UBATIZO

Wakati Yohana Mbatizaji alikuja akihubiria watu habari za kuja kwa Yesu mara ya kwanza,wote waliomwamini, “walitubu dhambi zao naye akawabatiza-Mat.3:6”.Kubatiza maana yake ni kuzika ndani ya kitu.Sio lazima iwe ni maji.Hii ni neno lililotafsiriwa kutoka kwa neno la kigiriki,ambayo maana yake ni,”kuingiza kitu ndani ya kingine mpaka kimefunikwa kabisa”.Kwa hivyo,waliomwamini,aliwaingiza ndani ya maji kwenye mto Yordani,yaani,aliwazika ndani ya maji. Hii ina maana gani?Inayo umuhimu wowote katika wokovu? Je,ni lazima mtu abatizwe ndio aweze kuwa mkristo? Hebu tuweze kumsikiliza yeye ambaye peke yake ndiye ajuaye mambo yote.Baadaye,Yohana aliwaambia wote aliowabatiza,”Mimi nawabatiza kwa maji,kuonyesha kwamba mmetubu.Lakini kunaye ajaye nyuma yangu ambaye atawabatiza kwa roho takatifu na kwa moto-Mat.3:11”.Tunaona baadhi ya watu wengine wanaojionyesha kumwamini huyu anayenenwa na Yohana,wakibatiza watu wao kwa kuwapitisha chini ya kitambaa chekundu,kumaanisha,wamewabatiza kwa moto.Wengine hawabatizi kabisa,huku wakiamini kwamba,mtu akimkubali Yesu,tayari amepata ubatizo wa roho,yaani amebatizwa kwa roho takatifu,hii ikiwa ni njia ya kutimiza usemi wa hicho kifungu tumeona(kwa roho na moto).Lakini sasa,ukweli uwapi? Ni upi ubatizo wa haki unaokubalika mbele ya Mungu? Ili tuweze kuelewa,ni vizuri tuone utaratibu uliowekwa,ambao umeelezwa katika maandiko,ndiyo tuweze kufuatilia bila kubahatisha.Baada ya Petro kuwahubiria wayahudi wakati wa sikukuu ya Pentekosti huko Yerusalemu,wengi wao waliguswa na hayo mahubiri,wakamuuliza Petro; “basi tufanye nini?” “Petro akawaambia, ‘tubuni dhambi mkabatizwe kila mmoja kwa jina la yesu,mpate ondoleo la dhambi,nanyi mtapokea roho takatifu-Matendo.2:38”. Hizi ndizo hatua tutakaofuatilia ikiwa tutaelewa maana ya ubatizo,na pia ndio kipimo kwa wale watu waliobatizwa, kujichunguza na kuona kama kweli ni ubatizo wa haki au la. Jambo la kwanza ni,

                                                             KUTUBU

                            Kutubu maana yake ni kuwacha, au kugeuka,kutoka kwa kitu Fulani. Hapa, Bwana wetu kupitia kwa Petro anatuambia tutubu dhambi-yaani kwa neno lingine,tuwache au tutoke dhambini. Sasa,hii dhambi ni nini,maana hatuwezi toka kwa kitu ambacho hatujui.Tukisoma katika maandiko,Mungu anatuambia kwamba, “dhambi ni kuvunja amri za Mungu- 1yohana.3:4”.(kwa maelezo zaidi,agiza ujumbe wetu uitwao,”Amri kumi”).Kila mtu mwenye kutengeneza bidhaa huwa,anapomaliza kutengeneza bidhaa yake,anaandika kijitabu chenye maelezo ya vile hiyo bidhaa inatumika.Hayo maelezo ndiyo huitwa sheria,ambazo kazi yake ni kuelezea hiyo bidhaa ni nini, na inatumika kwa njia gani.Kila wakati mtu anapoitumia hiyo bidhaa kinyume na hayo maelezo, huwa anaiharibu.Kwa neno lingine,ameikozesha utumishi wake ,na kwa hivyo anaiharibu.Kwa namna yiyo hiyo,sisi wanadamu ni bidhaa iliyoumbwa(tengenezwa) na Mungu.Alipomaliza kutuumba,aliziandika amri zake ambazo ni maelezo kwa wanadamu wote kuhusu vile wanapaswa kuishi,maana anatuambia kwamba hii amri ni,”uhai kwa wale wazishikao…”,ni mti wa uzima-Mithali.4:22;3:18”. Kwa maelezo tofauti,hii amri ni maisha ya wanandamu.Baada ya kumuumba mwanadamu,na kumpa maelezo ya namna ya kuishi(hizi amri),alimwuonya pia dhidi ya kudanganyika na kuyakataa hayo maisha mazuri,maana alimwonya hivi,”Lakini utakapokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya,hakika,utakufa-Mwa.2:17”(Agiza ujumbe uitwao,”Miti miwili” kwa maelezo zaidi). Tunaelewa kwamba,Adamu alikubali uongo wa Shetani na hivyo akala(kukubali na kuishi maisha ya shetani) yale matunda yaliyokatazwa.Kwa hivyo,alivunja amri za Mungu.Akaanza kujitumia(kuishi) kinyume na vile aliumbwa ajitumie. Hii ndiyo sababu tunaona leo maisha yakiwa na matatizo,na shida za kila aina,maana hatufuati yale maelezo kutoka kwa muumba wetu, ya jinsi tunavyopaswa kuishi. Mwishowe,Mungu alimtuma mjumbe wake aitwaye Yesu Kristo,akaja akiwatangazia wanadamu wote yale maisha walidanganywa na Shetani wakayaacha.Kila anayeyasikia haya matangazo(habari njema),anaambiwa,”Tubuni,mkaiamini injili(matangazo)-Marko.1:15”.Ndugu zangu,huku ndiko kutubu.Ni kuwacha kuishi haya maisha ya sasa ambayo mwanadamu aliyasoma kwa shetani,na kuamua kuishi haya ya Mungu anayoyafundisha Yesu.Huku kukubali,ndiko kunaitwa kuamini.Hii uwezekana tu wakati mtu ameelewa vizuri sana na kukubali kwamba haya maisha ya shetani ambayo ndiyo ulimwengu mzima unafuata ni ya uongo,na ndio sababu mtu anaamua kuyaacha.Akisha fikia huo uamusi,Bwana wetu Yesu anaamrisha hivi;

                                                         MBATIZWE

Ikiwa mtu ameamua na kuwacha kuishi vibaya,ya nini abatizwe? Eee,ya nini azikwe ndani ya maji? Zote tunakubaliana kwamba Shetani ndiye mfalme na mtawala wa Dunia hii,na ndiye mwenye haya maisha ambayo karibu watu wote wanaishi. Yesu alipokuja akiishi na kutangaza maisha ya Mungu,ambayo yanapinga haya maisha ya Shetani, alikuwa kama muasi kwa Shetani,na hivyo,shetani akaanza kupigana naye,mpaka mwishowe,akamuua pale msalabani.Mungu anatuambia kuwa,”Kristo alikufa kwa ajili ya wote waaminio- 2 Wakori.5:15”.Je wajua kwamba,kama Kristo angekubali kuishi kama wanadamu,asingeuliwa? Angekuwa amekubaliana na Shetani,kwa hivyo,Shetani hangekuwa na sababu ya kumuua.Lakini kwa sababu alimpinga Shetani,kwa sababu alisema hawezi kuishi kwa dhambi,basi alikuwa hai kwa maisha ya Mungu,na akawa ni kama mtu amekufa kwa maisha ya shetani kwa sababu, hayaishi kamwe.Hii ndiyo maana ya ubatizo,maana,”..Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi,basi dhambi haina nguvu tene juu yake;yale maisha anaishi,anaishi kwa Mungu-Warumi.6:10”. Basi,vivyo hivyo,wakati mtu ameamua kuishi maisha ya Mungu yaliyo katika kristo Yesu,yeye uyawacha kabisa haya ya ulimwengu,na uwa kwa ulimwengu,ni mtu amekufa,maana,uhesabiwa kama,”amekufa kwa ulimwengu,na ulimwengu umekufa kwake-Wagal.6:14”.Sasa,Mtu akikufa,ufanyiwa nini? Si huwa anazikwa? Na vivyo hivyo,kila anayeamini, uzikwa ndani ya maji,hii ikiwa ni onyesho,au ishara ya,”wakati mlibatizwa katika Kristo Yesu,mlibatizwa katika kifo chake.Kwa njia ya huu ubatizo,tumeungana naye katika kuzikwa kwake(kufa)……ili,kama alivyofufuka,nasi pia tujiisi kufufuka pamoja naye,ili tuishi maisha mapya(yale ya Mungu)-Warumi.6:3-4”.Tumeelewa hapo? Tumeyakataa maisha ya shetani.Tumesema; “kama maisha ni haya ya shetani,basi mimi sipo,nimekufa;naweza kuishi tu ikiwa nitaishi maisha ya Yesu,vile yeye aliyakataa ya Shetani akaishi yale ya Mungu”. Mtu akiisha fikia huo uamuzi,basi yeye uthibitisha uamuzi wake kwa kuzikwa(kubatizwa)ndani ya maji(kaburi). Kama mtu yeyote anasema amebatizwa,na hakuzikwa ndani ya maji,basi huyu anajidanganya na wala haelewi maana ya hili neno-ubatizo.Tukisha fikia hiyo hatua,basi tunakuwa tuko tayari kuanza kujifunza kuishi kama Yesu Kristo. Lakini hapa,tunagundua kitu kingine ambacho kinatufanya tusiweze kuishi kulingana na uamuzi wetu.Bwana wetu Yesu anatuambia kuwa,”mtu wa mwili wa nyama,hawezi kuyaelewa maisha ya kiroho,na wala hawezi kuyatii- 1 Wakori.2:14;Warumi.8:7”.Kama ni hivyo basi,tutawezaji kuishi maisha ya uamuzi wetu na sisi ni viumbe wa nyama na damu?

                                           KUBATIZWA KWA ROHO

Bwana wetu Yesu Kristo anayaelewa hayo yote,maana hata yeye anatuambia kwamba,”..bila mimi,hamwezi chochote-Yohana.15:5”.Hii ndiyo sababu,aliahidi kwa kinywa cha Petro wakati huo wa pentekosti akisema,kuwa,mkiamini na kubatizwa kila mmoja kwa jina la Yesu,”….mtapokea roho mtakatifu-Matendo.2:38”.Maisha ya kiroho,uwezekana tu kwa mtu aliye na roho ya Mungu.Kwa hivyo,tukisha zikwa(batizwa kimwili),ni lazima tena tuingizwe ndani(tubatizwe kwa roho) ya roho ili,”..atuongoze katika kweli yote-Yohana.16:13”.Kwa sababu hizi sheria za Mungu ni za Kiroho-ona Warumi.7:14, ikiwa tutazishika(kuishi vile zinasema),basi ni lazima tuongozwe na huyu roho,maana,”zinawezekana tu kwa wale waongozwao na roho takatifu-Warumi.8:4”. Hii ndiyo maana ya kubatizwa kwa roho. Mtu akisha zikwa ndani ya maji(kaburi),yeye utoka kwa maji(ishara ya kufufuka),halafu kutoka hapo,kwa njia ya kuwekelewa mikono,anabatizwa(zikwa ndani ya) kwa roho. Kuanzia hapo,anawacha maisha ya kuenenda kimwili na kuanza hayo ya kiroho.Hapa ndipo ubatizo unakamilika,na ndipo pia mtu anaitwa mkristo.Kabla mtu hajabatizwa,na kuwekelewa mikono,huyo huwa sio mkristo,maana huwa bado hajapokea roho ya Mungu.Wengine ambao  ,” ……upenda kugeuza amri ya Mungu ili iwafae wao-Zephania 3:4” watasema kwamba kornelius walipokea roho kabla hawajabatizwa;hivyo watajaribu kusema ubatizo si lazima na hauna umuhimu.Angalieni mtu hasiwapotoshe kwa mdomo mtupu utokanao na akili ndogo isio ya kimwili.wakati ule petro alitumwa kwa koneliasi,wayahudi walikuwa hawachanganyikani na wamataifa.Kwa hivyo,ilimbidi Mungu abomoe huo ukuta kwa kuwapa mataifa roho sawa na wayahudi.Hi iliwazaidia kuelewa kwamba, “ …Mungu amewapa mataifa  kutubu kama sisi pia-Matendo.11:18”. Hata vivyo,baada ya kupokea roho,walibatizwa pia,maana, “aliagiza wabatizwe kwa jina la Yesu-Matendo.10:48”.Tangu hapo,wote waliopokea roho takatifu ilikuwa ni baada ya ubatizo na sio kabla.Kwa akina koneliasi,Mungu alifanya hivyo ili kuwaunganisha waumini wa kiyahudi na wa mataifa,kusiwe na utofauti katika kanisa lake.Kristo anatuambia kuwa,”ikiwa mtu hana roho ya Kristo,huyo si mkristo(wa Yesu)”.Maana ni wale tu waongozwao na roho wa Mungu ambao uitwa wana wa Mungu-Warumi.8:9,14”. Yohana alituambia kuwa,Kristo atatubatiza kwa,”….maji,na kwa roho,na kwa moto-Mat.3:11”.Kufikia hapa,tumebatizwa kwa maji,na kwa roho. Sasa je,huu ubatizo kwa moto nao uja lini, na kivipi?

KUBATIZWA KWA MOTO

Wandugu.Mmeona mara nyingi tukishauri watu wawe na uhakika kwamba wanajua kile wanafanya.Ubatizo sio jambo la kukimbilia.Ni kitu ambacho mtu akishaa fanya,hakina kurudi nyuma.Ni kwa nini nasema hivyo? Sisi zote ni watu ambao tumepitia haya maisha ya uongo ambao Mungu alikuwa ameonya Adamu vizuri sana.Alimwelezea wasi kwamba,akiyafuata,hakika atakufa.Watu wengi,karibu wote, mpaka dakika hii wanayaishi na hawajui kama ndiyo yaletao kifo.Wanaishi maisha yenye matatizo ya kila aina,lakini hawaelewi kwamba yanauja kwa sababu maisha yenyewe sio yale waliumbwa waishi kwayo. Lakini kwa kila mtu ambaye amepewa kuelewa huu ujumbe wa Yesu,na akafikia kuukubali mpaka akabatizwa,huyu ni mtu ambaye macho yake yamefunguliwa,na akajua alikuwa akiishi vibaya.Hii ndio sababu aliamua kutubu,yaani,kubadilisha maisha. Tunajua vizuri sana kwamba,Mungu hawezi kusema uongo.Na pia,hawa wote ambao wamebatizwa, ni watu ambao, “wamepewa kuzijua siri za ufalme wa Mungu-Mat.13:11”.Wanajua kuwa uovu wote utokana na haya maisha ya awali.Kwa hivyo,wanajua kwamba wakiwacha haya maisha ambayo walibatizwa ndani yake na kurudia haya ya uongo, watakufa. “Yesu hakujitoa sadaka mara mingi;maana hiyo ingemaanisha,ateseke mara nyingi……..lakini sasa,alijitokeza mara moja tu akawa sadaka kwa ajili ya dhambi.Kwa hivyo,kila mtu ni lazima afe mara moja.Kwa namna hiyo, Kristo pia alitolewa kuwa sadaka kwa wengi mara moja tu-Waebra.9:25-29”.Sasa tuelewe vizuri.Mtu akibatizwa huwa amekufa  na kuzikwa kwa ajili ya dhambi mara moja tu. Haiwezekani afufuke, tena afe mara nyingine. Kwa hivyo,ikiwa mtu atapokea roho takatifu,ambapo itamwezesha kuelewa na kuyaishi maisha ya kiroho,halafu baada ya hapo,ayakatae na kurudia maisha ya Shetani,hiyo itakuwa ni kama kusema,maiti imefufuka baada ya kukaa kaburini,na imerudia yale maisha yaliifanya ikufe.Hapa,mtu huwa anathibitishia Mungu kwamba yeye hataki kuishi;anataka kufa.Pia,anaonyesha kwamba hataki kuokolewa na Yesu.Kwa hivyo,anaonyesha kwamba,hata kama Yesu angeamua kumfia tena,atakataa,na,”….anaweza hata kumsulubisha mara ya pili”.Na kwa vile,”Hakuna mwingine au jina lingine lipaswalo wanadamu kuokolewa kwalo isipokuwa Yesu-Matendo.4:12”, na huyu mtu amemkana  baada ya kujua uzuri wa yale maisha ya Mungu,”basi haiwezekani kuwaleta tena kwa toba,maana hii ni kama kumsulubisha Yesu mara ya pili-Waebr.6:6”.Huyu ndiye Yule usemekana kwamba amefanya dhambi ya kukufuru,na hawezi kusamehewa maana ata yeye hataki msamaha.Hii inambidi Mungu aheshimu uamuzi wa huyu mtu ,maana,”Mungu utimiza nia ya mioyo yetu-Zab.37:4”.Na kwa vile alituumba tukiwa viumbe wenye uhuru wa kuchagua,basi,kile mtu uchagua ndicho Mungu ampeacho,maana,”mtu akipanda kwenye tamaa za mwili,atavuna kifo;akipanda kwa roho,atavuna uzima wa milele-Wagal.6:8”.Basi,huyu mtu amepanda kwenye mwili,kwa hivyo,hakuna njia nyingine,”…ila kungojea kwa woga ile hukumu ya moto mkali utakaowaangamisa wote wale wampingao Mungu-Waebr.10:27”.Itakuwa basi,hapo Yesu atakaporudi,”kila mtu ambaye jina lake haijaandikwa kwenye kitabu cha uzima atatupwa kwenye ziwa la moto-Ufunuo.20:15”.Kama wakitupwa ndani ya moto,si wataingia ndani mpaka moto iwafunike? Wandugu wapenzi,huu ndio ubatizo wa moto na ni kwa wale watakaokuwa wamemwasi Mungu baada ya kupewa nafasi ya wokovu,wakajua ukweli,wakauishi,na baada ya hapo,wakaukataa.Hapa ndipo ukamilivu wa kifungu chetu utatimia-yaani, “ubatizo kwa maji,kwa roho,na kwa moto”.Wale wanaobatiza wengine kwa moto,kwa kuwapitisha chini ya bendera nyekundu,waelewe ule uovu wanawatakia waumini wao,maana ni kama kuwaingiza kwenye ziwa la moto. Nafikiri kufikia hapa,unaona na kuelewa ni kwanini huwa tunatahadharisha watu wasikimbilie ubatizo.wauelewe vizuri na kuamua kwa ufahamu,maana,”nafasi ya wokovu ni moja tu,na wakati huwa mmoja tu,ambao ni pale mtu anapobatizwa na kupokea roho takatifu-2 Wakor.6:2”.Naamini kila mwenye kutaka ubatizo ameelewa, na sasa,ako tayari kuchukua uamuzi.Pia kwa wale wameshaa batizwa,naamini mmepata ukumbusho.Ni ombi letu kuwa tutajikabithi kwa mungu kwa mioyo yetu yote,ili aishi maisha yake ndani yetu,katika Kristo yesu,ili,”..maisha tutakayoishi yawe si yetu mbali ni ya yeye Yesu alietufia- 2 Wakori.5:15”.Neema ya Mungu na iwe kwa wingi ndani ya wote walio Israeli wa Mungu-Wagal.6:16. Je,unahitaji maelezo zaidi kuhusu haya maisha ya Mungu yalio katika Kristo yesu? Sisi ni watumishi wake walio tayari kushirikiana nawe,na kukujulisha yote yale ambayo Bwana wetu Yesu Kristo ametufunulia na kututuma tuwajulishe wote wamtafutao.Ongea nasi kupitia kwa, KANISA LA MUNGU.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *