Kila mtu sasa hivi anapigania kuwa mkuu. Eee, watu kila mahali wanatafuta ukuu. Kulingana na vile mambo yalivyo, huu ukuu upimwa kwa yale mapato mtu amepata. Kunayo aina tatu za mapato ambazo ufanya mtu aonekane, ama kuhesabiwa kuwa mkuu. Ya kwanza, na ambayo ndiyo unayodhaminiwa zaidi ni utajiri, ikifuatwa na kiwango cha uongozi, na mwishowe tunaona la tatu likiwa kiwango cha elimu. Kunao mengine mengi lakini yenye dhamana ndogo. Utasikia kama vile, mwenye mbio zaidi, mpiganaji hodari, mwenye nguvu kushinda wengine, aliye msafi zaidi, eee, taja chochote kile na utakuta Yule aliye mbele kwa hilo jambo akihesabiwa kuwa mkuu kwa namna yake. Watu utumia huu mpango wa ukuu na kuibuka na viwango vya kimaisha katika uma. Kwasababu ya huu mvumo wa kuhesabiana ukuu, mashindano yameibuka, kila mtu akijaribu kujionyesha kuwa mkuu kushinda mwenzake.Hii imezaa, wivu, chuki, kampeini ya kimyakimya(masengenyo), vita na mauaji. Badala ya mtu kusaidia mwenzake afike kile kiwango cha maisha amefika, utakuta kwamba, kila mmoja anajaribu kumzuia mwenzake asimfikie ili abaki kuwa mkuu peke yake. Ni kwa nini? Kama kweli kuwa hapo juu( ikiwa ndio juu kweli) ndiko kufikia ukamilivu wa maisha, kwanini basi hawa wamefika wasizaidie wenzao hata na wao wapafikie ili wote pamoja waweze kufurahia maisha na ushirika wenye raha? Kwa nini mtu atake kuwa pale juu peke yake huku wengine wote wakibaki kumuimba- yaani kumsujudu? Kama huku ndiko kufaulu, ni kwanini matokeo yake ni haya maisha yalio kinyume na ya kuharibu ? Maana tunaona matokeo yake yakiwa ndoa zilizovunjika, taifa zilizogawanyika huku Serikali zake sikilumbana na waasi wanazozipinga; tunaona wengi wakifa kwa njaa ilhali wengine wamejaza magala na hawawezi kuzaidia wanaokufa. Eeee, ni kwa nini?
KUNAO KUTOKUFAHAMU
Mambo yote yale tumetaja hapo juu kuhusiana na maisha ni ya kiwango cha kimwili. Ama kunaye mtu anaweza kutuambia kitu kinachofanywa maishani leo ambacho hakihusu vitu au watu? Ni kwa nini basi maisha ni kuhusu vya kimwili tu? Labda hatujawahi kujua, lakini sasa, wakati umefika wa kufahamu, ya kwamba, kizazi cha leo kimekosa ufahamu ulio muhimu kabisa, ambao, watu wakiufahamu, wataweza kutatua matatizo yote yaliyomo ulimwenguni leo na kufikia ile amani na ushirika unaotafutwa usipatikane. Wasomi na wenye hekima wamegundua kwamba uhai ni lazima utoke kwa uhai, na pia, kila tukio ina chanzo chake. Hebu basi tutumie huu ufahamu kujifikiria. Kunaye Mungu muumba mbinguni ambaye aliviumba vitu vyote, wakiwemo wanadamu. Yeye peke yake ndiye mwenye uwezo wa kutuambia ni kwa nini maisha yako vile yalivyo sasa, na ni kwa namna gani yanaweza kubadilishwa yakawa mazuri na ya kutamanika. Basi, kumhusu mwanadamu, ndio, kuhusu lengo lake la kumuumba, anasema, “ Na tuumbe mtu kwa mfano wetu, na kwa sura yetu, na wawe na utawala juu ya…..dunia- Mwa.1:26”( Kwa maelezo ya ndani, soma ujumbe uitwao, “ Msingi wa milele”). Ikiwa tutaipata siri ya kushinda, lazima tuanze kwa kujifahamu. Basi, kulingana na muumba wetu, kunayo mambo mawili tunapaswa kufahamu kutuhusu sisi. Ya kwanza: Tuliumbwa tuwe kama Mungu(viumbe wa kiroho, wenye akili na utukufu kama Mungu). Baada ya kuwa kama Mungu, tunaenda jambo la pili ambalo ni; kuitawala Dunia. Sasa, Mungu ni roho na wa milele. Lakini, kinyume na hiyo, ameumba mtu wa mavumbi, na mwenye maisha mavupi (some ujumbe wa “mwanadamu ni nini” kwa maelezo zaidi). Ina maana basi kuwa, Katika huu mwili wa mavumbi, Mungu hajamaliza kumuumba mtu, maana hatujioni tukiwa roho na wenye uhai wa milele kama yeye( kama alivyokusudia). Kama ni hivyo basi, kwa nini Mungu hakutukamilisha mara ile alituumbia huu mwili? Anangojea nini?( Kwa maelezo zaidi, soma ujumbe wa, “msingi wa milele”). Mungu halazimishi mapenzi yake kwa mtu yeyote. Kwa sababu hii, alituumba tukiwa na uhuru wa kuchagua tutakacho, ili tuchague kwa kupenda kwetu kama tunataka kuwa kama yeye au la. Mpaka sasa hivi, Mungu anangojea uamuzi wetu, ili aweze kuendelea na uumbaji wa mwanadamu, maana anatuambia, “ Angalia nimeweka mbele yako Baraka na uzima, laana na mauti……….kwa hivyo, nakushawishi uchague uzima- Kumbu kumu.30:15,19”. Basi, kufuatana na huu mpango, baada ya kumuumba Adamu, Mungu alimpa nafasi achague kama anataka kuishi kama Mungu au la( Soma ujumbe uitwao, “Miti miwili. Utaupata kwenye website> www.endtimecog.org). Soma pia katika Mwa.2:16-17. Ijapokuwa mapenzi ya Mungu ni kwamba, mwanadamu achague uzima, Adamu alichagua laana na mauti- Mwa.3:4-6. Na Mungu naye, akithibitisha uhuru wa mwanadamu wa uchaguzi, alimruhusu Adamu kuendelea na hayo maisha, lakini akajitenga naye, maana, “Alimfukuza kutoka katika shamba la Edeni- Mwa.3:24” ; Na tena, “ ….akimtenga na maisha yake-Waef.4:18”; “….akawaruhusu watu wa kila taifa kuenenda katika njia zao wenyewe- Matendo.14:16”.
