ZAKA, NANI AWAJIBIKAYE?

Katikati ya kipindi cha waleodikia, watu ambao wana akili za shauku, ambao hawana uhakika wa kile walipokea kwa Yesu, ambacho ndicho wanapaswa kuamini, wengi kati yao wanadhania mambo kuhusiana na vile wanapaswa kumwabudu Mungu, na vile wanapaswa kumtumikia. Hivyo, wamefikia kufanya, “ kile wanachoonelea kuwa chema machoni pao-Mith.14:12”. Kwa hivyo, “ kila mmoja anatenda kulingana na akili yake isivyo na ufahamu inavyomtuma- Yerem.18:12”. Huku wakikosa kudhamini ile taa(Zab.119:105,9-10) ya pekee ambao ndiyo inapaswa kuwamlikia na kuwachunga katika njia zao, Kila mmoja amealalisha kile anachodhania kuwa sawa, na yeyote anayejaribu kuwajia na ukweli huwa anasemekana kujifanya hakimu, na huwa anatengwa na wao. Lakini wandugu, tuelew kwamba, kukataa kwao hakuifanyi neno la Mungu kuwa mbaya, maana anasema, “Mimi nachunga neno langu ili niitekeleze-Yere.1:7”, na tena, “ nimesema na nitatenda, nimekusudia, na nitatekeleza, asema Bwana-Isa.46:11”. Najua, haya mafundisho ya  ukweli mtupu hayapendwi na wengi; inachukulia kuwa kikwazo, ila, wakati umefika wa kuelewa kwamba, neno la Mungu haikaribishwi na akili ya kimwili, maana ni, “ uadui kwake-Warumi.8:7”. Kwa hivyo, yeyote atakaye kuusoma na kuuelewa huu ujumbe, na lazima ajikane kwanza-Mat.16:24. Hapo kila mtu atakapojikana, zote tutabakia na akili tupu, ambazo ziko tayari kusoma upya kutoka kwa Mungu ambaye peke yake ndiye mwenye ufahamu wa kwelMat.18:2, na ambaye atatuumbia ataiumba akili yake ndani yetu-Yerem.31:33. Hii itatufanya tuwe kitu kimoja, tukikubaliana katika kila jambo-Waef.4:3-6. Hali tukiyaelewa hayo, hebu kila mmoja ageuke na kujangalia ndani, kwa ajili ya kuuchunguza moyo-2 wakor.13:5, ili kudhibitisha kama kumcha, na kumtumikia Mungu kwake ni kwa kweli ama amedanganyika huku bado akiendelea na dhana zake za uongo. Basi sasa, hebu turudi kwa swali letu. Ni nani anayefaa kuwajibikia zaka na sadaka zitolewazo kwa kanisa la Mungu?Ni kila mshirika wa kanisa? Jibu ni ndio kwa njia mmoja, na la kwa njia nyingine. Ni yule anayewafundisha watu na hivyo, kuwaangiza walete hizo zaka kwake? Jibu hapa pia ni ndio kwa njia moja, na la kwa njia nyingine. Ninamaanisha nini, la na ndio? Hebu tupate maelezo kutoka kwa yeye aliye amrisha huo utoaji.

