maana, kuweka akili yako katika mwili ni kuiweka katika mauti-warum.8:6. Lakini kuweka hazina yako mbinguni ni kuwa na moyo uliojawa na ufahamu wa kile Mungu anaendelea kuumba ndani yetu( soma ujumbe wa, “mchakato wa uumbwaji wa mwanadamu”). Kwa vile huu umbwaji ni wa kiroho, basi, hauwezi kufanyika kwa vifaa vya kimwili, maana, mwili utamani ukipigana na roho, na roho ikipigana na mwili-Wagal.5:17. Hivyo basi, ili tuweze kuanza huu ujenzi wa uzima wa milele, lazima akili zetu zibadilishe ufahamu tulionao sasa, kutuhusu, kuhusu maisha yetu, na tuanze kutumia ufahamu tunaofundishwa na neno la Mungu, maana kwa hakika, hili neno ndilo uzima na roho-Yohana.6:63. Eeee, kwa kuitenda, tunaishi maisha ya milele. Baada ya kumaliza mafunzo yetu, huu mwili na vitegemeo vyake, yaani mali, ikiwemo hiyo akili ya uongo ya Shetani,vitapita- 1 Yohana.2:17. Kama ni huu mwili; utaondolewa-Wafilip.3:21; Yakubu.4:14. Kama ni mali, viwango vya kimaisha, na chochote kilicho kwenye mpango wa huu mfumo wa kimwili, vitayeyushwa kwa moto mkali- 2 Petro.3:12. Je, tunaona sasa ni kwa nini tunaambiwa tujitenge na haya maisha ya kimwili? Ni kwa sababu yanapita.
IWENI NA AKILI MOJA TU
Basi wandugu, ikiwa kweli tunatafuta uzima wa milele, Mungu ameuweka wazi mbele yetu, na anatuambia, chagueni uzima mpate kuishi-Kumbukumbu.30:19. Hebu kila wakati tupate kukumbuka hiki kitu kimoja ambacho ni cha muhimu sana. Kama Shetani hangekuwa hapa duniani, tusingeliumbwa katika mwili huu wa nyama na damu. Lakini kwa sababu ya Shetani, na dhambi, Kristo aliuvaa huu mwili wa dhambi, kwa sababu ya dhambi-Warumi.8:3. Tunaelewa kuwa, chochote kile Kristo alifanya, kilikuwa ni kielezo cha yale maisha na hatua tutakazopitia kuufikia ukamilifu. Hivyo, ni wazi kwamba, huu mwili uliumbwa kwa sababu ya Shetani na dhambi(maisha aliyoyaanzisha). Ni huu mwili ambao Shetani uutumia kuingiza hii, sheria nyingine ipingayo maisha-War.8:13; wag.5:17. Ni hii akili ( maisha) mbovu, vifaa na matendo yake, ukiwemo mwili, ambavyo, ndio yale maisha Mungu atayaangamiza kabisa yasiweko tena. Basi, tunachotakiwa kufanya ni rahisi. Tutoe hii akili na kuwacha kuitumia kabisa-Waef.4:22. Kwa yule ambaye ameamua kumcha Mungu, basi, itakuwa ni kama hii akili haimo tena ulimwenguni, maana kwake, huu mfumo(ulimwengu) umesulubishwa(umeangamizwa) kwake, na yeye, kwa huo-Waga.6:14. Mtu aliyefikia huo msimamo huwa amebaki na akili moja tu, na ndio sababu, hafanyi chochote kulingana na anavyofikiria, ila, kwa kila jambo, anakuwa mwangalifu kufahamu vile Mungu anaagiza-Mith.3:5. Wandugu, hii haitakuwa ni kama kuvuka barabara tu. Kama vile ilivyotuchukua kukua katika haya maisha ya kimwili, tuking’ang’ana kujifunza kutembea, huku tukianguka mara kwa mara, na mengine, ndivyo inavyokua katika huku kukua kwa kiroho. Kwa sababu hii, Bwana wetu anatuambia, pigeni vita vizuri vya Imani- 1 Tim.6:12. Sasa hivi tuko katika huu mwili, na tumezoea maisha yake kwa ushauri wa Shetani kiasi kwamba, haituchukui kung’ang’ana kutenda dhambi-Waef.2:3. Lakini kutenda amri ya Mungu uchukua kupigania kwa kung’ang’ana zaidi-War.7:21-23. Hapa ndipo kujifunza kwa njia ya uamuzi wa kila hatua kati ya hizi akili mbili kunakujia. Wengi wa wale tayari tumeamua kumcha Mungu tumekwama hapa kwenye kuamua. Hapa ndipo Yesu ananena juu yake anapoongelelea kuhusu mbegu iliyomea katika miiba ikasongwa isiweze kukua wala kuzaa-Mat.13:22. Na kama hatujui, basi na tuelewe kwamba, hii ndiyo maana ya kuwa kuwili, yaani kujaribu kutumikia mawazo mawili tofauti. Kwa maana tuko sasa katika roho. Lakini kila wakati mahitaji ya mwili na masumbuko ya maisha yake yanapotukabili, tunaanza kutumia akili ile ambayo tunajaribu kuitoa. Basi, tunabaki kwenda mbele na nyuma, na ndio sababu unaona, karibu wamchao Mungu wote hawajabadilika sana kiwango cha kuweza kuonyesha tofauti kamili kati yao na walimwengu. Kama hatutakubali kwa kauli moja kwamba, hakuna ufahamu mwingine wala namna nyingine ya maisha isipokuwa yale Mungu anatufundisha, yaani neno lake, basi, tutakuwa kila wakati tukigeuka na kurudia huu uongo wa Shetani, na kukaa kuyumbayumba kati ya mawazo hayo mawili; na mnajua kitakachofanyika? Hatutafaulu kuufikia uzima wa milele wala kuuingia ufalme wa Mungu ambao kwa huo, tuliumbwa. Mungu ako hapa saa hivi unapoendelea kuusoma huu ujumbe, akiita katika Kristo mwokozi wetu, na kukuambia wewe mwenye masikio; kimbieni mtoke Babeli(huu mfumo), kila mtu na aokoe nafsi yake. Maana niko karibu kuung’oa huu mti ambao sikuupanda-Yerem.51:6; mat.15:13. Tuamini tusiamini, lakini kila mtu ajue kwa hakika kuwa, haya maisha yote yanayotufanya tusimtii Mungu kama anavyosema katika neno lake yanafikia mwisho wake. Mwenye masikio na asikie vile roho anavyoliambia kanisa la Leodikia-Ufu.3:17-21.
Na Sauti yake ikikujia kupitia kwa mtumishi wake,
KANISA LA MWISHO LA MUNGU: TOVUTI( WEBSITE) > www.endtimecog.org: BARUA PEPE > endcog@gmail.com : ANWANI ZAIDI ZIKO NDANI YA TOVUTI KWENYE UKRASA WA MAWASILIANO. Makinika.
.