UUMBAJI WAKOMA KWA MUDA
Tulianza kwa kushangaa ni kwa nini maisha yanahusu mambo ya kimwili tu; tukashangaa ni kwa nini Mungu hakuumba mwanadamu wa kiroho kama yeye na ilhali anataka mtu aliye kama yeye? Ukweli ni kwamba, mwanadamu alidanganywa na kutolewa kwenye mpango aliopangiwa na Mungu. Hivyo basi, alitenganishwa na Mungu akiwa bado kwenye kiwango cha kimwili; eee, kabla hajapata ufahamu wa kusudi la kuumbwa, wala kuumbika kikamilivu. Tunajua kwamba, akili ya mwanadamu haiwezi kutengeneza ufahamu. Lazima ipate ufahamu kutoka mahali, aitha kwa njia ya kusoma kutoka kwa mtu au kwa experimenti kwa vitu anavyohusiana navyo katika kazi zake, na hii ni kupitia kwa milango mitano ambayo huwezesha akili kushika, yaani, kwa kuona, kusikia, kunusa, kushika ama kuonja. Kitu chochote kilicho nje ya hiyo milango, akili ya mwanadamu haiwezi kufahamu( kwa undani wa hayo, soma ujumbe wa, “jina la Mungu” katika website yetu, yaani >www.endtimecog.org). Shetani naye, hali akiyaelewa hayo yote, na akiwa na ufahamu kuwa mwanadamu atafanywa kuwa mungu( yohana.10:34), Alimdanganya Awa kuwa, tayari ashaa fanywa kama Mungu, kwamba amekamilika na haitaji Mungu ili kuendelea na maisha, maana alimwambia, “…….hakika hautakufa(una uzima wa milele kama Mungu)…….wewe ni kama Mungu(wewe ni kiumbe wa kiroho)-Mwa.3:4-5”. Kwa vile mwanadamu alikubali huu uongo, basi Mungu aliheshimu uamuzi wake, na hivyo akamwachilia avune matunda ya maisha hayo mabaya ambayo ni haya tunaoyaona leo kila mahali. Mpaka dakika hii, isipokuwa wachache sana, mwanadamu anaishi katika ujinga(kutokufahamu). Hamjuhi muumba wake, hajijui, wala hajui ni kwa nini aliumbwa na ni maisha yapi yaliyo ya haki, maana, “….amepofuka katika ufahamu wake, na kutengwa na Mungu(Ambaye ndiye pekee awezaye kumfundisha ufahamu)……Waef.4:18; Warumi.3:9-12pia”. Kwa hivyo, katika huu ujinga, na kufuatilia uongo wa Edeni, kila mtu anaishi kujifanya mungu( yaani anayejiweza); na hapa ndipo uja ule ushindani na maisha yaliyojaa maovu. Huku mwanadamu akiwa na uwezo wa kufahamu ya kimwili pekee, na akitumia uongo wa Shetani kuhusu hayo ya kimwili, ulimwengu wa kiroho haupo katika fikira na mipango yake, na matumiishi ya kweli ya huu mwili hayaeleweki pia. Je, utashangaa nikikuambia kwamba sasa hivi( na ninaongea na uthabiti), karibu watu wote hawana ufahamu wa Mungu , au Shetani? Kile wanaita shetani si yeye, na pia, wanachodhania kuwa Mungu si cha kweli. Huku ndiko kutofahamu kulioko kwa wanadamu na ndio chanzo cha maovu yote. Je, wataka kufahamu na utoke kwenye huu ujinga? Kama ndio, basi hapa ndipo siri ya kushinda uanzia. Kwa vile tumeona jinsi akili ya kimwili haitengenezi ufahamu, vile ni lazima ipate ufahamu kutoka kwengineko, basi tuelewe kwamba kunao ulimwengu wa kiroho ambao ndio unatumia akili zetu kuzipa ufahamu, na ueleweka tu kwa njia ya ufunuo, maana, “ akili ya asili haiwezi kuyafahamu mambo ya kiroho……. Maana yanaeleweka tu kwa jinsi ya kiroho- 1 Wakpri.2:14”. Pia, tunapaswa kuelewa kwamba, Shetani ni muongo na hawezi kuwafunulia wanadamu kitu cha kweli, maana nia yake ni kwamba wanadamu wote wafe. Kwa vile akili ya kimwili inategemea uwezo wa kiroho ili ipate ufahamu wa kiroho, na tumeona vile mwanadamu alikubali uongo wa shetani, basi, badala ya kupata ufahamu wa kusudi la Mungu la kuwaumba, ambao ungewezekana tu kama mwanadamu angepokea roho ya Mungu, alipata uongo kupitia roho wa Shetani, ambao ulimpa ufahamu wa uongo kuhusu kusudi la maisha yake-Waef.2:2-3; Ayubu.9:24. Basi, hali akiwa hajui kusudi la maisha, na huku akiwa na ufahamu wa kimwili peke yake, ambao unaelewa tegemeo la kimwili pekee, yaani mali na watu, watu walibakia kukimbizana, kutafuta, na kutegemea vya kimwili, ata wakafikia kusema kuwa, mtu amekufa bila pesa. Hii ndio sababu, pesa na mali zimekuwa ndizo mungu wa ulimwengu huu, maana kiroho hakijulikani kwa hii akili ya mwili. Kwa vile pesa ndio inayoabudiwa zaidi, basi imeachiria wenye pesa kuwa kama miungu na watu wakuabudiwa na wale sio nayo. Hata hivyo, hata mtu awe tajiri kiasi gani, au kiongozi wa juu zaidi, au aliye soma zaidi ya wote, kile utasikia wakiongelelea, wakifikiria, amakutenda, kitakuwa tu kwenye kiwango cha kimwili, yaani, vitu kama maendeleo, afya njema, usalama na kadhalika; vitu ambavyo ni vya huu mwili ambao mwisho wake ni kaburini. Uniambie basi, kama huu ni ufahamu kweli. Yaani umesoma sana, ukatajirika zaidi, ukawa kiongozi wa wote, ili baadaye ufe tu. Huu ni ufahamu wa aina gani unaoishia kwenye kifo ilhali Mungu alituumba ili tuishie kwenye uzima wa milele huku tukiwa kama yeye? Eee ni ufahamu wa aina gani unaowaacha watu wakitegemeana, na kutegemea mali, vitu ambavyo uisha baada ya muda? Wapenzi, huu ni ujinga, ni kukosa ufahamu, maana muumba wetu anatuambia, “ Lakini wanapojipimanisha na wanadamu wenzao, na kujifananisha wao kwa wao, ni kwasababu hawana ufahamu- 2 Wakor.10:12”. Ndio, kama vile tumeona tangu mwanzo wa ujumbe wetu, tuliumbwa ili tuwe kama Mungu, sio kama wanadamu wenzetu. Lakini sasa, tuko hapa, tukitaka kujifananisha sisi kwa sisi. Unataka kuwa kama kiongozi Fulani; kama tajiri Fulani; kama msomi Fulani badala ya kuwa kama Yesu. Eeee, Mungu hayupo popote katika akili zetu. Hii ndio sababu Mungu anatuambia kuwa, ikiwa tunajifananisha sis kwa sisi, basi hatuna ufahamu, maana nia ya pekee ya kufanikiwa kulingana na kusudi la Mungu la kutuumba, ni kumwangalia na kujifananisha naye, maana alituumba tuwe kama yeye, tuishi yale maisha yake. Hii ndio sababu anasema, “ Amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu, na kumfanya kuwa msaada wake, eee, Yule ambaye moyo wake umsahau muumba wake- Yerem.17:5”. Hii ni kwasababu, Mungu peke yake ndiye awezaye kutupa uhai, na kututegemeza kwa huo huku akiendelea kutuumba hata atufanye viumbe wa kiroho, “ maana hiki ndicho alichotuahidi, yaani, uzima wa milele- 1 Yohana.2:25”. Lakini kuhusu mwanadamu ambaye unataka kumtegemea, “..yeye ni mavumbi; na mavumbini ni lazima arudi baada ya muda Fulani- Mwa.3:19”. Basi ikiwa mtu ndiye tegemeo lako, hapo atakaporudi mavumbini, utabaki na tegemeo gani? Wandugu, fahamuni na kuelewa kwamba, hakuna mwanadamu aliye mkuu kushinda mwingine, maana wanadamu wote ni viumbe ambavyo bado havijamaliza kuumbwa, bado, “….viko mikononi mwa mfinyanzi- Isa.64:8”. Kila mtu, wakuu kwa wandogo, matajiri kwa maskini, wanyonge kwa wenye nguvu, wote wanamtegeme Mungu ikiwa watakamilishwa kuwa viumbe wa kudumu, la sivyo, “ …… kwa mwanadamu, hakuna msaada(awe mkuu au mdogo). Maana uhai ukimtoka, yeye urudi mavumbini; siku hiyo hiyo, mipango yake yote ukomea hapo—Zaburi.146:3-4”. Lakini kwa vile tulitenganishwa na Mungu kabla hajatupa huu ufahamu, basi, tunaishi kubahatisha, mtu mtu aliyelewa, “….kila mtu akibahatisha mipango yake, akitenda kulingana na roho yake iliyo mbovu- Yerem.18:12”. Hii yote ni kwa sababu, tulijifunza namna ya kuishi kutoka kwa wazazi wetu ambao, “….walirithi uongo, vitu ambavyo haviwezi kufaidi chochote- Yerem.16:19”. Tufanye nini basi? Je, unataka kushinda? Unakata kutatua shida zako zote na uishi kwa furaha? Kama ndio, ni lazima ugeuke; uwache kuwatazama wanadamu, na kuwategemea, na badala yake umtazame na kumtegemea muumba wako, maana Bwana anaita akisema, “ Usiwatazame wanadamu wenzako kwa msaada. Njooni kwangu enyi nyote msumbukao na wenye mizigo mizito ya dhambi, name nitawapumzisha—Mat.11:28”. “ Mtumaini Bwana(sio mwanadamu) kwa moyo wako wote, wala usitegemee fikira zako mwenyewe, mbali, kwa kila jambo, mtumaini yeye, naye atazinyoosha njia zako- mith.3:5”. “ Maana mimi ndimi Bwana Mungu wako; akufundishaye kufaidi, akuongozaye kwa ile njia unapaswa kuenenda kwayo- Isa.48:17”. Wandugu, hatuwezi kushinda ikiwa hatutaanza kwa kuamini kile Mungu ametuambia hapa. Nini? Kwamba wewe sio Yule mwanadamu Shetani alikudanganya kuwa, wala mwanadamu mwenzako sio mkuu au mdogo kukushinda. Ndio, tunapaswa kuelewa kwamba viwango vyote wanadamu wanatumia kujihesabia kuwa wameitimu kimaisha vinatokana na ule uongo wa Edeni, wakati mwanadamu alikubali kwamba yeye ni kama Mungu. Tumesikia mara nyingi katika mazishi, wahubiri wakifundisha kwamba, mwanadamu ni kuwili, yaani ni mwili, na pia ni roho, kwamba anapokufa(kama Shetani alivyowafundisha), hajafa mbali ametoka kwa huu mwili wa nyama, na kuhama kwend mbinguni. Ikiwa tutashinda, ni lazima tutubu kuhusiana na huu uongo, na tuanze kujifunza upya kutoka kwa muumba wetu kupitia kwa maandiko. Huu ndio mwanzo wa siri ya kushinda. Lazima tugeuke, tutoke kwenye “giza na kuingia kwenye nuru, tutoke kwenye uongo na kuingia kwenye ukweli- Matendo.26:18”. Ikiwa tunataka kuanza safari yetu ya kushinda, ni lazima tukubaki kuwa, wanadamu wote sawa ni mavimbi, na, isipokuwa Mungu awaumbe wawe kitu tofauti( ambayo ni yeye pekee awezaye kufanya hivyo), waote wtakufa, maana, “ Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke ni wa siku chache na amejawa na shida(maana hajijui)…..; yeye utoweka kama kivuli, na hawi tena; uja kama ua, na kunyauka-Ayubu.14:1-2”. Tuko pamoja? Tuko tayari kugeuka? Kama ndio, basi kuanzia hapa, tuwe wasikifu, na tufuatilie mafundisho kwa makini huku tukijirekebisha kulingana na haya maagizo ya muumba wetu. Eleweni kwamba, ni wale tu watakaokubali Mungu awajenge kwenye haya maagizo yake ambao watafanywa Yule mtu wa kioroho Mungu aliyekusudia wakati alituumba. Basi, je, Mungu anasema mwanadamu ni nini katika huu mwili wa nyama na damu?( soma ujumbe wetu uitwao, “mwanadamu ni nini” kwa maelezo zaidi). Ijapokuwa tuliumbwa tuwe kama Mungu, sasa hivi hatujafikia hicho kiwango. Katika haya maisha ya sasa, tuko nusu wanadamu, maana mpango wa Mungu kuhusu uumbaji wa mwanadamu ni kwamba, “ Tuwe mwili wa mavumbi kwanza, halafu baadaye tuvae wa kiroho. Maana kam vile tulivyouvaa huu wa mavumbi, na vivyo hivyo, tutauvaa ule wa kiroho- 1 Wakor.15:46,49”. Hii ni kwa wanadamu wote, mkuu kwa mdogo sawa. Kumbuka, ushauri tunaoutoa hapa ni kwa wale wamekubali kutoka kwenye uongo na kufuatilia ukweli. Eee, wale wamegudnua kwamba hakuna viwango tofauti vya wanadamu. Maana tumeona vile wote wamedanganyika, na vile, isipokuwa Mungu awaumbe zaidi, wote wanaelekea kuangamia maana, “ Mungu hana upendeleo- Warumi.2:11”. Hali tukiyaelewa hayo, tuendelee basi. Kama tulivyoona, katika huu mwili, Adamu, na sisi zote, hatukuumbwa na ufahamu. Wakati wa kuzaliwa(ua Adamu kuumbwa), hatukuwa waovu wala watakatifu. Hali ya maisha uanzia hapo, ikitegemea kile mtu binafsi atachagua(soma ujumbe wetu uitwao, “Je, wewe ni mkristo?”). Kufuatia mpango huu wa uhuru wa kuchagua, Mungu anawapatia watu wote nafasi ya kuchagua kama wanataka kuwa kama yeye, kabla ajaendelea kuwaumba na kuwakamilisha kuwa viumbe wa kiroho. Kwa hivyo, wale wamechagua kuwa kama Mungu, hawa ndio wanaitwa kanisa la Mungu, na hao ndio wamerudi kwa muumba wao, ambao kwao, Mungu naye ameanza hatua ya pili ya kuwakamilisha, hatua ambayo uanza kwa kupokea roho takatifu, ambayo utupa ufahamu wa kweli kuhusu maisha ya Mungu aliyokusudia kwa mwanadamu, na ambao tukianza kutenda kulingana na huu ufahamu, tunaanza kuumbika tabia hiyo ya Mungu mwenyewe, na hivyo kufanyika watoto wake, maana, “ Ni roho ya Mungu ikiunganika na roho yetu ambayo utushuhudia kuwa tu wana wa Mungu”, “ Maana sasa tumepokea roho wa Mungu ili tuweze kufahamu—Warumi.8:16; 1 Wakor.2:12”. Kuanzia hapa, mtu upanda ngazi ya uumbaji, na uanza mtazamo wa maisha uliyo tofauti na huu wa sasa. Roho ya Mungu ufungua macho ya mwenye kuipokea na kumpa kuyafahamu haya maisha ambayo hayawezi kujulikana katika hii akili ya kimwili. Hii pia umfanya mtu kuanza kuhusiana na Mungu huku akimpinga Shetani. Kuanzia hapa pia, mtazamo wa maisha ugeuka, kutoka kwa ubinafsi, na watu wanaotuzunguka. Tunaanza kujifahamu, na kuwafahamu wandamu kulingana na vile Mungu anasema, na sio vile tunadhania. Tunaingia kwenye ulimwengu war oho ambapo tunaanza kuhusiana na Mungu huku tukipigana na Shetani aliye aitha kwa akili zetu, ama za watu tunaohusiana nao. Hii ndio sababu Mungu anatuambia kuwa, “ Maana vita vyetu sio dhidi ya nyama na damu mbali(hatupigani na watu), ni dhidi ya mamlaka,….dhidi ya pepo wabaya katika ulimwengu war oho- Waef.6:12”. Wapenzi, ni huu ufahamu ambao unatufungua macho kuielewa siri ya kushinda. Ulimwengu katika hali ya upofu kuhusu ulimwengu war oho, na ukiweza kuelewa mambo ya kimwili pekee, unawacha kila mtu akipigana na jirani yake. Watu wanapigana, au kutegemeana, kutafuta sifa,kulaumu, taja chochote kile na utaona vyote vunahusu wanadamu na sio Mungu wala Shetani(sio ulimwengu wa roho, mbali huu wa mwili), na hii yote ni kwasababu hawaoni ile roho inafanya kazi ndani yao, iwe ni ya Mungu au ya Shetani. Kwa sababu ya huu upofu, “….. wanabadilisha ukweli kuhusu Mungu kuwa uongo, huku wakiabudu kiumbe badala ya kumwabudu muumba- Warumi.1:25”. Pia, wakitumia huku kutofahamu kuhusu vitendo vya shetani mioyoni mwa watu, wanalaumu mtu badala ya kumlaumu Shetani anayemshika mtu mateka, “…roho Yule atendaye kazi katika wana wa kuasi- Waef.2:2”. Hila kwa sasa, wale wamefunguliwa macho wameanza kutenda kulingana na ukweli.
NDANI YA AKILI YAKO
Majaribu yale makali zaidi katika maisha, na ambayo yamewafanya wengi wasikue kiroho huwa yanatoka kwa akili ya mtu binafsi, na pia kwa watu wanaomsunguka wakati huyo mtu anawapa nafasi katika akili yake. Lakini haya yote utendeka kulingana na mawazo yaliyomo ndani ya hiyo akili. Baada ya mwanadamu kukubali uongo, na kujenga maisha yake juu ya huo, basi alifanyika kuwa mtumwa wa Shetani; ama hamjasoma kwamba, “…..mtu ni mtumwa wa Yule anayejikabithi kwake kumtii, iwe ni dhambi iletayo mauti, au ni utiivu uletao uhaki na uzima- Warumi.6:16”. Kwa hivyo, kufuatana na huu utumwa, wanadamu uhuzisha yote yanayotendeka maishani mwao, aitha na wao wenyewe, ama na majirani zao, na hii ni sababu, kama tulivyoona, ulimwengu wa kiroho haujulikani kwao. Kwa matendo mema, Shetani huwaonyesha watu kwamba ni wao wanaofikiria na kufanya, huku akihakikisha Mungu hajaonekana kabisa. Kwa matendo mabaya, yeye pia anahakikisha kuwa hajagundulika kuwa mwene kuwapa wanadamu huyo roho wa kuasi; badala yake, huwaonyesha wanadamu kwamba ni mtu binafsi anayefanya hayo. Kwa sababu hii, tunaona watu kila mahali, wakisifiana, au kulaumiana, maana hawajui mwenye kuwapa huyo roho awafanyaye kutanda hivyo, eee, hawajui ni nani anayetawala akili zao kuwapa kufikiria na kutenda hayo. Kila ambaye amefunguliwa macho nakuelewa huu uongo amegundua kwamba, sio yeye wala jirani yake ambaye anayatenda, mbali ni Yule roho atendaye kazi ndani ya mtu, maana imeandikwa, “ Vita miongoni mwenu utoka wapi? Si zinatoka kwa tamaa(sio kwa watu) zipigao vita ndani yenu-Yakubu.4:1?” Sasa, kwa vile akili zetu zimefunguliwa( naongea kuhusu walio wa kanisa la Mungu), na tumeelewa unyonge wetu, na hivyo tumeamua kuvaa utu wema na wa kweli kama anavyotufundisha muumba wetu, ni lazima tukubali kuanza upya. Tutaanzia wapi basi? Lazima tuwache kumsikiliza Shetani kupitia kwa tama zetu, au kupitia kwa watu wanaotuzunguka, na tuanze kumsikiliza Mungu, eee, “ tutoe utu wa zamani utokanao na maisha yetu ya awali yanayotuharibu kupitia kwa tama zenye kudanganya-Waef.4:22”. Huku ndiko kujikana. Kukubali kwamba, chochote tumekuwa tukishikilia kama ukweli kutuhusu, kuhusu wanadamu wenzetu, kuhusu Mungu, Shetani, ama mali, na maisha kwa ujumla ni uongo, na baada ya hapo, “kama watoto wachanga, tutamani maziwa(neno la kweli lisiochanganywa) yasio goshwa, ili kwa hiyo, tuweze kuukulia wokovu- 1 Pet.2:2”. Lakini sasa, sisi zote tumezoea kuangaliana na kuigana sisi kwa sisi. Hapa tutaiga nani sasa? Ni mfano gani tulionao wa kufuata? “ Iweni watu wa kumuiga Mungu-Waef.5:1”. Wandugu, tuliumbwa tuwe kama Mungu, na sio kama wanadamu waliodanganyika. Lakini sasa, Mungu yuko wapi hata tumuige? Tutamwona wapi na aonekani kwa macho?
YESU KRISTO
Ili kuonyesha upendo wake usio na kifani kwa wanadamu, Mungu(neno) alijinyima utukufu na umilele wake, “……akachukua kiwango cha mtumishi, akazaliwa kama mwanadamu wa kimwili; na huku akiwa kama mwanadamu, akajinyenyekeza kufika kiwango cha mtumwa, ata kujitiiisha kwa kifo-Wafili.2:7-8”. Hii alifanya ili atupe kujielewa kwamba sisi ni mavumbi, watu waharibikao na kufa, na wala sisi sio miungu kama alivyotudangana Shetani. Eee alichukua haya maumbile atuonyesha yale maisha tunapaswa kuwa tunaishi sasa hivi katika huu mwili, ni kile tutakuja kuwa tukiisha kamilika, “…..akawa mtangulizi na mwongozo wa maisha yetu-Waeb.12:2”. Ndio, Kristo aliyapitia yale maisha tunapaswa kupitia kabla hatujafanywa miungu, hivyo akawa ndiye ule mfano tutakuwa tukiangalia(sio watu) kujipima kama tunaendelea vizuri. Kwa hivyo, kama tutamuiga Mungu, ule mfano aliotupa ni Kristo Yesu(sio mchungaji au mtu yeyote), maana, “…. Mungu alikuwa ndani ya Kristo Yesu akupatanisha ulimwengu naye-2 Wakori.5:19”. Akiongezea uzito hapa, anatuambia kwamba, “ Ndani ya Kristo ndiko kumeficha utajiri wote wa hekima na ufahamu wa siri za Mungu- Wakolos.2:2-3; Waebr.1:i-2”. Wapenzi, tunataka kufaulu kupiga hii vita nzuri ya imani. Hii ndio sababu tunachimba kila andiko ili tuipate kwa ukamilivu hii siri ya kushinda. Kufikia hapa, naamini tumewaondoa wanadamu wote(tukiwemo baadhi yao), wasiwe tena waalimu wetu au mfano kwetu kuhusu yale maisha tupaswa kuishi. Pia, kama Yesu mfano wetu, tumejikana, na kujikubali kuwa mavumbi(tusio na maana yeyote katika huu mwili), na kutoa uongo wote ambao tumekuwa tukitumia kujikweza, kujitukuza, kujitakia na kukubali kuanza upya, huku tukifuatilia kwa uangalifu, maagizo ya maandiko. Tumebakia kumtazama Mungu peke yake ambaye ametupa Yesu kuwa kielelezo chetu kwa kila kitu- yohana.13:35”. Hii imetuacha tukiwa na goli tofauti kabisa ya kimaisha, ambayo ina ufahamu na njia tofauti kabisa kuhusu vile tutaifikia; hii ikiwa sababu nzuri iliyomfanya Kristo kutuambia vile hatupaswi kufuata mfano wowote kuhusu, kufikiria au kutenda kutoka kwa walimwengu, maana anasema, “ Mataifa uwakalia wanaowaongoza(kujifanya miungu), na kuwa na mamlaka juu yao. Lakini isiwe hivyo kwenu(nyinyi wa kanisa la Mungu)- Mat.20:25-6”. Ni kwa nini? Maana anaelewa vile sisi na wanadamu wenzetu tusivyo wakamilivu, na hivyo tusivyo na ufahamu wa kutenda haki. Anaelewa vile kila mtu katika huu mwili anaendelea kuumbwa nab ado hajakuwa kama Mungu. Anaelewa pia vile mwanadamu alidanganywa na kuondolewa kwenye huu mpango( soma ujumbe wetu uitwao, “msingi wa milele”). Hali tukijijua kuwa wasio wakamilivu, inawezekanaje basi tumuiga mtu ambaye sio hana ufahamu,na asiye mkamilivu? Si Yesu mwenyewe asema waziwazi kuwa, “…..kipofu akimfuata kipofu, hao wawili utumbukia kwenye shomo-Mat.15:14?” Wandugu, ikiwa tutashinda, ni lazima tuwe waangalifu kujifunza kwa Mungu na sio kwa mtu yeyote. Ndio, tunaelewa kwamba, Mungu utumia wanadamu, ila, ambaye atatumiwa na Mungu atajulikana kwa kuwa, “..ataongea neno la Mungu(sio mawazo yake mwenyewe)-Yohana.3:34”. Kufuatana na huu uangalifu, badala ya kutenda kulingana na vile tunaona watu, au vile tumezoea kufanya, Kristo anatuambia, “ Msitende kulingana na vile mnavyofikiria, mbali kwa kila jambo, mtumainini Bwana, naye atazinyoosha njia zenu- Mith.3:5”. Hii itawezekana tu kwa wale ambao wamekubali kwamba, wamekuwa wakiishi kwa uongo. Kama uwezi kukubali hivyo, basi haiwezekani kwako kumtumaini Mungu; bado uko katika uongo wa Shetani(kwamba wewe ni kama Mungu). Katika huu mwanzo mpya, badala ya kusifu watu, huku ukiwatumainia, Yesu anatuambia kwamba, “ tuwe na Bwana wa majeshi kuwa hofu yetu,… na peke yake awe ndio tumaini-Is.8:13”. Soma pia, Mat. 10:28. Kuonyesha mfano wa kile anachosema, Yesu wakati wa maisha yake ya kimwili, “….hakujiaminisha kwa mtu yeyote; maana alijua mwanadamu ni nini na hakuitaji mtu amwelezee- Yohana.2:24”. Hii ndio sababu uangalifu wake na mafundisho yake yote yalikuwa kwa Mungu, maana, “…hakumjali mtu yeyote, wala kuogopa mamlaka ya wanadamu-Mat.22:16”. Je, huu ndio msimamo wako katika imani ulionayo katika Kristo? Labda, utaharakisha kusema ndio kabla ujafikiria na kujichunguza. Lakini ukijiangalia, utakuta mafikira yako yote, nia za moyo wako maneno na vitendo vinahusiana nawe, ama wanadamu, kujifanansha, kujitegemeza, kutafuta sifa, n.k. Utakuta raha yako ni wakati wanakuunga mkono na kukusifu. Hofu yako ni wakati wanakudharahu, na kukutenga nao. Hii in maana gani? Utaita huku, kusimama mbele ya Mungu, ukijifananisha na Yesu? Ikiwa bado hofu yako ni kwa wanadamu, basi, “…. Wewe ni nani umwogopaye mwanadamu ambaye ufa, mwana wa adamu ambaye ni kama nyasi, na kumsahau Bwana muumba wako-Isa.51:12-13?” Ikiwa wewe bado uko kwa huu msimamo wa wanadamu, basi usijidanganye kwamba unanfuata Yesu. Bado uko kwa ile akili ya kimwili ielewayo ya kimwili pekee. Kwa ujumla, Maisha ya kiroho ambayo Mungu anaumba ndani ya wale wameyakubali hayategemei chochote cha kimwili. Ninachosema ni kwamba, “Imani yetu haipaswi kusimama juu ya hekima ya wanadamu mbali, juu ya nguvu za Mungu…..maana hatuongei kuhusu hekima ya ulimwengu huu, ama, ya wakuu wa huu ulimwengu ambao wanapita. Lakini twanena siri, hekima iliyofichika kwa Mungu, ambayo Mungu alikusudia tangu kuwekwa misingi ya Dunia, mambo ambayo wakuu wa dunia hii hawawezi kuyafahmu- 1 Wakori.2:5-7”. Hatuongei kuhusu haya maisha ya kimwili ambayo yanafananishwa na, “….. nyumba iliyojengwa juu ya changarawe, ambayo mawimbi yakija uanguka- Mat.7:26”; ambayo Bwana anatuambia, “ …….inapita-1 Yohana.2:17”. Tunaongea kuhusu, “……ulimwengu unaokuja wenye namna ya maisha tofauti- Waebr.2:5”, “……….ambayo jicho halijawahi kuona, wala sikio kusikia, wala kueleweka kwa akili za kimwili- 1 Wakor.2:9”. Hii inamaanisha nini basi? Hatuwezi kutumia hekima ya ulimwengu wa leo kufanya mambo au kuishi maisha yetu kama wacha Mungu. Kuonyesha vile haiwezekani kutumia ufahamu wa sasa kishi maisha ya kweli, Bwana wetu kwa kinywa cha Paulo anasema, “..huu ulimwengu umekufa kwangu ,name nimekufa kwa ulimwengu-Wagal.6:14”. Ndio, kwa wale ambao tumemgeukia Mungu, ulimwengu umekuwa haupo kwao, nao hawapo kwa ulimwengu; hawaishi kwa ulimwengu, maana, “….waaminio Mungu, hawaufahi huu ulimwengu-Waebr.11:38”. Huku ulimwengu ukihesabu kufaulu kuwa ni kupata utajiri, uongozi, na elimu ya juu, vitu ambavyo vinahusiana na huu mwili, na vikitumika kufuatana na uongo wa Shetani, wanaomwamini Mungu wana mtazamo tofauti. Kufaulu kwao utegemea vile mtu ameumbika akili na tabia za Mungu(soma ujumbe wetu, “Thamana ya mkristo” kwa maelezo ya ndani). Kinyume cha ulimwengu, angalia vile Mungu na wenye kumwamini uhesabu kufaulu kimaisha.
UKWELI DHIDI YA UONGO
Ulimwengu wa leo utegemeza maish yake kwa Shetani, ule uongo wa Edeni(mwa.3:4-6), ambo uliwaacha wanadamu wakiwa wametengwa na ufahamu wa kweli, huku wakibakia kutenda mambo ya kimwili kama walivyofundishwa na Shetani. Ulimwengu ujao, ambao wote wamchao Mungu wanatazamia unategemea kuishi kulingana na vile Mungu anaseam katika neno lake, nah ii uwezekana tu kwa njia ya ufunuo, na haieleweki nah ii akili ya kimwili, “maana twaenenda kwa imani, sio kwa kuona kwa macho- 2 Wakori.5:7”. Kulingana na uongo wa Shetani, mwanadamu ni kiumbe mwenye miili miwili, mmoja wa kiroho, na mwingine huu wa nyama. Kulingana na huu uongo, mtu hafi; mbali yeye uhama kutoka kwa huu mwili wa nyama na kuenda mbinguni- eee, Mungu amemuita. Kulingana na ufunuo wa Mungu muumba, “ Mwanadamu ni mavumbi, kuvuli kinachopita, aharibikaye, kama nyasi-Mwa.3:19; Ayubu.14:2; Isa.40:6-7”. Kulingana na maisha ya Shetani, mwanadamu aliumbwa kuishi haya maisha ya kimwili peke yake; yaani alizaliwa, asome, apate mali, ajifurahishe kimwili, baada ya hapo, amefikia kilele cha maisha, yaani—kifo-Mhubiri.2:17-22; 5:15-17. Kulingana na ufunuo wa Mungu, Mwanadamu ako hapa ili ajifunze kufikiria na kuishi kama Mungu, ambayo uwezekana tu ikiwa mtu ataishi na kufikiria kulingana na neno la Mungu, ambayo kwa kuitenda, mtu uumbika tabia ya Mungu, ili atakapo kamilika abadilishwe na kufanywa kiumbe wa kiroho, na kuurithi ufalme wa Mungu-Mwa.1:26; Waef.4:23-24; Wafili.3:21; 1 Yohana.2:25. Ukiangalia yale maisha watu wanaishi leo, yote ufanywa kwa mtazamo wa watu wengine; vile wanaona, vile wanasema, vile wanafikiria, vile wanatenda. Lakini kwa wale wamemgeukia Mungu, wanafanya kila kitu kwa mtazamo wa, vile Mungu anaona, anasema, anataka, anatenda. Tunao mifano mizuri ya wale wliotutangulia kumgeukia Mungu na kuishi maisha yake. Petro aliweza kuwakabili wakuu wakiyahudi, na kuwaambia, “…imetupasas kumtii Mungu kuliko kuwatii wanadamu- Matendo.5:29”. Paulo naye anasema, “ Natafuta kupendwa na wanadamu? Au najaribu kuwafurahisha watu?. Ikiwa mpaka sasa natafuta kuwafurahisha wanadamu, basi sifai kuwa mtumishi wa Kristo- Wagal.1:10”. Yeyote ambaye amemgeukia Mungu amehamisha mapenzi yake kuhusu maisha kutoka kwa huu mwili, na kuanza kutazamia ule tulioahidiwa wa kiroho. Na kwa vile maish ya Mungu ni mageni kwetu, na ambayo akili ya kimwili haiwezi kuyaelewa, basi sisi ufuata tu kile Mungu anasema, na sio kile akili zetu zinafikiria. Hii ndio sababu yanategemea imani. Nini? “…….hakikisho la vitu vitumainiwavyo, thibitisho ya vitu visivyoonekana- Waebr.11:1”. Kuwezesha hiyo, Mungu ametupa mlango mwingine wa ufahamu, ambao uiwezesha hii akili ya kimwili kuyaelewa mambo ya kiroho, kwa njia ya ufunuo, maana, “ Ingawa tunaishi ulimwenguni(huu mwili), hatupigani vita vya kimwili, maana silaha za vita vyetu….. vina uwezo wa kiroho wa kuvunja ngome. Tunaharibu mabishano(ndani ya akili zetu), n kila kijiinuacho(kiburi) kinyume na ufahamu wa Mungu, na kutega kila fikira na tama viweze kumtii Kristo- 2 Wakori.10:3-5”. Imani ni kukubali kile Mungu asemacho katika neno lake, halafu kulazimaisha ile milango mitano ya ufahamu, kuona, kusikia, kunusa, kuonja, na kushika kulingana na neno la Mungu. Hii ndio kazi ya roho takatifu ya Mungu ndani ya mioyo ya waaminio. Baada ya muda wa kusizitiza kuishi kulingana nah ii neno, hii milango ya ufahamu uanza kutenda kila kitu kulingana na neno kinyume na ile kawaida ya mwili ya kudhania, na kwa njia hii, tabia ya Mungu na akili yake uumbika ndani ya mwenye kujitiisha hivyo. Kila wakati mtu huyo anavyoona ama kusikia, hatua ya pili huwa ni( sio kudhania na kuamua mbali ), “ Mungu anasemaji kuhusu hiki ninachoona ama kusikia( maana akiwa ndiye muumbaji, yeye peke yake ndiye ajuaye kila kitu)”. Ni kwa huku kusizitiza pia ambapo, sheria za Mungu uandikwa mioyoni mwa wenye kujitiisha, na kuzifanya kuwa, “……hekima na ufahamu wetu- Kummb kumbu.4 :6”. Wandugu wenzangu; hii ndio siri ya kushinda, yaani, sio kunenda kulingana namadhanio yetu, mbali kulingana na vile Mungu anasema, maana, “ Huku ndiko kushinda kushindao, ile imani yetu- 1 Yohana.5:4”. Mukwaruzano uliyoko kati ya akili zetu za kimwili, zikiendeshwa na tama zetu kama zinavyoongozwa na Shetani, na roho wa Mungu akituwezesha kuzipinga, ndiyo ile hali inayowezesha uamuzi na kuumbika tabia- Warumi.5:1-5, na ni wale tu wanaokaa kitako(kwa uwezo wa roho), wakipinga akili ya kimwili huku wakitumia ile ya roho wa Mungu(kwa neno lake) ambao wanaendelea kuumbika kiroho, maana, “ ni kwa wale ambao akili zao zimefundisha kwa kutenda kupitia uvumilivu, kutofautisha kati ya wema na uovu-Waebr.5:14”. Inachosema hapa kwa kumalizia, ni kwamba, kushinda ni kwa wale ambao wameamini kabisa kuhusu lengo la maisha yao kama anavyoeleza Mungu katika neno lake, ambao, “…kwa uvumilivu huku wakiendelea kutenda wema, ikiwa ni jitihada la kutafuta heshima na kutokuharibika, ambao Mungu atwapa uzima wa milele- Warumi. 2:7”; maana hii ndiyo siri ya kushinda, yaani kuenenda kwa maagizo ya muumba wetu, maana anatuambia, “ Mimi ndimi Bwana Mungu wenu, awafundishaye kufaidi, awaongozaye kwa njia iwapasayo kuenenda kwayo-Isa.48:17”. Mwenye masikio na asikie vile roho wa Mungu analiambia kanisa. Haya yote unayapokea kutoka kwa muumba wako, kupitia kwa mjumbe wake, Yesu Kristo, kwa njia ya chombo chake kiteule, kanisa lake. Ikiwa unataka kujikabidhi kwake ili aendelee kukuumba, na uanze hii safari ya kushinda, basi jifunze mengi zaidi kwake kwa kujiunga naye kupitia kwa,
KANISA LA MWISHO LA MUNGU.