MUNGU NDIYE MWENYE VYOTE

Mungu tunayeongea juu yake hapa ni yule, “ aliyeziumba mbingu, nchi, Bahari na vyote vilivyomo- Nehem.9:6”, “ ambaye, vitu vyote ni watumishi wake-Zab.119:91”, Na aliye na uwezo juu ya vyote kiasi kwamba, anapoziita, zote uja mbele zake-Isa.40:26”. Kwa hivyo, ni Mungu ambaye, “ndiye uwapa wanadamu uhai, pumzi na vitu vyote-Matendo.17:25”. Hii ndiyo sababu anasema, “Vitu vyote, mikono yangu iliumba, na kwa hivyo, hivi vyote ni vyangu, asema Bwana-Isa. 66:4”. Fedha ni yangu, na dhahabu pia ni mali yangu-Hagai.2:8”. “ Kwa hivyo, kama ningelikuwa na njaa, singewaambia; maana ulimwengu wote, na vyote vilivyomo ni vyangu-Zab.50:12”. Kama ndivyo basi, kwa nini anataka watu walipe zaka na sadaka? Kwa nini aangize kuletewa kilicho chake tayari? Wandugu, inatupasa kuelewa kwamba, Mungu ufanya kila jambo kwa kusudi Fulani, na utoaji wa zaka ni baadhi ya mengi anayofanya. Kwa hivyo tunajiuliza, ya nini kutoa zaka? Mungu tangu mwanzo amekuwa akiwatumia wanadamu, kutumikia wenzao kulingana na mapenzi na kusudi lake kwao. Tunajua kwamba, baada ya mwanadamu kudanganywa, Mungu alianzisha mpango wa kumjulisha kuhusu huo uongo huku akimfundisha maisha ya kweli-Isa.42:6-7. Angu vizazi vyote, Mungu amekuwa na watu katika kila kizazi kuhakikisha huu ukweli umesikika kwa wote kila wakati. Zote tunaelewa kwamba, kilichojaa katika akili ya Mungu sasa hivi, ni kuurudisha ufalme wake hapa duniani, na kuwa sis wanadamu tuliumbwa kwa ajili ya huo. Lakini, ili tuweze kufanya hivyo, ni lazima kwanza tujifunze kuishi haya maisha yake, ambapo, baada ya kufaulu, atatupatia hayo maisha milele. Tunapoangalia tabia za hayo maisha, tunaona kwamba, Mungu  wakati wote huwa upande wa kupeana. Hakuna wakati ambao Mungu huwa akitarajia kupewa. Hivyo, tuko sawa kusema kwamba, msingi wa maisha ya Mungu ni hali ya kupeana- kuwashughulikia wengine.

HUDUMA YA BURE

Kwa vile tunajifunza kuishi kama Mungu, na kila atufanyaiacho huwa ni huduma bila malipo yoyte, basi, yeyote afauliye kuishi kama Mungu, ni lazima ajifunze kuishi hayo maisha ya kupeana bila kutarajia malipo yoyote, eee, kuhudimia bila masharti yeyote, kama namna yake ya kuishi. Hii ndiyo sababu, Mungu anapowateuwa watumishi wake, anawaambia hivi, “ mlipewa bure, kwa hivyo, peaneni bure-Mat.10:8”. Hiyo itawezekanaje na tuko katika huu mwili unaohitaji vitu, ambavyo ni lazima vitokane na huduma tunazopeana, na hata yeye mwenyewe anajua tunaviitaji-Mat.6:32? Basi, ikiwa mtu ameitwa kwa huduma ya namna hii ninayofanya ambayo ni ya hali ya kikuhani, ambayo mtu anahitajika kujikabidhi kikamilifu, atapataje mahitaji ya hivi vya kimwili, na huku anahudumu bure kulingana na maagizo? Mungu anaposema, ulipewa bure, kwa hivyo, peana bure, huwa anaongea na kila mtu, sio wanaohudmia wengine kwa njia hii peke yao. Kwa hivyo, kwa kuwa  kila kitu ni mtumishi wake-Zab.119:91, , kila mtu chochote alichonacho, ,inamaanisha ni Mungu umpa kila mtu kile anachopeana, maana imeandikwa, “ Mkaribishane nyinyi kwa nyinyi pasipo kunungunika; kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu. Mtu akisema na aseme kama mausia ya Mungu;  mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili kwa kila jambo, Mungu atukuzwe-1 Petro.4:9-11”. Nimesikia mara nyingi, wengine wakisema eti vitu vya wandugu; je, wanaongea sawa, ikiwa tutaishi katika hii hali ya kiroho, hii ya kupeana, na sio hii ya kimwili ya kupokea? Nasema hapana. Kwan in? Kwanza, tuelewe kwamba, hii dhana ya kwamba eti hili agizo la kupeana bure ni kwa wahubiri peke yake, ni uongo, kwasababu kanisa lote( washirika) ni mwili mmoja wenye kila kiungo kikitekeleza kazi yake, hivyo, kila mmoja ni mhudumu kwa njia moja au nyingine. Hali tukielewa hivyo, hebu tuje kwa hizi huduma zitegemeazo vipawa, tukikumbuka kwamba vyote ni vya Mungu amewapa watu bure. Wandugu, sio vizuri tuendelee bila kupata mfano kutoka kwa wale waliotutangulia kuishi haya maisha ya Mungu-Waeb.12:1. Hebu tumsikilize mmoja wao akiongea kuunga mkono yale tunayojifunza hapa. “ Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe, tumekutole1 Mambo nyakati.29:14”. Anayeongea hapa ni Mfalme Daudi. Je, anazungumzia kuhusu hawa anaowatawala peke yao, huku akiendelea kuwaagiza wamletee vitu, awe upande wa kupokea bila yeye kuwa baadhi ya watoaji? Hasha ata kidogo, maana alijua anachokiongea ni cha Mungu ambaye uwaagiza watu wote, akianzia na anayewafundisha wengine-Warumi.2:21. Msimamo hapa ni, kulingana na kipawa cha kila mtu, iwe ni anayeongoza au wanaoongozwa, kila mmoja anapaswa, “Kumjua Mungu muumba vyote, na kumtumikia kwa moyo wake wote, na kwa  akili ya kujitolea- 1 m. nyakati.28:9”. Ijapokuwa hapa Daudi alikuwa akizungumza na Suleimani, hayo maagizo yalikuwa ni kwa wote, maana tunaona kila mtu hapa akitii hali hiyo hiyo kwa, “… kwa utumishi wote wa nyumba ya Mungu; nao watakuako pamoja nawe kwa kazi ya kila namna, kila mtu mwenye hiari, aliye stadi kwa utumishi wowote-1 m. nyakati.28:21”. Ndio, wote wanakubali kuwa, akiba hii yote tuliyoiweka, ili tukujengee nyumba kwa ajili ya jina lako takatifu, yatoka yote mikononi mwak1 M nyakati.29:16. Kwa hivyo wandugu, ni muhimu kuwa kama wazazi wetu wa kiimani, la sivyo, tutamwabudu Mungu bure- Marko.7:6-7. Hapa, tumethibitisha kuwa, hivi vitu tunavyopatiana katika kila huduma ya aina yoyote ile, si vyetu bali ni vya Mungu. Kwa hivyo, kwa kupeana bila malipo, tunajifunza tu kutumia hivyo vitu aliotupa, kufanya vile tunaona akifanya, ili tuwe kama yeye-Yohasna. 5:19.

ZAKA NI ZA MUNGU

Kama ilivyokuwa wakati wa agano la kale, ndivyo inaendelea kuwa wakati huu wa agano jipya, maana,  Jana, leo na hata milele, Kristo ni yeye yule-Waeb.13:8”. Kwa vile chochote kile kijaacho akilini mwa Mungu ni kuurudisha ufalme wake hapa duniani, ikiwa pia ndio kusudi lake la kutuumba, basi kila jambo afanyayo Mungu kuhusiana na wanadamu, na kila mwanadamu afanyacho kuhusaiana na huduma kwa Mungu, inalenga kutimiza hilo kusudi. Huo mpango sasa hivi huko kwenye hatua ya kuumba akili na tabia ya Mungu ndani ya hao watakaotawala katika huo ufalme-Waeb.2:5-7( ujumbe wetu uitwao, “ Mchakato wa uumbaji wa mwanadamu”, unamaelezo ya kina). Kwa sababu hii, chochote mwanadamu afanyacho katika kumtii Mungu kinalenga kumjenga kumfikisha kwenye hioyo goli, maana, “ maandiko ni ya kumfundisha, kuomwonya makosa, kumwongoza, na kumwadabisha katika haki, ili mtu wa Mungu awe mkamilifu, katika kutenda kila tendo njema-2 Tim.3:16-17”. Ikiwa hatujafahamu, natufahamu sasa. Na kama tumekwisha fahamu, na tukumbuke, kwamba, sis wa kanisa la Mungu ni watu ambao Mungu amechagua, na akawakabidhi kazi ya ujenzi wa hekalu lile lile Suleimani alikabidhiwa kujenga mwaka mingi iliyopita, ambayo baada ya kuharibiwa, Mungu alimkabidhi Zerubabeli kulijenga upya-Zekaria.4:1-6, ambayo aliwaamrisha watu wa wakati huo akisema, “pandeni milimani, mkalete miti, mkaijenge nyumba; name nitaifurahia, asema Bwana-Hagai.1:8”. Wapenzi, inatupaswa kuelewa jambo hapa tafadhali. Japokuwa Mungu anawachagua  na kuwaamrisha watu kutenda kazi yake, yeye halazimishi yeyote, maana hufurahia, kazi ya hiari. Kwa wale ambao wanasikia na kutii kwa hiari yao, Mungu uwapa kile wanachohitaji katika hiyo kazi, na pia uwatumia wale watu wenye ujusi wa kila aina ili, “…. Na mtu yeyote…. Na azaidiwe na watu wa mahali pake, kwa fedha , dhahabu, mali na wanyama, Zaidi ya vitu vitolewavyo kwa hiari ya mtu-Ezra.1:4”. Ni nyumba hii hii ambayo kuihusu, Mungu anasema, “utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza-Hagai.2:9”. Kwan in uwe mkuu kushinda wa kwanza? Tukikumbuka kwamba Mungu ameumba vya kimwili vimwezeshe mwanadamu kuelewa vizuri vile vya kiroho- Warumi.1:20-21, na kwamba chochote alichokifanya katika agano la kale kinalenga kile anachotaka kutimiza ndani ya mwanadamu, ambacho ni kumfanya kiumbe wa kiroho ili aweze kuutawala ufalme wake-Mwa.1:26; Waeb.2:5-7, Basi, ukuu wa hii tunayoijenga sasa hivi unategemea ile hali yake ya kiroho, kwa kuwa, ni utimilivu wa kile Mungu alianzisha tangu kuumbwa msingi ya dunia. Akikiongelela, Bwana anatuambia, “… mambo ya wakati huu sio kitu yakilinganishwa na utukufu utakaofunuliwa kwetu-Warumi.8:18”. Basi, kwa vile tumepata picha ya kile tumeitiwa kujenga katika huu mpango wa kumhudumia Mungu sasa, hebu sasa turudie ujumbe wetu. Kanisa la kweli la Mungu ni watu ambao, baada ya mjengo huu wa kiroho( washirika) kuvaamiwa na mbwa mwitu-Matendo.20:29-31, na waumini kupelekwa uhamishoni katika Babeli ya kiroho(Leodikia), hawa wa sasa hivi ni wale wamesikia witu wa Kristo wa kupanda milimani na kulete miti( kwa wao wenyewe kurejea katika msingi, ambao ni maisha ya kweli ya kiroho, na kuwa mfano kwa wengine) ya kujenga hii nyumba upya-Hagai.2:9.

                               MUGNU NDIYE ANAPEANA BIDHAA ZA UJENZI

Kwa kuwa kazi yetu wakati huu ni kuumbika akili na tabia za Mungu, na Mungu amewateuwa watu( kanisa lote) kuifanya hiyo kazi, basi amewapa kila mmoja( kipawa) kile anahitaji kuchangia huo ujenzi. Hivyo basi, tutaenda mlima gani ule ambao tutapata hii miti ya kiroho? Mungu uagiza kila mmoja wetu akisema, “Leteni zaka na sadaka katika gala langu, ili kuwa na chakula katika nyumba yangu-Malaki.3:9”.Mtu yeyote ambaye hatii hii amri, Mungu anamuita, sio mwizi tu, lakini, myang’anyi_mal.3:9. Basi Je, hii zaka ni mtu yeyote yule? Je, ni mali ya yule anayemtolea Mungu?  Hasha ata kidogo, maana tumeona vile sisi wote tunapeana kile ambacho ni cha Mungu ametupa.  Basi ni makosa kwa mtu yeyote kusema ni zaka ya washirika, jambo ambalo mara nyingi imeleta utata kanisani, kila mtu akitaka kujua pesa yake inavyotumika.  Ni makosa pia kwa mtu kudhania eti amempa mchungaji. Kila mtu uipeleka kwa Nyumba ya Mungu, ee, kwa Mungu, ambapo, ni Mungu umpa yule aliyemchagua yeye mwenyewe. Katika agano la kale, Mungu aliwateuwa makuhani wawe wahudumu kuwatumikia makutano ya Waisraeli( kanisa la wakati ule). Halafu anasema,  Na wana wa walawi, nimewapa( sio mwanadamu awapaye mbali ni Mungu) zaka yote katika Israeli( kanisa) iwe urithi wao, kwa huo utumishiwautumikiao-Hesab.18:21-22. Katika huu wakati wa kiroho, hekalu la Mungu ni miili ya waumini wa kanisa ambako Mungu kwa njia ya roho yake, anakaa-1 wakor.6:19; 3::16. Hii ni kwasababu, wakati mtu anapobatizwa, Mungu na Kristo huja ndani ya roho ya huyu mtu na kufanya makao yao humo-Yohana.14:23. Hii ndiyo sababu Yesu anasema kwamba, unapompokea yeyote aliyemtuma, unampokea kristo mwenyewe-Mat.10:40. Kwa hivyo, gala la Mungu wakati huu, ambako tunapeleka zaka za Mungu, ni watu ambao Mungu amewateuwa, na kuwapa kipawa cha makuhani ili, kutoka kwa vinywa vyao kupatikane maagizo ya Mungu, maana midomo yao uchunga maarifa, ili watu watafute ufahamu kutoka kwao-Malaki.2:6-7. Kwa vile sis sote tumeitwa katika Kristo, nay eye sasa hivi anakuja kupitia kwa wale anaowatuma-Wagal.2:20, basi, hawa watu ndio gala za kiroho za Mungu, ambako zaka inapaswa kupelekwa, maana ndio Mungu amewapa zaka zake, kwa kuwa anasema, na yule afanyaye kazi ya kuhubiri injili, imempasa kupata chakula chake katika injili-1 Wakor.9:14. Maana kwa kweli, ikiwa mafundisho tunayopata kutoka kwa hao ambao Mungu ametuma, yanatupatia kile tunachotafuta, na kutujenga,  ni jambo nzito kwa wao kuvuna kutoka kwetu- 1 wakor.9:11? Bwana wetu anaamrisha kwamba, yeyote afundishwaye neno, imempasa kumshirikisha mwenye kunfundisha kwa mema pia-Wag. 6:6. Sasa basi, hali tukiyafahamu hayo, hebu tujibu swali letu sasa. Ni nani anapaswa kuwajibika kwa zaka za Mungu? Ni Mungu, sio mwanadamu yeyote. Baada ya Mwanadamu ameipeleka zaka kwa nyumba ya Mungu, Mungu naye uwakabidhi aliowachagua hiyo zaka. Lakini pia, ni wajibu wa kila mshirika. Kwa njia gani? Elewa tafadhali.

TUMEKUSANYIKA NDANI YA KRISTO

Tafadhali, hebu na asomaye aelewe. Huu ujumbe ni kwa wale wanaotaka kufanya ukweli kuwa, fikira, nia, , ndio, wale ambao hawana chochote kile cha kujitakia isipokuwa kufanywa miungu kama kristo mwenyewe; na ambao wanayatafuta maisha ya Mungu kwa mioyo yao yote, na akili zao zote, hali ambayo haiwezekani kwa mtu mwenye ubinafsi wa aina yeyote ile. Hii nasema kwasababu, yeyote mabao haitoi roho yake yote kwa kristo, atakuwa na sehemu ndani yake ya ubinafsdi, ambao hauwezi kutii Mungu-Warumi.8:7. Mtu wa aina hiyo atakakuwa saa yote anatafuta njia ya kupinga neno huku akihalalisha fikira zake mwenyewe, na kubishana saa yote. Hali tukiwa na huu ufahamu, hebu basi turudi kwenye mada yetu. Kristo anasema, popote ulipo mzoga, hapo ndipo tai ukusanyika-Mat.24:28. Kwa hivyo, ni wajibu wa kila mshirika, kwa maombi makali, na kwa uchubnguzi wa ndani sana, kutatufat na kujua mahali kristo anapofanyia kazi yake, kupitia kwa aliyemchagua. Ni jambo la kuhusunisha kuona vile washirika wa kanisa leo  hawawezi kuthibitisha aliko Kristo, ilhali Bwana mwenyewe anasema kwamba, mtu wa kiroho huyachunguza mambo yote-1 wakor.2:15. Ni kwa nini basi iwe vigumu kwa mtu kuelewa mahali kristo anakofanyia kazi? Sababu inaweza kuwa tu kwamba, tumemfinyilia roho ya Bwana kiasi cha kutoipa nafasi ya kutawala akili zetu, huku tukiruhusu roho ya kimwili kuchukua nafasi yake. Tunaelwa kwamba huyu roho wa kimwili kwamba, sio eti hawezi kumtii Mungu tu peke yake, bali, pia, hawezi kufahamu mambo ya kiroho-Warumi.8:7; 1 Wakor.2:14, na hivyo, imfanya mtu kutoamini samecho Mungu katika neno lake. Sasa hivi, kanisa la Mungu tumekuwa hali ile ile waliokuwa mafarisayo, katika upofu wa akili kiasi kwamba, ijapokuwa, walikuwa na neno lililo sema mambo ya kristo midomoni mwao, hawakumfahamu alipokuja. Lakini hilo halikufanya neno la Mubngu kuwa uongo. Hii ndiyo sababu Kristo anatuambia, ikiwa mapenzi ya mtu ni kufanya mapenzi ya Mungu, basi ataweza kuelewa kama mafundisho yangu ni ya Mungu ua, nanena yaliyo yangu mwenyewe-Yohana.7:-16-17. Wandugu, haya nasema katika Bwana kwamba, mshirika wa kweli wa kanisa la Mungu huwa saa yote anajua mahali Yesu yuko, maana ni mtu anaijua sauti yake, na anajua tofauti yake na zile zingine-Yohana.10:27,5. Wapenzi, kwa neno la Mungu isiyopubguzwa wala kuongezewa kitu, ambao, mfuasi wa Yeus atajua mahali yeye yuko, maana imeandikwa, mtumishi wa Mungu unena neno la Mungu( na mshirika pia- yohana.8:47)-yohana.3:34. Hapa ndipo wajibu wa mshirika katika zaka ya Bwana unakujia. Basi, tukishaa thibitisha mahali mtumishi wa kristo wa kweli alipo, hapo ndipo tunapeleka zaka zetu kwa gala la Mungu( naongea ligha ya kiroho kwa wanaopewa kuifahamu)- 1 Wakor.2:14-15. Baada ya hapo, wajibu wao unaisha. Tumeipeleka zaka la Mungu kwake mahali tumepaelewa kwa kusikia neno lake likitoka kwa mtumishi wake. Kutoka hapo, unakuwa wajibu wa Mungu kumpa huyo mtu hiyo zaka, naye uwajibika kwa Mungu, sio kwa washirika wenzake, maana Mungu anasema, lakini wasiulizwe habari ya hizo hela wanaokabidhiwa, maana wanatenda kazi kwa uaminifu-2 Wafalme.22:7. Huu mpango hauwezekani katika Leodikia ambapo kila mtu amekataa agizo la kutokufanya kulingana na vile mtu afikiriavyo-Mith.3:5. Maana, ispokuwa Mungu katika Kristo anafanya kazi ya kuumba ufahamu wake ndani ya mtu, anayejaribu kwa nguvu zake anafanya kazi ya bure-Zab.127:1. Basi wandugu, ili tuweze kufikia huu ufahamu, ni lazima tuwe na kujitoa kikamilifu kwa mapenzi ya Mungu, maana asipotuumbia huo ufahamu, hakuna mwingine awezaye, ama, atafanya hivyo( ujumbe wetu uitwao, “ kazi ya Mungu”, na, “ kanisa la Mungu”, zinao maelezo Zaidi). Ikiwa kunao wakati ambao kanisa la Mungu linaitaji kujengwa, ni wakati huu wa Leodikia, maana tuko karibu kwenye kikomo cha kazi yote aliyoianzisha kristo, kama ilivyotabiriwa na manabii na mitume, mpango ambao Mungu aliuweka tangu kuumbwa msingi wa dunia, yaani kuurudisha ufalme wake hapa duniani. Huu ndio wakati ambao Mungu anatuambia kuwa, utkufu wa nyumba hii ya mwisho utakuwa mkuu kuliko wa ile ya kwanza-Hagai.2:9. Hii itawezekana tu kwa yule ambaye amejitoa na anayejibidiisha kwa moyo wake wote, kujifunza kukaa kama Mungu-Mat.5:48, mpeanaji pasipo masharti, jambo liwezekanalo tu, ikiwa huu ufahamu wa kweli humo mioyoni mwetu. Hii itamwacha kila mtu akitenda chochote atendacho kama anayesimama mbele za Mungu na sio mbele za mwanadamu, akitumia kipawa cha Mungu alicho nacho kama anavyopenda Mungu, hali akielewa kwamba ni cha Mungu na sio chake. Hii ndio sababu Bwana wetu anatuagiza kwamba, huu utendaji  usiwe wa machoni tu kama mtu anayesimama mbele za watu, bali  kama mtumishi wa kristo antendaye mapenzi ya Mungu kutoka moyoni-Waef.6:6. Je, wewe ni baadhi ya waliopewa kuyaelewa haya, ambao wameisikia hii amri?  Kama ndio, basi,  panda juu yam lima, ukalete miti ili nyumba ya Mungu ijengwe( roho za waumini), ili aweze kuingi na kuonyesha utukufu wake-Hagai.2:9. Mwenye masikio na asikie kile roho analiambia kanisa. Huu ujumbe unakujia kutoka kwake Kristo kupitia kwa mtumishi wake,

KANISA LA MWISHO LA MUNGU.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *